Tafuta

2024.07.05 Askofu Mkuu Gallagher akiwa katika Monasteri ya Kugeuka sura Malaybalay Bukidnon, Ufilippini, 4 Julai 2024. 2024.07.05 Askofu Mkuu Gallagher akiwa katika Monasteri ya Kugeuka sura Malaybalay Bukidnon, Ufilippini, 4 Julai 2024. 

Ask.Mkuu Gallagher kwa maaskofu Ufilipini:Mamlaka pekee ni ya huduma

Katika mahubiri ya misa Takatifu katika Monasteri ya Kigeuka Sura kwa maaskofu hao alisisitiza juu ya dhana ya mamlaka ya Askofu,kuwa si kwa maana ya mamlaka ya kisheria au mamlaka,lakini aina nyingine ya mamlaka,ambayo tunaweza kuiita mamlaka yetu ya maadili.Lakini jinsi wanavyotumia uwezo huo ndio huchangia mamlaka yao ya kimaadili kama wachungaji.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 4 Julai 2024, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusino na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa akiwa nchini Ufilipini tangu tarehe Mosi Julai, aliadhimisha Misa pamoja na maaskofu wa Baraza la maaskofu nchini Ufilippini katika Monasetero ya Kugeuka Sura huko  Malaybalay Bukidnon. Akianza mahubiri yake alianza na salamu kwa Kardinali Jose Advincula, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Manila, Askofu Pablo Virgilio S. David, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Ufilippini na maaskofu wote ndugu zake. Injili yetu asubuhi ya tarehe 4 Julai 2024 ilikuwa inasimulia uponyaji wa mtu aliyepooza na Yesu, uponyaji unaoanza kwa Yesu kutambua imani ya watu waliombeba mtu huyo mbele yake. Ni kwa sababu ya imani yao dhahiri kwamba Bwana anamwambia mtu aliyepooza ‘dhambi zako zimesamehewa.’

Muujiza wa kuponya

Hatua hii ya Bwana inawafanya waandishi kuhitimisha kwamba amekufuru. Na kwa hivyo, Bwana anauliza, labda kwa maneno: “Ni lipi lililo rahisi zaidi, kusema, 'Umesamehewa dhambi zako,' au kusema, 'Simama, uende'?” Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi”,  kisha alimwambia yule mwenye kupooza: “Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako.” Mtu huyo anaponywa, na umati wa watu unamtukuza Mungu ambaye amewapatia watu mamlaka ya namna hiyo.” Kwanjia  hiyo, kuna matendo mawili ya Yesu katika Injili hiyo, alisema Askofu Mkuu Gallagher na kufafanua kuwa: “lile la  kusamehe dhambi na ya uponyaji wa kimwili; ambapo zimeunganishwa na muhimu ni kwamba Yesu ana mamlaka ya kufanya yote mawili. Askofu Mkuu Gallagher alisema“Sisi, kama Maaskofu na mapadre, tunayo mamlaka ambayo si yetu wenyewe. Kama vile Katekisimu ya Kanisa Katoliki inavyofundisha, kuwekwa wakfu “hutoa zawadi ya Roho Mtakatifu ambayo inaruhusu matumizi ya 'nguvu takatifu' (sacra potestas), ambayo inaweza tu kutoka kwa Kristo mwenyewe kupitia Kanisa lake” (Rej.1538).

Matendo yetu kwa niaba ya Kristo

Matendo yetu ya kisakramenti, yanayofanywa “in persona Christi”, kwa ‘niaba ya Kristo’ yanatokana na uwezo huu, ambao ni Wake, si wetu. Zoezi letu la “sacra potestas”, hata hivyo, lazima pia liidhinishwe na Kanisa. Kuna mifano mingi ya hili: kwa mfano, Askofu anaweza kuwa na “potestas” ya kumweka wakfu  padre kuwa uaskofu, lakini anaweza tu kutumia uwezo huo ikiwa pia ana mamlaka aliyopewa na Baba Mtakatif.  Kwa njia hiyo Askofu Mkuu alipenda kujikita juu ya dhana hii ya “mamlaka” ya Askofu, si kwa maana ya mamlaka ya kisheria au mamlaka, lakini aina nyingine ya mamlaka, ambayo tunaweza kuiita “mamlaka yetu ya maadili” au kwa Kiitaliano; “autorevolezza.” Kama alivyokuwa ametaja  alisisitiza “sisi, kama wahudumu waliowekwa wakfu, sote tunafanya “potesta” zile zile tulizopokea katika kuwekwa wakfu. Labda ni jinsi tunavyotumia uwezo huo, kwa jinsi tunavyotumia uwezo huo ndio huchangia mamlaka yetu ya kimaadili kama wachungaji.” Alisisitiza Askofu Mkuu Gallagher.

