Tafuta

2024.07.07 Ziara ya Papa ya kichungaji huko Trieste. 2024.07.07 Ziara ya Papa ya kichungaji huko Trieste.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto) Tahariri

Papa huko Trieste,Ruffini:miguu duniani lakini kwa maadili bora

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,Dk.Paolo Ruffini katika Gazeti la Osservatore Romano tahariri yake inaakisi kuhusu vifungu muhimu vya hotuba ya Papa Francisko aliyoitoa tarehe 7 Julai 2024 mwishoni mwa Juma la Mafundisho ya Kijamii ya Wakatoliki nchini Italia huko Trieste iliyo funguliwa tarehe 3 Julai.

Na  Paolo Ruffini

Kuna swali lililoelekezwa kwa wote na sio tu kwa wale wanaojiita wanasiasa weledi, katika hotuba ya Papa Francisko hapo mjini Trieste.

Siasa ni nini kwetu?

Na pamoja na swali hilo kuna hata swali nyingine, na labda tuseme kuna mawili: demokrasia ni nini? Na ni jukumu gani la kila mtu, na kwa hivyo pia la Wakristo, kwa Wakatoliki, katika mgogoro wa  demokrasia?

Haya sio maswali ya shule. Labda ni kinyume chake. Kwa hakika, yanatuuomba tutoke wkwenye ule uzushi mwingi ambao mara nyingi tunakimbilia tunapopunguza siasa kuwa mchezo wa madaraka, wa hesabu, au upanuzi mdogo, hadi kushika nyadhifa za amri; na tunapobadilisha demokrasia kuwa mwongozo baridi wa sheria zinazoongoza mchezo huu ambao wengi sana - kimakosa - wanachukulia kuwa wa mtu mwingine. Ukweli ni kwamba kwa kujifanya kuwa watazamaji tu, badala ya kuwa wadau(wahusika wakuu wanaowezekana wa maendeleo kuelekea manufaa ya wote), kwa kubaki kutazama kutokea kwenye balkoni, tunaishia kutenda kama Pontio Pilato; na kunawa kwetu mikono kunaishia kuzidisha mzozo wa siasa na ule wa demokrasia; na pamoja nao hatima yetu.

Jibu la Papa Francisko ni tofauti; ni la dhati. Na wakati wa mgogoro hasemi katika mipango ya kufikirika; lakini anatupa changamoto ya  kuchunguza dhamiri yetu ya kibinafsi na ya pamoja. Kama watu binafsi na kama watu kwa ujumla.

Je tunacheza mchezo gani?

Ikiwa siasa na demokrasia haziwahusu baadhi tu (wengine: wanaopiga kura, wanaotawala, wanaopinga, wanaopigana, wanaokwenda viwanjani); ikiwa zinahusu kila mmoja wetu, maisha yetu, uchaguzi wetu, na sio tu wakati wa kupiga kura, ikiwa kila kitu kimeunganishwa; Tunacheza mchezo gani?

Maswali ya Papa yanaelekezwa kwetu; na kuturudisha duniani. Ni thabiti. Kama vile Papa  Francisko anavyorudia kunukuu watangulizi wake  kwamba “upendo wa  siasa ni mtindo wa juu zaidi.” Unafanya kuonesha mipango iliyojengwa mezani kwa uangalifu juu.Kwa kuchukua dhana kwamba uoni ufupi tu wa wakati wetu ambao  hauzingatii kisiasa. Mtazamo wa upendo, unaodai ushiriki,unaojumuisha kila kitu, “ambao hauridhiki na kutibu madhara bali hujaribu kushughulikia visababishi vyake. Na ni aina ya upendo unaoruhusu siasa kutekeleza majukumu yake na kuepuka ubaguzi.”

Je, upendo kwa wengine, una nafasi gani katika mawazo yetu ya kisiasa?

Kama vile Papa Francisko anavyosisitiza Upendo ni thabiti. Unajumuisha. Unatujua kwa majina. Unatuita kwa majina kuchukua jukumu la kibinafsi kwenye njia ya kuelekea maendeleo zaidi ya mwanadamu. Unatuhusisha katika ujenzi wa mbadala kutoka kudhoofisha maadili ya mienendo ya kubagua. Ndiyo dawa pekee ya kweli dhidi ya saratani inayoharibu siasa na demokrasia, ambayo hulisha chuki na kutojali. Ni juu ya kila mmoja wetu kutopunguza siasa, ambazo sote tunazihitaji, kwa jumla ya idadi, ya asilimia. Kwa “kisanduku kitupu” cha kujaza. Ni juu ya kila mmoja wetu kurejesha tumaini, unabii wa siku zijazo kujengwa pamoja, wote kwa pamoja; uzuri wa kushiriki mipango na historia katika ujenzi wa manufaa kwa wote.

