Tafuta

2024.07.01 Kifuniko cha kitabu cha Kardinali Semeraro:"Wasindikizaji wa matumaini,"kilichochapishwa na LEV. 2024.07.01 Kifuniko cha kitabu cha Kardinali Semeraro:"Wasindikizaji wa matumaini,"kilichochapishwa na LEV. 

Kuanzia Paulo VI hadi Ulma,kitabu cha Wasindikizaji wa matumaini ya kikristo

Kinapatikana kitabu kuanzia Julai 1,2024:'Wasindikizaji wa Tumaini'kilichoandikwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na kuchapishwa na Nyumba ya vitabu,Vatican(LEV).Katika mtazamo wa Jubilei 2025,kinaripoti historia za wanaume na wanawake,watakatifu na wenyeheri wa enzi na tamaduni tofauti mashahidi wenye uwezo wa kutazama siku zijazo.

Vatican New

Papa Yohane XXIII na Papa Paulo VI, Mtumishi wa Mungu Madeleine Delbrêl, Mtakatifu Giuseppina Bakhita, Mwenyeheri Franz Jägerstätter na Mtumishi wa Mungu Kardinali François Xavier Nguyên Van Thuân, na Wenyeheri familia ya Ulma. Hawa ni wanaume na wanawake, watakatifu na wenyeheri, wahusika wakuu wa kitabu kipya cha Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Barazal a Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu kinachopatikana katika maduka ya vitabu kuanzia tarehe 1 Julai 2024. Kitabu kina kichwa: “Wasindikizaji wa tumaini. Historia ya mshahidi wenye uwezo wa siku zajazo,” kilichochapishwa na Nyumba ya vitabu ya Vatican (LEV).

Historia  na shuhuda

Historia na shuhuda zilizoripotiwa katika kitabu hicho, zenye manufaa kwa kuweka hai nuru ya  matumaini ambayo tumepewa, na kufanya kila kitu ili kila mtu apate tena uhakika wa kutazama wakati ujao kwa akili iliyo wazi, moyo wa ujasiri na mbali,  akili inayoona, kama alivyoonesha nia ya Papa Francisko katik Jubilei ijayo ya 2025, iliyojikita hasa kwa mada ya matumaini. Utu wema huu wa Kikristo ni wa kurukaruka, na ili mruko huu utokee, hamu inahitajika, ambayo Thomas Aquinas anaiita mfasiri wa matumaini. Hamu  ambayo lazima iombewe kwa maombi.

Mtindo wa tumaini la Kikristo

Katika kurasa za kitabu cha Kardinali Semeraro, maisha na kazi ya watu kutoka tamaduni na zama mbalimbali yameoneshwa ambapo inawezekana kutambua mtindo huu wa matumaini ya Kikristo, kwa kuonesha mifano na kutia moyo kutoka kwayo. Ni historia za wanaume na wanawake ambao wamepitia magumu sawa na sisi na sasa wanaishi katika kumbatio la Mungu kama vile Benedikto XVI alivyoandika, “katika majaribu mazito sana, ambayo lazima nifanye uamuzi wangu madhubuti wa kuweka ukweli mbele,” kuwa, kazi, kumiliki, uhakika wa kweli, tumaini kuu inakuwa muhimu. Hii ndiyo sababu tunahitaji mashahidi ambao wamejitoa wenyewe kabisa, ili kuwaacha watuoneshe sisi.” Kanisa linaundwa na kaka  na dada wasiohesabika, ambao mara nyingi hawajulikani majina yao, waliotutangulia. Mfano wao unatuambia kwamba maisha ya Kikristo si maisha ya kujua historia hizi za matumaini tu bali huleta hata faraja na kuaminiana.

Kitabu cha Kardinali Semeraro kuhusu watakatifu
02 July 2024, 16:00