Askofu Mkuu Ettore Balestrero,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa. Askofu Mkuu Ettore Balestrero,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa. 

Mons.Balestero katika UN:Lazima kutokomeza umaskini wa kukithiri!

Je,mnaona ni jukumu gani la mashirika ya kidini yanachukua na sio tu kupunguza athari za umaskini uliokithiri,lakini pia katika ujenzi wa uchumi wa haki zaidi na utu wa binadamu katika msingi wake?Ni swali la Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika UN alilowaachia kwenye Kikaio cha Baraza la Haki za Binadamu kuhusu:"Umaskini wa kukithiri na haki za binadamu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hotuba ya Mwakilishi wa Vatican katika Umoja wa Mataifa katika kikao cha Baraza la Kawaida la Haki za Binadamu kuhusu Umaskini wa kuklithiri na haki za binadamu, tarehe 3 Julai 2024, amesema kuwa “Ujumbe wa Vatican umekaribisha fursa ya kuzungumza na Mwandishi Maalum kuhusu Ripoti yake yenye mada inayoitwa: ‘Kutokomeza umaskini wa kukithiri.” Hata hivyo Ripoti inapinga mitindo hiyo kwa kuzingatia ukuaji wa uchumi pekee, wa kuongezeka kwa Pato la Taifa, na kuongeza faida, na kusema kuwa ni kengeusho kutoka kwa kile ambacho ni muhimu sana, yaani: kutokomeza umaskini na ustawi kwa wote.”

Kuhusiana na hilo, Papa Francisko alibainisha kwamba: “baadhi ya kanuni za kiuchumi zimethibitika kuwa na matokeo katika ukuaji, lakini si kwa ajili ya maendeleo muhimu ya binadamu. Utajiri umeongezeka, lakini pamoja na ukosefu wa usawa, na matokeo yake ni kwamba ‘aina mpya za umaskini zinaibuka’. Madai ya kwamba ulimwengu wa kisasa umepunguza umaskini yanatolewa kwa kupima umaskini kwa kutumia vigezo vya zamani ambavyo havilingani na hali halisi ya sasa.” Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican aidha alisema kuwa “Hata hivyo, kuna wale wanaoendelea kuunga mkono nadharia ya uchumi duni ambayo inadhania kwamba ukuaji wa uchumi, unaohimizwa na soko huria, bila shaka utaleta haki zaidi ya kijamii. Hata hivyo sivyo ilivyo: waliotengwa wanaendelea kusubiri.”

Kwa hiyo ni “muhimu kwamba uchumi usizingatie ukuaji pekee. Na mnamo mwaka  1967, Papa Paulo VI  alisema kwamba: “maendeleo hayawezi kuzuiwa tu kwenye ukuzi wa kiuchumi. Ili kuwa halisi, lazima iwe na mzungumko mzuri; ni lazima kustawisha maendeleo ya kila mtu na ya mtu mzima.”  Kwa njia hiyo aliongeza kusema Mwakilishi wa Vatican kuwa “Dira hii muhimu ya ukuaji inajumuisha pamoja na mambo mengine haki ya kuishi, uadilifu wa mwili, na uhakikisho unaohitajika kwa maendeleo sahihi ya maisha, ikiwa ni pamoja na chakula, mavazi, malazi, matibabu, elimu, mapumziko, na hatimaye, huduma muhimu za kijamii. Ni jinsi gani bado kunahitajika kufanywa ili hili liwe ukweli, si kitu haba kupitia kujitolea kwa dhati na kwa ufanisi kwa upande wa viongozi wa kisiasa na wabunge.” Kwa njia hiyo mwakilishi wa Kudumu wa Vatican aluhitimisha kwa kuuliza  swali:   Je, mnaona ni jukumu gani mashirika ya kidini kuchukua katika sio tu kupunguza athari za umaskini uliokithiri, lakini pia katika ujenzi wa uchumi wa haki zaidi na utu wa binadamu na utu wa binadamu katika msingi wake?

Hotuba ya Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika UN
04 July 2024, 16:33