Tafuta

Chuo cha Kipapa cha Urbaniana, Roma. Chuo cha Kipapa cha Urbaniana, Roma. 

Saini ya Urbaniana na Baraza la Mawasiliano ya uzalishaji kisayansi wa uchapishaji

Mkataba wa usimamizi wa uzalishaji wa uhariri wa kisayansi katika Huduma ya Uchapishaji wa Chuo Kikuu cha Kipapa umetiwa saini tarehe 18 Julai 2024 na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.Ni Makubaliano yanayolenga kuzidi kuitikia utume wa Uinjilishaji wa Kanisa ambao unatajwa katika Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium.

Vatican News

Kuitikia kwa uthabiti mahitaji ya utume wa Uinjilishaji wa Kanisa ndilo lengo la Baraza la Kipapa la  Mawasiliano na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana  ambao wametia saini Alhamisi tarehe 18 Julai 2024, kuhusu mkataba wa usimamizi wa uhariri wa uzalishaji  kisayansi wa huduma ya uchapishaji ya chuo kikuu. Kwa msingi wa makubaliano haya yaliyotiwa saini na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk, Paolo Ruffini, na mjumbe wa Papa wa chuo kikuu, Vincenzo Buonomo kwa kazi zilizoundwa zitakuwa na alama iliyosajiliwa ya Uchapishaji wa  Chuo cha Kikuu Urbaniana pamoja na Nyumba ya Vitabu ya Vatican(LEV).

Makubaliano sambamba na Praedicate evangelium

Mkutano huo, kwa mujibu wa maelezo ya pamoja, unaendana na masharti ya Katiba ya Kitume ya ‘Praedicate evangelium’ yaani ‘Hubirini Injili’ ambayo kifungu cha 183 kinatoa muunganisho wa “hali halisi yote ya Vatican  katika nyanja ya mawasiliano,” ili mfumo mzima ujibu kwa mshikamano wa mahitaji ya utume wa uinjilishaji wa Kanisa.

Maono ya kimisionari ya kimataifa na mawasiliano baina ya tamaduni

Nyumba ya Uchapishaji ya Chuo Kikuu cha Urbaniana ni mrithi wa uchapaji wa Propaganda fide ambayo, tayari katika karne ya 17, ilikuwa na sifa ya maono ya kimisionari ya kimataifa. Ilikuwa, kiukweli, miongoni mwa machapisho ya kwanza katika herufi zisizo za Kilatini (kama vile Biblia Takatifu ya Kiarabu ya 1671) na kuhutubia hadhira ya kimataifa, ikivuka mipaka ya Ulaya katika harakati zake za umisionari na kuweka kwa ufanisi misingi ya mawasiliano kati ya tamaduni na hali isiyo na kifani kuenea kwa ujumbe na maarifa ya Kikristo.

Uboreshaji wa lugha za mashariki

Leo hii katika ulimwengu unaozidi kuunganishwa, dhamira hii ni muhimu zaidi kuliko hapo awali: inatosha kusema kwamba Nuyumba ya Uhapishaji ya Chuo Kikuu cha Urbanianiana imechapisha kwa lugha ya Kichina katika jarida lake kongwe, ‘Urbaniana University Journal-Euntes docete,’kila robo mwaka ilianzishwa mwaka 1948, na ambayo inapanga kuongeza uzalishaji wa kiutamaduni na kisayansi katika lugha nyingine za mashariki kama vile Kikorea, Kijapani, Kivietinamu na Konkani, zinazozungumzwa hasa nchini India.

Ubunifu wa kisayansi

“Kwa wito huu wa kimisionari wa kimataifa, kuheshimu tamaduni na utambulisho wao wa ndani kabisa kunaongezwa kuthaminiwa zaidi kwa jukumu la kichocheo la kisayansi na utafiti la Vyombo vya Habari vya Chuo Kikuu kwa kujitolea kwa utekelezaji wa mara kwa mara wa mazoea bora ya kitaaluma na kisayansi. uvumbuzi", kama inavyooneshwa kwa uwazi na katalogi ya chuo kikuu inayojumuisha majarida, miongozo ya kufundishia na mifurulizo  mahususi inayohusu mada ya umisionari katika aina zake zote. Bila kusahau kazi kubwa kama vile Katalogi ya Hati za Kichina katika Jalada la Kihistoria la "Propaganda Fide" ambalo lilifanya kupatikana kwa vyanzo vya maandishi ya Kichina vya thamani isiyo na kifani kwa ujenzi mpya wa historia ya Ukristo nchini China.

Makubaliano kati ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana na Baraza la Kipapa la Mawasiliano
19 July 2024, 15:55