Tafuta

Kardinali Camillo Ruini. Kardinali Camillo Ruini. 

Kard.Camillo Ruini amelazwa hospitali ya Agostino Gemelli,Roma

Kufuatia maumivu ya kifua,Kardinali Camillo Ruini alilazwa katika hospitali ya Gemelli,Roma.Ujumbe kutoka kwa kituo hicho unaripoti kwamba yuko macho na hali yake ya kiafya kwa sasa inaendelea vizuri. Mnamo Februari iliyopita Kardinali huyo alitimiza umri wa miaka 93.

Vatican News

Katika taarifa iliyotolewa na kituo cha Kiafya cha Hospitaali ya A.Gemelli, Roma imesema: “Jana jioni Kardinali Camillo Ruini alilazwa hospitalini kwa dharura huko Gemelli kutokana na maumivu ya kifua. Kwa kuzingatia umri mkubwa wa Kardinali na historia ya matibabu, kulazwa hospitalinikatika utunzaji mkubwa wa moyo ilikuwa muhimu. Mgonjwa yuko makini na ana ushirikiano na hali yake ya kliniki kwa sasa ni thabiti. Ufuatiliaji na matibabu unaendelea." 

Mnamo tarehe 19 Februari 2024, Kardinali Ruini alifikisha miaka 93. Alizaliwa Sassuolo, jimbo la Modena, Italia na kuhitimisha  masomo yake ya falsafa na Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, akiwa  mwanafunzi wa Taasisi ya  Almo Capranica, akipata leseni ya falsafa na Taalimungu. Alipewa daraja la Upadre tarehe 8 Desemba 1954, baada ya muda mrefu wa kufundisha katika Jimbo la Reggio Emilia Tarehe 16 Mei 1983 aliteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Nepte na Askofu msaidizi wa majimbo ya Reggio Emilia na Guastalla.  Mnamo mwaka 1985 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Maaskofu ya Elimu ya Kikatoliki, Utamaduni na Shule.

Tarehe 28 Juni 1986 Yohane Paulo II alimteua kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia. Tena Papa Wojtyla tarehe 17 Januari 1991 alimchagua kuwa Makamuwake Jimbo kuu la Roma, akamuumba kuwa Kardinali na kumteua kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia. Wadhifa alioshikilia hadi tarehe 7 Machi 2007, wakati Papa Benedikto XVI alipokubali maombi yake ya kustaafu kwa sababu ya umri wake. Mwaka uliofuata, 2008, alihitimisha huduma yake, kwa mara nyingine tena akiwa amefikia kikomo cha umri, katika nafasi ya Makamu Jimbo kuu la Roma na Mkuu wa Basilika ya Kipapa ya Laterano.

Kuanzia Januari 2008 hadi Januari 2013, ndani ya Baraza la Maaskofu Italia (CEI,) alikuwa Rais wa Kamati ya mpango  wa kiutamaduni. Kuanzia 2010hadi 2014, Kardinali Ruini aliongoza Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi kuhusu Medjugorje iliyoanzishwa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Alishiriki katika Baraza la Uchaguzi mnamo Aprili 2005 lililomchagua Papa Benedikto XVI, na pia kuwa Rais wa Kamati ya Kisayansi ya Joseph Ratzinger – (Benedict XVI Vatican Foundation) kwa miaka mitano ya kwanza kuanzia 2010-2015.

07 July 2024, 15:45