Tafuta

2024.07.19 Kardinali Parolin akiwa amefika Uaskofuni huko  Lviv (Leopoli). 2024.07.19 Kardinali Parolin akiwa amefika Uaskofuni huko Lviv (Leopoli). 

Kard.Parolin:Nchini Ukraine anapeleka ukaribu na Papa na kusali kwa ajili ya amani

Katika ziara ya Ukraine ya Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican ilianza na mkutano huko Lviv na wawakilishi wa mamlaka za kikanisa na kiraia aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Mwakilishi wake kwa ajili ya maadhimisho ya mwisho ya hija ya kitaifa ya Wakatoliki wa Kilatini wa Ukraine kwenye Mahali patakatifu pa Bikira Maria wa Berdychiv, itakayofanyika Dominika tarehe 21 Julai 2024.

Mariusz Krawiec – Lviv, na Angella Rwezaula - Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Balozi wa Vatican nchini Ukraine, Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas, aliwasili alasiri Ijumaa tarehe 19 Julai 2024 kwenye Curia ya Jimbo kuu Katoliki la Lviv, ambapo alikaribishwa na Mkuu wa Kanisa Kuu, Askofu Mkuu Mieczyslaw Mokrzycki na maaskofu wasaidizi Edward Kava na Leon Maly. Askofu Volodymyr Hrutsa, askofu msaidizi wa Upatriaki wa Lviv wa Kanisa Katoliki la Ugiriki, pia alishiriki katika mkutano huo. Walikuwepo pia Maksym Kozytskyi, mkuu wa utawala wa mkoa wa Lviv, na Andriy Sadovyi, meya wa Lviv.

Sala ya amani

Baada ya salamu fupi kwa waliohudhuria, mjumbe wa Papa aliacha maoni yake ya kwanza kwa vyombo vya habari vya Vatican. “Tukio la ziara hiyo linahusishwa na sherehe katika Madhabahu ya Maria ya Berdychiv. Kwa hiyo, ndiyo sababu iliyomfanya Baba Mtakatifu kunituma kama mwakilishi wake maalum, pia kwa ombi la Maaskofu wa Kilatini, kwa ajili ya kuinua mahali Patakatifu hapo kuwa na hadhi ya Basilika ndogo,” alieleza Kardinali Parolin, kuwashirikisha waamini juu ya maadhimisho hayo na sala hiyo ambayo, kwa asili, itakuwa ni sala ya amani kuliko yote, itakuwa ni sala ya kwaya inayoinuliwa kwa Mama wa Mungu, ili hatimaye aijalie amani nchi hii, ambayo Baba Mtakatifu daima anafafanua kama 'kuteswa', 'Ukraine iliyopasuka'. Na bila shaka, hali hii pia inanipa fursa ya kukutana na mamlaka ya nchi. Pia kwa sababu  daima kumekuwa, kwa muda, mwaliko wa kuja Ukraine katika hali hii ya vita,” alisisitiza Kardinali Parolin. Na kwa hiyo, baada ya sherehe za Dominika tarehe 21 Julai, kutakuwa na fursa ya kukutana na mamlaka kuanzia, naamini, na rais. Na bila shaka, hapo, nadhani, tutazungumza juu ya amani, kuhusu matarajio yanayowezekana ya amani ni nini.”

Ukaribu wa Papa

Zawadi ambayo Katibu wa Vatican amepeleka kwa ardhi ya Ukraine ni ukaribu wa Baba Mtakatifu: Ziara hiini kielelezo kimoja zaidi cha umakini ambao Baba Mtakatifu anaendelea kuwa nao katika nchi ya Ukraine. Na kisha matumaini yake makubwa ya amani kwamba “tangu mwanzo Papa alijaribu kutafuta njia za kufikia mwisho wa vita, kile ambacho hivi karibuni kimeitwa amani ya haki. Tulizungumzia pia kuhusu hilo huko Bürgenstock nchini Uswiss, wakati Kongamano la Amani lilipofanyika. Kwa hiyo, ukaribu, maombi na matumaini, kwamba njia zinaweza kupatikana kufikia hitimisho, haraka iwezekanavyo, la mgogoro huu.”

Kujitolea kwa amani ya haki

Tena kwa niaba ya Papa Francisko, Kardinali Parolin kwa mara nyingine tena alionesha wasiwasi wake kwa hali ya Ukraine na kusisitiza kujitolea kwake kutafuta suluhisho la amani ili kufikia amani hii ya haki ambayo nimeizungumzia. Akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican alieviambia kuwa: “Hadi sasa imeonekana kwetu, pia kuanzia ziara ambayo Kadinali Zuppi alifanya hapa Kyiv na kisha Moscow, kwamba ahadi ya kibinadamu ilikuwa njia ya kukuza amani hii. Zaidi ya hayo, inaonekana mimi pia mawazo ya viongozi wa Kyiv, kwa sababu huko Uswizi pia walizungumza juu ya vipimo vitatu: kwanza kabisa suala la nyuklia, kwa hiyo kuepuka kuongezeka; basi mada ya uhuru wa usafirishaji wa bidhaa; na, hatimaye, juu ya mada yote ya kibinadamu. Kwa hiyo Vatican imezingatia hili pia kwa ombi la Serikali yenyewe, lakini kwa nia ya kuchukua hatua ambazo zinaweza kuleta amani ya haki.”

Kardinali Parolin nchini Ukraine
20 July 2024, 12:08