Tafuta

Utatu Mtakatifu usiogawanyika: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Utatu Mtakatifu usiogawanyika: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. 

Utatu ni kisima cha huruma:Baraza limeridhia ujumbe wa Genovese kuhusu 'Utatu wa Huruma'

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa,ametuma barua na idhini ya Papa kwa Kardinali Oscar Cantoni,Askofu Mkuu wa Como kuhusu uzoefu wa kiroho wa Madhabahu ya Maccio inayohusishwa na maono ya Mwalimu wa Muziki na Mkurugenzi wa Kwaya Gioacchino Genovese.

VATICAN NEWS

Kuanza kutumika Kanuni mpya za kutambua matukio yanayodaiwa kuwa ya Kimungu, kunaruhusu njia mpya kutoka  Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Wakati huu ni rejeo la  tukio la kiroho la mahali Patakatifu huko Maccio katika Jumba la Guardia, katika eneo la Como nchini Italia. Ni mahali ambapo Gioacchino Genovese, Mwalimu  wa muziki na mkurugenzi wa kwaya, aliyeoa na baba wa mabinti wawili, alianza kutambua, kupitia maono ya kiakili, uwepo hai wa fumbo la Utatu Mtakatifu mnamo 2000. Mtu makini, mwenye busara ambaye halikuwa hajawahi kutafuta umaarufu wowote, miaka mitano baadaye aliomba kwamba watu wengine wahusishwe na ibada, maombi, na  novena. Baada ya uchunguzi wa awali wa maandishi ya Mwalimu  Genovese, kwa ujumla,  juu ya jambo hilo, mnamo 2010, Askofu Diego Coletti wa wakati huo wa Como alihusisha Kanisa la parokia sifa ya  mahali patakatifu na kupaita jina la Utatu Mtakatifu wa huruma.”

Barua ya Mwenyekiti wa Baraza la DDF

Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Mafundisho ya Tanzu ya Kanisa alituma barua tarehe 15 Julai 2024  kwa Kardinali Oscar Cantoni, Askofu Mkuu wa Como, ambayo imechapishwa kwa umma Jumatano, tarehe 24 Julai 2024 na ambaye alikuwa amemwomba uwezekano wa kutangaza idhini kwa jambo la Maccio kwa mujibu wa masharti ya Kanuni mpya. Katika barua hiyo, iliyoidhinishwa na Papa Francisko, Kardinali Fernandez alitoa ufafanuzi fulani juu ya maandishi ya Genovese.

Vipengele vyema

Kwanza kabisa, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa(DDF) anaorodhesha vipengele vyema vilivyomo katika ujumbe: “Utatu ni chanzo cha huruma na utambuzi wake kamili. Kwa kuzingatia usadikisho huo, yale yanayosemwa mara kadhaa kuhusu huruma ya Mungu au Kristo katika maandishi ya kiroho na katika Majisterio yanapata maana yenye nguvu ya Utatu. Na anafafanua juu ya kutengwa kwa fumbo la Utatu katika tafakari ya kitaalimungu na hali ya kiroho ya karne zilizopita kunajulikana sana. Kwa maana hiyo, “uzoefu wa kiroho wa Mwalimu Genovese unaendana na ugunduzi upya wa kiini cha Utatu Mtakatifu  kwa imani na maisha ya Kikristo ambayo yametokea katika karne iliyopita.” Katika maandishi ya Mwalimu Genovese “ukweli huu unaoneshwa kwa njia ya kusisitiza na ujumbe wa Huruma uliojaa uzuri unaobubujika kutoka Utatu. Katika Mwana wa Mungu aliyefanyika mwanadamu, tangu Umwilisho wake hadi leo hii, upendo usio na kikomo wa Ushirika wa Utatu unadhihirishwa kwa ajili yetu: “Ndani Yangu, Neno lililofanyika mwili, au Bibi-arusi wangu, mnaona na kugusa Upendo, Fadhili na Huruma Yangu, Mungu Mmoja, nanyi mnatafakari, lakini hamwezi kuelewa, isipokuwa ndani Yangu, Neno, au Bibi-arusi wangu. Zawadi ya Sisi UTATU (864)”. Katika haya yote sehemu za ujumbe zimetolewa tena katika barua hiyo , kama hii: “Mwili Wangu ni zawadi ya UTATU wa huruma! Neno langu ni zawadi ya UTATU wa Huruma!Shauku yangu ni ZAWADI ya UTATU  wa HURUMA! Ufufuko Wangu ni Zawadi ya  UTATU wa Huruma! Mimi ni huruma!” (49).

Sala ya Utatu

Kwa hiyo, hata kama Mwana pekee ndiye aliyejitwalia ubinadamu, Kardinali Fernandez anabainisha “Kanisa limeitwa kugundua tena zaidi na zaidi katika ishara za Kristo kwamba huruma isiyo na kikomo ya Mungu wa Utatu, ambaye katika maandishi ya Mwalimu Genovese anaitwa kwa jina la Utatu wa Huruma:” Hiki ndicho kitovu cha jumbe zote kwa sababu, hatimaye, ndicho kitovu cha Ufunuo.” Katika barua hiyo Kardinali pia anatoa sala hii, ambayo anaifafanua kuwa ni nzuri:”"Ni Wewe unayenitazama, unaniinamia, Unanivuta Kwako na, ukichukua uso Wangu ulioinama, unainua kuelekea Kwako na unasema ujitengeneze katika Moyo, Moyo Wako, ambapo Upendo ulio nao Kwangu unavuma ili niweze kuzama sikio langu katika mdundo huo wa milele na niweze kupumzisha kichwa changu kwa amani. Na tena, inua Uso Wangu ili niutazame Uso wako. Katika Wewe, mwanadamu Yesu, ambaye ni Mungu, Uso uleule wa Huruma ya Utatu ili, nikitazama machoni pako, niweze kukutumaini Wewe, Bwana Wangu na Mungu Wangu, kwa hivyo, tazama, ingawa mimi ni mwenye dhambi unaweza, ndani Yako, kuinua na kuweka macho bila woga. KWA HURUMA, KWA UPENDO WAKO USIO NA KIKOMO, MUNGU WANGU WA PEKEE, UTATU USIOPENYEKA WA FUMBO LISIOISHA LA UPENDO NDANI YAKO, ULIVYO! Ninakupenda Wewe na ndani Yako ninahisi kufanywa mpya na kusafishwa kutokana na uchafu elfu wa dhambi” (1331).

