Joto jijini Roma Joto jijini Roma  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Majira ya joto kwa wale ambao hawaendi likizo!

Likizo sio uvivu ni wakati mzuri wa kujitolea kwa maadili ya maisha na kupunguza kasi ya kijamii ambayo sasa inatuzuia kuelewa kikamilifu kile kinachopita mbele yetu kila siku.Tatizo kubwa katika miji ni kuacha wazee peke yao ambapo kuna haja Ulaya kutafuta mipango ya kuwajali wasio na uwezo kama maskini na wazee.

Na Alessandro Gisotti – Vatican.

“Natafuta majira ya joto mwaka mzima na ghafla yako hapa.” Huu ni ubeti wa wimbo maarufu wa Azzurro unaotafsiri vyema hali ambayo Waitaliani,  iwe ni wanafunzi vijana au watu wazima wanaofanya kazi, ambao  hupitia kwa kuwasili kwa msimu wa kiangazi, kipindi cha likizo kinachosubiriwa na kutafutwa kwa muda wote wa mwaka. Kwa muda sasa, nchini Italia kama katika nchi nyingine za Magharibi, likizo zimekuwa haki halisi. Na zaidi ya hayo, Mapapa wa mwisho wamesisitiza umuhimu wa kupata mapumziko kutoka katika kazi ili kusitawisha mahusiano muhimu zaidi, kuanzia yale ya familia, na kufurahia Uumbaji ambao hutolewa bure kwa kila mmoja wetu.

Likizo siyo uvivu ni wakati mzuri wa kujitolea katika maadili ya maisha

Kwa hivyo likizo sio kusema ni uvivu lakini ni kama wakati mzuri wa kujitolea kwa maadili ya maisha na kupunguza kasi ya kijamii ambayo sasa inatuzuia kuelewa kikamilifu kile kinachopita mbele yetu kila siku. Wakati huo huo, “kwenda likizo” mara moja inakumbuka tabia ya asili ya mtu kusafiri. Binadamu amekuwa safarini siku zote. Ni daima yuko katika mwendo. Kama Mtakatifu Augostino alivyosema: “Dunia ni kitabu. Wale ambao hawasafiri husoma ukurasa mmoja tu.” Si kwa bahati mbaya kwamba leo hii kwa kawaida tunasema: “Ninakwenda likizo” kwa kutumia kitenzi kinachoashiria kwenda kwa sababu la sivyo likizo isingehisiwa hivyo. Walakini katika miji yetu ya jua, kuanzia Roma iliyojaa watalii ambao ni kama hawajaonekana kwa muda mrefu, lakini kuna watu  ambao hawatakwenda likizo kwa sababu hata haki hiyo kati ya wengine wengi, wananyimwa  ambao ni maskini…  Wao, wasioonekana au wanaoonekana kwa kutojali, hawatakuwa na fursa hiyo. Miaka michache iliyopita, walipata kujulikana kwa habari iliyoripotiwa sana ambapo, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, Kardinali Konrad Krajewski, alikuwa amechukua kikundi cha watu wasio na makazi kukaa siku moja kwenye bahari.

Watu wasio na makazi na wasiojiweza wanapaswa kusaidiwa

Na zaidi Ziara ya kwanza ya watu wasio na makazi kwenye Kikanisa cha Sistine iliyotolewa na Papa iliamsha mshangao sawa na huo. Ishara mbili zinazoonekana kuwa ndogo bado ni kubwa katika maana, kwa sababu zinaonesha kwamba hata maskini - kama na zaidi ya wale ambao hawaishi katika umaskini, wanahitaji nafasi na fursa za kujifurahisha na kufurahia uzuri wa sanaa ambayo  nchini Italia ni amana isiyo na mipaka. Kwa nini usifikirie basi, katika msimu huu wa kiangazi wa 2024, kwamba kila jiji, ndogo au kubwa, linapanga mipango kama hiyo? Hatimaye, muundo wa kijamii na kiraia pia unarekebishwa kwa njia hii: kwa kuweka wale walio kwenye mpaka, ambapo mara nyingi huwekwa hadi sasa kwenye ukingo ambao hatuwezi hata kuwaona.

Hata waliotupwa wana utajiri mwingi wa kibinadamu

Kwa hivyo tungegundua kwamba hata kati ya hawa “waliotupwa” kuna utajiri mwingi sio tu wa ubinadamu bali pia wa uzoefu wa kitaalamu, wa tamaduni, wa akili kama inavyoonekana katika usomaji wa Gazeti la Oservatore la Barabara ambalo kila mwezi wanaleta katika uso historia za watu wa mwisho. Karibu na wale maskini kuna watu wengine ambao wanateseka hasa wakati wa kiangazi na ambao wako karibu sana na moyo wa Bergoglio yaani: wazee. Kwao pia, katika miji ambayo inakuwa tupu wakati wa kiangazi, huduma za umma zinazopungua na wapendwa wao wanaohama ni changamoto ngumu kuikabili. Kama Askofu Mkuu Vincenzo Paglia alivyobainisha kuwa: “Wazee wetu hawafi kwa joto, lakini kwa upweke na kutelekezwa.” Hata hivyo ni babu na bibi hasa ambao, wakati wa mapumziko ya mwaka, huwa na kazi ya hali ya ustawi halisi, hasa wakichukua jukumu la kukaa na kutunza wajukuu wao.”

Mara kadhaa Papa ametoa wito wa muungano kati ya vijana na wazee

Tangu kuanza kwa Upapa wake, Baba Mtakatifu ametoa wito kwa nguvu zote  hasa haja ya kuwepo muungano kati ya vijana na wazee ili kufungua mustakabali wa ubinadamu uliojeruhiwa. Aliwatia moyo vijana wasiwaache wazee peke yao, wafuate mfano wa kibiblia wa Ruthu, ambaye hakumwacha mama mkwe wake mzee Naomi. Hakuna njia mbadala halali ya kusaidiana huku kwa vizazi ikiwa kweli tunataka kuifanya jamii tunamoishi kuwa ya utu zaidi. Angalau kanuni hii, inaonekana kwa Papa Francisko anataka  kutuambia kwamba, ni vizuri yeye haendi kamwe likizo.

Likizo ya kiangazi kwa mujibu wa Gissotti
02 July 2024, 16:16