Kard.Parolin:Ushuhuda wa Mtakatifu Rosalia sawa na watakatifu wengine wa Sicilia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tangu tarehe 10 Julai, matukio ya heshima ya Siku kuu ya miaka 400 kwa heshima ya mtakatifu mlinzi wa Palermo yamerekodi ushiriki mkubwa wa vijana, watu wazima, wazee na watoto. Kama vile tarehe 15 Julai 2024 katika Kanisa kuu lililojaa licha ya joto kali, wenye ibada ya mwanamke na 'mtume, kama alivyo fafanuliwa na Papa Francisko katika ujumbe uliotumwa kwa ajili ya tukio hilo kwa Askofu mkuu wa Palermo, pamoja katika sala katika Ibada ya Misa Takatifu ya Kipapa, iliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican na akiwa pamoja na Askofu Corrado Lorefice na Maaskofu wa Sicilia. Kwa hakika kumekuwa na ushiriki wa dhati na mshikamano wa waamini wa Palermo ambao umefanya dhahiri, pengine zaidi ya hapo awali, upendo kwa mja wa Mungu Mtakatifu Rosalia, wakiwa na imani yao, kuomba, kujiamini na kujiacha kwa Santuzza, kama anavyoitwa hapo Palermo.
Kardinali Parolin:salamu kutoka kwa Baba Mtakatifu
"Nimefurahishwa na kuheshimiwa kuongoza maadhimisho ya sikukuu ya Mtakatifu Rosalia mwaka huu ambayo inaambatana na karne ya nne ya ugunduzi wa mabaki ya mwanadamu huyu na hapa katika Kanisa kuu la Palermo, ambapo alihamishwa kutoka Monte Pellegrino tarehe 15 Julai 1624 na bado amehifadhiwa katika Kanisa lililowekwa wakfu kwa ajili yake", alisema Kardinali Parolin katika mahubiri yake, huku akikaribishwa kwa uchangamfu na hisia nyingi na waamini wa Palermo alipoingia katika Kanisa kuu, kwa kupeleka salamu za Papa Francisko. Kardinali alisema “Baba Mtakatifu tayari amewatumia ujumbe kwa ajili ya tukio hili lakini nina furaha pia kuwaletea salamu zake binafsi. Anaungana kwa moyo mkunjufu katika furaha na shukurani zenu ninyi watu wa Palermo ambao mko hapa kwa wingi leo hii ili kujiruhusu kuelimishwa na hekima ya bikira Rosalia anakuhakikishia kwamba anaomba baraka kwa jimbo hili kuu, katika kisiwa kizima na juu yenu nyote.”
Ushuhuda wa Mtakatifu Rosalia na watakatifu wa Sicilia
“Ushuhuda wa imani katika Yesu Kristo unamfunga Rosalia kwa watakatifu wengine wa Sicilia wanaume na wanawake kama vile: Agata, Lucia, Gerlando, Vito, Alberto wa Abati, kwa kutaja wachache tu Mashahidi hawa wajasiri wa Kristo walipanda mbegu. mbegu ya Ukristo wa Kanisa la Sicilia na sisi leo, tunda la mbegu hiyo yenye kuzaa matunda, tunamkumbuka mmoja wa mashahidi hawa, Bikira Rosalia, kuheshimu ushuhuda wake wa kielelezo kwa hisia za shukrani na kuomba ulinzi wake wa kimungu juu ya Kanisa la Palermo,” alisema Kardinali Parolin katika mahubiri yake. Watakatifu wa kila wakati na mahali kiukweli ni vielelezo vya uaminifu na ujasiri kwa wale wote wanaotaka kuishi kulingana na Injili ya Yesu. Hata hivyo, kwa kuwa hatuna mafundisho ya moja kwa moja kutoka kwa Mtakatifu wetu, tunaalikwa kukubali yasiyo ya moja kwa moja mafundisho yaliyotolewa kwetu na Maandiko Matakatifu ambayo Liturujia inatupatia wakati wa sikukuu yake", aliongeza Katibu wa Vatican huku akinukuu Wimbo Ulio Bora.