Vipengele vya kufafanua

Kuhusu vipengele vinavyopaswa kufafanuliwa, katika barua ya Kardinali Fernández kwa Askofu Cantoni inatukumbusha kwamba “kwa hakika si rahisi kamwe kujieleza kwa usahihi juu ya fumbo la Utatu Mtakatifu;  na ikiwa hii ni kweli kwa wataalimungu wakuu na kwa Majisterio ya Kanisa yenyewe, inakuwa ngumu zaidi wakati mtu anajaribu kuelezea kwa maneno ya kibinadamu kile kinachoishi katika uzoefu wa kiroho.” Genovese mwenyewe alitambua hili kwa uwazi wakati, akirejea maneno yake, alisema: “ anafahamu kutokuwa sahihi kwao, kama vile kila kitu nilichoandika hadi sasa kimekuwa kisicho sahihi.” Kinachoakisi ni misemo inayotumia wingi wa Utatu “Sisi” pia kurejea kufanyika mwili “Sisi kwa Huruma[...] tumefanyika mwili” (541). Maneno ambayo “hayakubaliki na mgawanyiko wao lazima uepukwe, kwani unaweza kufasiriwa kwa urahisi kwa njia iliyo kinyume na imani ya Kikatoliki”, ikizingatiwa kwamba ni Mwana pekee aliyefanyika mwili. Lakini hii, barua inaendelea kuwa, “haimaanishi kuhusisha makosa kwa maandishi yote ya Mwalimu Genovese.

Katika mengi ya maandishi, kwa hakika, hasa katika yale yanayofuata, tunapata ufafanuzi unaotuongoza kuelekea kwenye tafsiri sahihi.” Katika maandiko mengine tunaweza kusoma kwa hakika kwamba “katika umwilisho Utatu haukuchukua ubinadamu, lakini katika ubinadamu wa Neno, wa Kitenzi, sisi pia tunatafakari na kugusa Umungu wake” (1407). Kwa hiyo ni wazi kwamba “kwa upande mmoja, ni Neno pekee lililofanyika mwili na kwamba maandiko yote yanayojumuisha “Sisi” wa Utatu yanarejea uwepo wa kawaida na wa kudumu wa Nafsi hizo tatu, na kwa upande mwingine kwamba, hata kama Neno pekee litakalofanyika mwili, Nafsi zote tatu zinadhihirishwa kama Huruma ya  Fumbo la Kristo.”

Tafsiri sahihi

Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa anabainisha kuwa “Tunaweza kudumisha kwamba pendekezo la kiroho linalotokana na uzoefu uliosimuliwa na Mwalimu Gioacchino Genovese kuhusiana na Utatu wa Huruma  ikiwa inafasiriwa katika mwanga wa kile ambacho kimefanywa, alisema, kama inavyoungwa mkono na wataalamu mbalimbali walioshauriwa, haina mambo ya kitaalimungu au ya kimaadili kinyume na mafundisho ya Kanisa. Kwa vyovyote vile, lazima tuendelee kwa njia ambayo, katika uchapishaji wa anthology ya maandishi, maandishi yenye maneno ya kutatanisha yaepukwe ... na kwamba barua hii imewekwa kama utangulizi wa kukusanya.” Hatimaye, barua imebainishwa kwamba baadhi ya maandiko yanayorejea shetani “lazima yafasiriwe kuwa ni kielelezo cha Mungu ambaye hasahau kamwe kiumbe wake mpendwa, hata wakati kwa uhakika na kwa uhuru wake amejitenga na Yeye. Na imeongezwa kuwa maandiko mengine, yenye “takwimu  za wakati wa askofu au kwa watu wengine (maelezo juu ya tarehe, nyakati, mahali, na maelezo mengine ya kina) hayana manufaa kwa waamini wengine na hayawezi hata kuchukuliwa kuwa ya kimungu kwa baadhi, bila utambuzi makini wa watu wanaohusika.” Ujumbe wowote wa siku zijazo lazima utathminiwe na askofu “katika mazungumzo na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa.”

Barua kutoka Baraza la Kipapa kwa  Askofu

Thamani ya jumbe zilizopokelewa na Genovese, pamoja na lugha yao ya ishara, ni kujaribu kushinda utengano wa kupita kiasi kati ya Mafundisho ya Kristo na Taalimungu ya Utatu huku ikitualika kugundua “Utatu wa Huruma ambao unaoneshwa katika kila ishara ya Yesu. Wakati huo huo na kuchapishwa kwa barua kutoka Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa Askofu Mkuu wa Como ni Idhini ya kuanzisha na kwa uhuru wa chochote kulingana na vifungu vya Sheria mpya.

Maono ya Mwalimu Genovese kuhusu "Utatu wa Huruma"
24 July 2024, 10:13