Papa Francisko anatuambia kuwa “Siasa  ni "kushiriki". "Ni kutunza kila kitu." Ni "kujifikiria sisi kama watu na sio kama mimi au ukoo wangu, familia yangu, marafiki zangu. Sio wingi. Hapana, ni kitu kingine." Ushiriki ni wajibu, Wingi wa watu (populism) kwa upande mwingine ni kufuta wajibu, ambao ni wa mtu binafsi, katika kutofahamika kwa wingi. Kufikiria makubwa, kukunja mikono na kufanya mambo makubwa, kwa pamoja. Hii ni kazi ya Wakatoliki katika siasa.

Miguu duniani  lakini maadili bora.

Wataalamu wenye hisia kubwa ya ukweli, na ya mipaka; ufahamu wa kuweza kubadili ukweli. Hatua kwa hatua. Katika safari ambayo daima inaendelea. Bila kubadilishana njia  kama alivyosema Padre  Primo Mazzolari katika hatua ya kuwasili na milki.Papa Francisko katika Waraka wake wa kitume wa Evangelii gaudium anaandika kuwa “Imani ya kweli  daima inamaanisha hamu kubwa ya kubadilisha ulimwengu, kusambaza maadili, kuacha kitu bora zaidi baada ya mapito yetu duniani". Padre Primo Mazzolari alitafsiri haya yote kwa kutualika kutazama juu na:sio kulia au kushoto, au katikati; lakini juu. Kuanzia kuwa watu wapya badala ya kuwa wadadisi wa mambo mapya.

Wanaume na wanawake wenye uwezo wa kuchukua wenyewe kwa uhuru na kuheshimu ahadi badala ya kufanya kama Pontio Pilato. Ambao hawabaki pembeni katika kupigania haki. Ambao hawabadilishi shauku kuwa chuki, haki kuwa muhtasari wa hesabu; ambao hawakatai hatima kwa njia ya vitu, hawakubaliani na utamaduni wa kubagua, hawahubiri ufumbuzi wa kiini macho; hawakatai utawala wa hisani katika siasa. Wanaume na wanawake ambao hawajidanganyi kwa kufikiria kwamba wanaweza kujenga mbingu duniani, ambao hawakosei siasa kwa changamoto ya kitambo ya nani atashinda na nani ashindwe, lakini wanaishi kama njia ambayo sisi sote tumeitwa. Wito wa kufanya vyema kila wakati.

Maneno ya Aldo Moro alipokuwa profesa kijana wa Chuo kikuu yanarudi akilini mwa Papa, kama kipimo cha uchunguzi wetu wa dhamiri: “Labda, licha ya kila kitu, mageuzi ya kihistoria, ambayo tutakuwa waamuzi wake, hayatatosheleza mahitaji yetu bora; ahadi adhimu, ambayo inaonekana kuwa ndani ya nguvu na uzuri wa asili ya maadili hayo, haitatimizwa.

Hii ina maana kwamba watu daima watalazimika kubaki katika hali ya mashaka zaidi au kidogo mbele kukabiliwa na sheria na Serikali. Na maumivu yao hayatafarijiwa kabisa. Lakini kutoridhika huku, maumivu haya, ni kutoridhika sawa kwa mtu na maisha yake,ambapo  mara nyingi sana na fInyu zaidi kuliko uzuri wake bora ungeonekana kupendekeza. Ni maumivu ya mtu ambaye daima hupata kila kitu kidogo kuliko angependa, ambaye maisha yake ni tofauti sana na ndoto bora. Ni maumivu ambayo hayapungui, ikiwa sio kidogo, yanaposadikika kwa roho zinazojua kuelewa au kuimba katika sanaa, au wakati nguvu ya imani au uzuri wa asili unaondoa wasiwasi huo na kurejesha amani. Labda hatima ya mwanadamu si kutambua haki kikamilifu, bali kuwa na njaa na kiu ya haki daima. Lakini daima ni hatima kubwa.”

09 July 2024, 15:57