Nicaragua:Serikali yafunga Radio Maria baada ya zaidi ya miaka 40!
Vatican News
Mnamo tarehe 9 Julai 2024, hadhi ya kisheria ya Radio María, kituo cha matangazo ambacho kimekuwa kimekuwa kikitangaza katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati kwa zaidi ya miaka 40, kimefutwa nchini Nicaragua. Hii iliripotiwa na tovuti huru ya ‘Noticias’. Kuvunjwa kwa matangazo ya Radio María, pamoja na ya mashirika mengine 12, kuliidhinishwa na María Amelia Coronel, Waziri wa Mambo ya Ndani, na kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali: “La Gaceta de Nicaragua.”
Ili kuhalalisha hatua hiyo, kiongozi huyo wa Serikali alidai kuwa Radio Maria haikutayarisha bajeti ya kipindi cha 2019-2023, na kwamba, kamati yake ya usimamizi iliisha tarehe 8 Novemba 2021. Hatua hiyo lakini inajiri baada ya mtangazaji kutangaza kupunguzwa kwa muda wake wa utangazaji, kutoka masaa 24 hadi 14 na kufuatia kufungiwa kwa akaunti zake mbili za benki, jambo ambalo lilizuia Radio hiyo kutopokea michango.