Papa Francisko amemteua msimamizi wa Vicarieti ya Kitume huko Nekemte,Ethiopia
Vatican News
Baba Mtakatifu Jumanne tarehe 16 Julai 2024 amemteua kuwa Msimamizi wa Vicarieti ya Kitume ya Nekemte nchini Ethiopia Padre Getahun Fanta Shikune, C.M., hadi uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi wa Kiroho wa Shule ya Lazarist huko Addis Ababa na Mkurugenzi wa Kiroho wa Watawa wa Mabinti wa Upendo nchini Ethiopia.
Wasifu wake
Monsinyo Getahun Fanta Shikune, C.M., alizaliwa tarehe 25 Februari 1973 huko Aleku Sassi, Wollega Magharibi, katika Vicariate ya Kitume ya Nekemte. Ana Shahada ya Uzamili katika Rasilimali Watu kutoka Chuo Kikuu cha DePaul huko Chicago (Marekani). Baada ya kuingia Seminari ya Shirika la Utume, alisoma katika Taasisi ya Falsafa na Taalimungu ya Mtakatifu Francis, Addis Ababa. Alipewa daraja la ukuhani tarehe 1 Julai 2001. Alishikilia nyadhifa zifuatazo: Paroko wa Parokia ya Mwokozi Mtakatifu, Sako, na Mtakatifu Maria, Metcha; Mkuu wa Seminari Kuu ya Taasisi yake; Mkuu wa Shirika Shirika la Utume huko Ethiopia mara mbili (2010-2013 na 2013-2016); alitoa huduma katika Parokia ya Mtakatifu Maria wa Sayuni. Kwa sasa yeye ni Mkurugenzi wa Shule ya Lazarist huko Addis Ababa na Mkurugenzi wa Kiroho wa Mabinti wa Upendo nchini Ethiopia.