Mons.Gyhra,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika UN huko Vienna
Padre wa Marekani na mwanadiplomasia wa Vatican Mons.Richard Allen Gyhra anahamia Vienna, kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko huko:U.N.I.DO,A.I.E.A,C.T.B.T.O. na O.S.C.E. huko Vienna,Uswiss.
Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 1 Julai 2024 amemteua Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Taasisi maalum huko Vienna nchini Uswiss na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda(U.N.I.DO), Mwakilishi wa Kudumu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki(A.I.E.A,) Shirika la Utekelezaji wa Mkataba wa Kupiga Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia(C.T.B.T.O.) na Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya(O.S.C.E.), Mweshimiwa sana Monsinyo Richard Allen Gyhra, Mshauri wa Ubalozi na ambaye hadi uteuzi huo alikuwa katika Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania.
01 July 2024, 16:04