Mungu anamwalika mwanadamu kutafuta uso wake
Kardinali amefafanua kuwa “Mungu anamwalika mwanadamu, na kwa hivyo kila mmoja wetu, kutafuta uso wake na kusikiliza neno lake. Ubinadamu unatamani kumuona Mungu, tulisema katika zaburi jibu, Binadamu anatamani kumuona Mungu, lakini Mungu pia anatamani kuona sura halisi ya ubinadamu na kusikiliza sauti ya binadamu,” aliendelea kusema Kardinali huyo. “Tunaelewa vizuri basi kwamba utakatifu ambao tumeitiwa sio ukamilifu wa kimaadili bali ni uhusiano wenye nguvu, si tu kuwa mzuri, kwa hakika hii pia ni sehemu ya msingi ya utakatifu, lakini zaidi ya yote ni uzoefu wa utakatifu wa maisha ya Mungu ambayo ni pamoja na mwelekeo wa urafiki, wa ukimya, hata wakati mwingine wa upuuzi ambao hukaa katika uwepo wetu wa kibinadamu. Utakatifu ambao Rosalia anatuitia leo hii ni kujihatarisha kupata mabadiliko yanayoletwa ndani yetu na Kristo, vinginevyo imani inakuwa shauku isiyo na maana.”
Kukuza utamaduni wa mazungumzo na akili
"Mabaki ya Mtakatifu Rosalia mnamo 1624 yalibebwa kwa maandamano katika jiji ambalo lilisafishwa na kuokolewa kutoka katika janga kubwa la tauni. Hebu tujiulize, kaka na dada wapendwa, ni janga gani ambalo bado linafunika jiji letu,” aliendelea Kardinali Parolin, linalofunika ulimwengu, ambao unahitaji sana makabiliano na ukweli na mang’amuzi ya imani, kwa hiyo pia tunapata nafuu katika maadhimisho ya Siku Kuu hii hisia kali ya utulivu na huduma ya Kiinjili ambayo ni tunu za kweli zinazomwilishwa na Rosalia. Mji wa Palermo umefuata haki kupitia aina za juu sana za ushuhuda, hadi kufikia hatua ya kutoa maisha ya mtu. Hapa kuna mashahidi wa haki, pamoja na Padre Giuseppe Puglisi mpendwa. Uvamizi wa Kardinali Salvatore Pappalardo umebakia kuchapishwa katika kumbukumbu yetu sote: Wakati kuna majadiliano, Roma, Sagunto inashindwa na maadui, na wakati huu sio Sagunto bali Palermo yetu. Hali ilikuwa ya kiza katika miaka hiyo lakini jiji lilijua jinsi ya kuitikia.”
Damu iliyomwagika ilizaa maelfu ya sauti na uzoefu wa safari ya mabadiliko
Katibu wa Vatican aidha alisema kuwa: “Kutoka katika damu iliyomwagika, maelfu ya sauti na uzoefu walizaliwa kwenye njia ya mabadiliko. Kanisa la Palermo linaendelea hata sasa kuwa makini na haraka katika kukuza michakato na njia zinazolenga kukuza utamaduni wa haki na uhalali, kushirikiana na vyama vingi vinavyofanya kazi ndani ya miji na ambavyo vipo katika eneo hilo kusaidia wananchi kuondokana na mawazo ambayo wakati mwingine yanaweza kuhatarisha kuwa katika mgogoro na sheria. Kuzaliwa utamaduni wa mazungumzo na akili ili kufanya jiji hili liweze kuishi, kukaribisha na kupendeza. Ardhi bila mbingu ni matope, lakini ardhi pamoja na mbingu inakuwa bustani. Wacha tushinde kujiuzulu, tutumie rasilimali zetu bora za akili na moyo. Kwa ushirikiano na ukarimu, jiji linaweza kufanywa kuwa salama, makini katika kutunza aina mpya za umaskini, waaminifu kwa mila yake ya jumuiya yenye ukarimu”, alihitimisha, Katibu wa Vatican.