Tafuta

2024.07.13 Askofu Mkuu Parra alibariki Ubalozi wa Vatican nchini Honduras. 2024.07.13 Askofu Mkuu Parra alibariki Ubalozi wa Vatican nchini Honduras. 

Peña Parra:Tumkabidhi Mama Maria wakati huu wa vita na umaskini

Katibu Msaidizi wa Vatican Askofu Mkuu Peña Parra akiwa Honduras kwa ajili ya ufunguzi wa Ubalozi wa Vatican huko Tegucigalpa,aliadhimisha misa katika Kanisa Kuu la Suyapa,mahali ambapo watu wa Honduras wanaheshimu Mama Maria kama Msimamizi wao:“tusali bila kuchoka ili alinde Kanisa,Papa,Nchi hii na ulimwengu wote.”

Vatican News.

Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Vatican ameomba kwa maombezi ya Mtakatifu mlinzi wa Honduras, (Nuestra Señora de Suyapa,) yaani Mama Yetu wa Suyapa, kwa wakati huu uliogubikwa na huzuni, hofu ya vita, na unyanyasaji wa nyumba yetu ya pamoja, umaskini wa kashfa na tabia ya kiburi ambayo inaathiri wengi majirani. Alisema hayo akiwa katika nchi ya Amerika ya Kati tangu tarehe 11 Julai 2024  kwa ajili ya kufungua tena Ubalozi wa Vatican katika mji mkuu wa nchi hiyo huko Tegucigalpa. Siku ya Ijumaa tarehe 12 Julai 2024 aliongoza sherehe katika makao makuu ya Uwakilishi wa Papa; na Jumamosi tarehe 13 Julai 2024, aliadhimisha Misa Takatifu mbele ya wajumbe wa Baraza la Maaskofu wa Honduras kwenye Basilika ya Suyapa, mahali patakatifu na pendwa kwa wakazi wa Honduras wanaoheshimu kama mlinzi wa Nchi hiyo.

Ziara ya Basilika mnamo 2011

Ni mahali pazuri pia kwa Katibu Msaidizi ambaye mwanzoni mwa mahubiri yake alikumbuka ziara yake katika Basilika hiyo nzuri mnamo 2011 kuwa: “Tangu mara ya kwanza nilihisi kukaribishwa na uwepo wa mama katika nyumba yake hii na pia kuzungukwa kwa upendo kutoka kwenu, dada na kaka wapendwa wa Honduras, ambao tangu mwanzo mlinifanya nijisikie nyumbani,”alisema.

Salamu kutoka kwa Papa Francisko

Zaidi ya miaka kumi baadaye, Askofu Mkuu Edigar Peña Parra alirudi katika maeneo haya “ili kulikabidhi Kanisa, Baba Mtakatifu na huduma yake kama mchungaji wa ulimwengu kwa maombezi ya upendo ya Maria Mtakatifu sana, Mama wa Mungu.” Kama alivyokuwa tayari Ijumaa tarehe 12 Julai amesema katika hotuba yake kwenye Ubalozi, hivyo aliwapatia salamu za joto kutoka kwa Papa, baba na mchungaji. Kwa mujibu wake alisema kuwa,  Jumanne iliyopita tarehe 9 Julai 2024 alimsalimia na kumjulisha kuhusu ziara hiyo na yeye: “alinipendekeza kwa uchangamfu kufikisha upendo wake na ukumbusho wake wa kudumu katika sala kwa watu wa Honduras na kuwaomba ninyi nyote kumwombea kwa  Mama yetu wa Suyapa.”

Maombi ya kutopotea katika njia za giza na mauti

Askofu mkuu Penna aliwaalika kutoa ombi zuri na la zamani  la iter para tutum, ili mlinzi wa Honduras aweze kulinda njia zao zote, “kuiweka salama na kutusaidia tusipotee katika njia za giza na vivuli vya kifo”. Kutokana na hiyo Askofu mkuu aliwatia moyo kusali bila kuchoka kwa “Mama yetu wa  Suyapa ili aweze kulinda Kanisa, Papa, taifa hilo  na dunia nzima na kwa utunzaji wa uzazi wa upendo na aendelee kuulinda na kuulinda utume ambao Mungu amekabidhi kwa kila mmoja wetu.” Matumaini ya Katibu Msaidizi wa Vatican ni kwamba “sote tunaweza kujitolea kuwa mashahidi wa upendo wa huruma wa Baba, wajenzi wa udugu na washiriki wa Bwana katika ujenzi wa ustaarabu unaosimikwa kwenye upendo.”

Askofu mkuu Parra huko Honduras

 

15 July 2024, 15:16