Tafuta

2021.03.11 Bandiera Vaticana 2021.03.11 Bandiera Vaticana 

Mons.Dubiel ni Balozi mpya wa Vatican nchini Angola

Monsinyo Kryspin Dubiel alizaliwa huko Nowa Sarzyna Poland tarehe 12 Novemba 1973.Alipewa daraja takatifu la Upadre mnamo tarehe 31 Mei 1989 kwa ajili ya Jimbo la Przemyśl.

Vatican News.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe Mosi Julai 2024  amemteua Balozi mpya wa Vatican nchini Angola, Mheshimiwa sana  Monsinyo Kryspin Dubiel, Mshauri wa Ubalozi na kumwinua hadhi kuwa Askofu Mkuu kwa makao ya Kanisa la Vannida.

Monsi. Kryspin Balozi mpya wa Vatican nchini Angola
Monsi. Kryspin Balozi mpya wa Vatican nchini Angola

Monsinyo Kryspin Dubiel alizaliwa huko Nowa Sarzyna  Poland, tarehe 12 Novemba 1973. Alipewa daraja takatifu la Upadre mnamo tarehe 31 Mei 1989 kwa ajili ya Jimbo la Przemyśl.  Alihitimu katika Sheria ya Kanoni.

Alijiunga katika Utumishi wa Kidiplomasia wa Vatican mnamo tarehe 1 Julai 2004, na kutoa huduma yake kama mwakilishi wa Kipapa katika nchi za: Rwanda, Belarus, Colombia, Ufilipino, Poland, Slovenia na Umoja wa Falme za Kiarabu. Anajua lugha ya Kifaransa, Kiitaliano, Kirusi na Kihispania.

Balozi mpya wa Vatican nchini Angola
01 July 2024, 15:50