Tafuta

Bustani za Vatican. Bustani za Vatican.  (Laura Lo Monaco)

“Nasa Asili”ni ziara kwa ajili ya familia yote katika Bustani za Vatican

Kuanzia tarehe 13 Julai hadi tarehe 26 Oktoba,umefunguliwa mpango uliohamasishwa na Makumbusho ya Vatican na ulioundwa kwa ajili ya wazazi wote ambao pamoja na watoto wao,wanaweza kutumia masaa mawili kuwa katika“bustani za Papa” kwa njia ya kujifunza mazingira.

Vatican News

Pendekezo jipya na la asili kutoka Jumba la Makumbusho ya Vatican lilianza tangu tarehe 13 Julai 2024, na litadumu hadi mwishoni mwa Oktoba linaloongozwa mada: “Nasa Asili” ambapo ni ziara ya kwanza ya kuongozwa katika Bustani ya Vatican maalum kwa wazazi ambao wanataka kutumia masaa mawili ya kupendeza wakiwa pamoja na watoto wao katika mandhari nzuri ya asili ya “Bustani za Papa, zilizojitolea kwa ajili ya mafunzo ya asili na ya wazi. Ratiba ya asili na ya kusisimua ilichochewa na Waraka wa Papa Francisko wa Laudato Si' ili kuongeza ufahamu wa watu wazima na watoto kuhusu masuala ya ulinzi wa kazi ya Uumbaji na ulinzi wa mazingira.

Kugundua mapafu ya kijani ya Jiji la Vatican

Mpango huo utaboresha kwa utoaji wa ziara na shughuli zinazoundwa na Makumbusho ya Vaticani iliyoundwa kwa ajili ya familia. Kila Jumamosi ya mwezi, hadi tarehe 26 Oktoba 2024 familia zitaongozwa na wataalam wa elimu ili kugundua “pafu la kijani” la jiji la Vatican ambapo kuna mimea ya Bustani ya Kibiblia, Miti, Bustani ya Kiingereza, Chemi chemi ya Spinster, Casina na Pio IV, Maria wa Ulinzi na ile ya Fatima, sehemu zinazopendwa na Mapapa wakati wa matembezi yao, nguo za upapa, na hatimaye historia nyingi na udadisi. Kile kitakachofanya safari hii kupitia asili, sanaa na imani kuwa maalum kitakuwa zaidi ya yote michezo, warsha na uzoefu wa burudani ambao utachangamsha ziara.

Ulinzi wa nyumba ya kawaida

Miongoni mwa shughuli zilizopendekezwa ni pamoja na uwindaji wa hazina usioepukika, uundaji wa “kito bora” cha Vatican chenye mbinu ya baridi kali, ugunduzi wa kasa, utambuzi wa mimea iliyotajwa katika Biblia, “Wood Wide Web na “Familia ya Miti” na  “Takataka au Asili?” kujifunza jinsi ya kutofautisha bidhaa asili na zile zisizo za asili. Uzoefu halisi wa elimu ya nje ili kukua pamoja katika ufahamu wa uzuri na ulinzi wa nyumba yetu ya kawaida. Ziara ya kuongozwa(inapatikana katika Kiitaliano na Kiingereza)imeundwa kwa ajili ya familia zilizo na watoto walio na umri wa kati ya miaka 6 na 12 na pia inapatikana kikamilifu kwa watu wenye ulemavu wa hisi, motor na kiakili(hifadhi iliyowekwa kwa anwani ya barua pepe: accessibilita.musei@scv.va). Mwishoni mwa ziara na bila gharama ya ziada, itawezekana kutembelea Makumbusho ya Vatikani kwa kujitegemea.

Kutembelea Bustani za Vatican kuanzia 13 Julai hadi 26Oktoba 2024
15 July 2024, 16:27