Cheo cha Askofu ni utumishi

Akisisitiza zaidi alisema: “Baba Mtakatifu Francisko ameendelea kurejea mada hii, akitukumbusha kwamba “cheo cha Askofu kwa hakika ni cheo cha utumishi – si uaskofu wa kweli bila huduma – si heshima kama wanafunzi walivyotaka, mmoja upande wa kulia, mmoja upande wa  kushoto, kwa sababu Askofu anapaswa kujitahidi kutumikia badala ya kutawala […] Na kwa huduma hii [Papa anasema] mtasimamia wito wenu na kuwa wachungaji wa kweli katika huduma, si kwa heshima, kwa nguvu, na kwa mabavu. Hapana, kutumikia, kutumikia kila mara” (Rej. Mahubiri 17 Oktoba 2021). Hii ndiyo aina ya mamlaka inayotekelezwa na viongozi watumishi, Maaskofu ambao wakleri na watu wanaweza kuhisi ndani yao nia ya dhati ya kutumikia, kumtumikia Kristo na Kanisa lake. Kama Papa Francisko alivyosema katika muktadha mwingine: “Kwa wanafunzi wa Yesu, jana, leo na siku zote, mamlaka pekee ni mamlaka ya huduma…” (Hotuba ya maadhimisho ya miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Sinodi ya Maaskofu, 17 Oktoba 2015). Askofu Mkuu Gallagher alisema kuwa: “ Wakati makuhani wetu na watu wanaweza kuona na kupata uzoefu huo wa roho ya huduma ndani yetu, watakubali kuongozwa; na watatuamini.”

Utumishi si kuwa waoga au kimya katika uso wa dhuluma na uovu

Mwakilishi wa Vatican huyo aidha alisema kuwa “Lakini uongozi wa utumishi haimaanishi kwamba tunaitwa kuwa waoga, kimya au kushiriki katika uso wa dhuluma na uovu. Kuna wakati sisi Maaskofu, kama viongozi watumishi, tunapaswa kutumia mamlaka yetu ya maadili kupinga mamlaka ya mamlaka ya ulimwengu huu. Tunafikiria mfano wa Mtakatifu Oscar Romero na ule wa mashahidi wasiohesabika katika historia ya Kanisa. Kama vile Muhtasari wa Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa yanavyofundisha: “Mamlaka ya mwanadamu inapovuka mipaka inayotakiwa na Mungu, inajifanya kuwa mungu na kudai utii kamili; inakuwa Mnyama wa Ufunuo, sanamu ya nguvu ya mtesaji wa kifalme "aliyelewa kwa damu ya watakatifu na damu ya mashahidi wa Yesu”(Ufu 17: 6) [...]. Lakini Kristo ndiye Mwana-Kondoo Mshindi ambaye, katika historia ya mwanadamu, anashinda kila nguvu ambayo ingefanya kuwa kamili. Kabla ya nguvu kama hiyo, Mtakatifu Yohane anapendekeza upinzani wa wafiadini imani; kwa njia hii, waamini wanashuhudia kwamba nguvu potovu na za kishetani zimeshindwa, kwa sababu hazina mamlaka tena juu yao.”

Mamlaka na ushuhuda wa kung'aa wa Mtakatifu Yohane Paulo II

Askofu Mkuu Gallagher alitaka kutoa mfano mwingine na kusema: “Hebu nitaje ukweli mwingine wa kihistoria, karibu na wakati wetu wenyewe: sura ya Papa Mtakatifu Yohane Paulo II. Hapana shaka kwamba mamlaka ya kimaadili ya Papa Yohane Paulo wa Pili, ushuhuda wake thabiti na wenye kung’aa juu ya thamani ya mwanadamu na mafundisho yake juu ya uhuru halisi wa binadamu, yalikuwa ni kipengele cha kuamua katika mabadiliko yaliyokumba Ulaya Mashariki katika miaka hiyo ya  1989-1991. Katika hili, kuna somo kwetu sisi kama Maaskofu katika wakati wetu wa kihistoria wa sasa. Nyakati fulani, inaweza kuonekana kwamba mahubiri na mafundisho yetu yameanguka kwenye masikio ya viziwi na hayana matokeo yoyote yanayoonekana. Lakini tukumbuke kwamba ni katika uthabiti na uthabiti wetu, daima katika upendo, ndipo mamlaka yetu ya kimaadili kama Maaskofu inatekelezwa.” Kwa njia hiyo alisisitiza kuwa “Tunahitaji kuwa na subira na kutumainia uweza wa Bwana. Atatenda. Nimekumbushwa jina la kitabu kilichochapishwa na Kardinali Agostino Casaroli kuhusu diplomasia ya Jimbo Kuu la Mtakatifu katika miaka iliyofikia kilele cha mabadiliko ya 1989: "Martyrdom of Patience".yaani Mashahidi wa vuvumilivu.

Kuwa tayari wakati wote

Askofu Mkuu aliendelea kueleza: "Kuwa mvumilivu, kuhubiri na kufundisha kwa usadikisho mtulivu, kama Mtakatifu Paulo asemavyo: “katika msimu mzurni na kama msimu usio mzuri,”: hii ni aina ya kifo cha kishahidi. “Lihubiri neno; kuwa tayari wakati mavuno na nje ya mavuno; sahihisha, kemea, na kuhimiza kwa uvumilivu mwingi na mafundisho makini” (2 Tim 4:2). Ni katika ushuhuda huu thabiti, wenye subira ndipo mamlaka yetu ya kimaadili kama Maaskofu inadhihirika. Nguvu zetu hutoka kwa Kristo, lakini nguvu hiyo  ambayo ni Yake -inakuwa dhahiri kupitia mamlaka yetu kama wanafunzi wake na watumishi wake. Hebu tuazimie basi kuwa na kutenda daima kama wachungaji “secundum cor Christi”, yaani "kwa mujibu wa moyo wa Kristo". Askofu Mkuu Gallagher alihitimisha mahubiri yakeakionesha furaha yake kuwa pamoja nao. Aliwashukuru kwa ushuhuda wao na ukarimu wao mzuri. Aliowamba wasonge mbele kwa kujiamini na kumtumaini Bwana, kwa kutambua daima ukaribu wa Bikira Maria, mama na Malkia wetu. Mungu awabariki!"

05 July 2024, 17:19