Tafuta

Mzani mara nyingi ni ishara ya haki na usawa katika maisha. Mzani mara nyingi ni ishara ya haki na usawa katika maisha. 

Viganò atengwa na Kanisa

Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa limetangaza juu ya kutengwa(latae sententiae)kwa Balozi wa zamani wa Vatican nchini Marekani ambaye hatambui uhalali wa Papa na Baraza la mwisho la Mtaguso.

Vatican News

Askofu Mkuu Carlo Maria Viganò, aliyekuwa Balozi wa zamani wa Vatican  nchini Marekani, amepokea hati ya kutengwa na Kanisa kwa sababu ya kutaka kuacha ushirika na Askofu wa Roma na Kanisa Katoliki. “Tarehe 4 Julai 2024,  kama tunavyosoma  katika taarifa iliyotolewa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kuwa lilikutana ili kuhitimisha mchakato wa kesi ya jinai isiyo ya kisheria 1720 CIC kwa ajili ya “Monsinyo Carlo Maria Viganò, Askofu mkuu wa Ulpiana, “aliyeshtakiwa kwa uhalifu uliohifadhiwa wa mifarakano(Kifungu cha Kanoni 751 na 1364 CIC; Ibara ya 2 SST).”

Taarifa hiyo inaendelea: "Taarifa zake za hadharani zinajulikana ambayo inaonesha kukataa kwake kumtambua na kujisalimisha kwa Baba Mtakatifu, ushirika na washiriki wa Kanisa chini yake na uhalali na mamlaka ya Mafundisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican.”  Na "mwisho wa mchakato wa  kesi ya jinai, Viganò alipatikana na hatia ya uhalifu uliohifadhiwa wa mgawanyiko. Baraza  lilitangaza kutengwa na latae sentencentiae ex can. 1364 § 1 CIC. Kuondolewa kwa udhibiti katika kesi hizi kumehifadhiwa kwa Kiti cha Kitume.” Uamuzi huo uliwasilishwa kwa Askofu Mkuu tarehe 5 Julai 2024.

Kama inavyojulikana, mnamo Juni 20 mwaka 2023, ni askofu mwenyewe aliyefichua kikamilifu amri iliyomwita Roma ili kujibu tuhuma hizo na kumpatia uwezekano hadi tarehe 28 Juni 2024, kuteua wakili wa utetezi kumwakilisha au kutuma maelezo ya utetezi. Kwa kuwa hili halikufanyika, alipewa mwakili wa umma ambaye alitekeleza utetezi wa Viganò kwa mujibu wa kanuni za sheria.

Mara kadhaa, katika miaka ya hivi karibuni, Balozi wa zamani wa Marekani alitangaza kwamba hatambui uhalali wa Papa na Baraza la mwisho la Mtaguso wa II wa Vatican. Katika taarifa za hukumu ya mwisho ya kutengwa(latae sentencentiae) ni kutokana na kuhusisha na ukweli wa kuwa ametenda uhalifu.

Kwa kutengwa kwake anakatazwa kuadhimisha Misa na sakramenti nyingine; kupokea sakramenti; kusimamia sakramenti na kuadhimisha sherehe nyingine za ibada za kiliturujia; kushiriki kikamilifu katika sherehe zilizotajwa hapo juu; kutekeleza huduma za kiofisi au majukumu au huduma au kazi za kikanisa; kutekeleza hatua za serikali. "Maana ya kutengwa, hata hivyo, ni ile ya kuwa na adhabu kama dawa ambayo inakaribisha toba, kwa hivyo tunangojea kila wakati mtu huyo arudi kwenye ushirika." Taarifa imethibitisha.

05 July 2024, 15:32