Windsor,Uingereza timu ya kriketi ya Papa yachuana na ya kifalme!
Na Joseph Tulloch – London
Siku ya Jumatano, tarehe 3 Julai 2024 timu ya kriketi ya Vatican ilisafiri hadi Windsor, nyumbani kwa Mfalme Charles na wajumbe mbalimbali wa Familia ya Kifalme. Huko, walicheza na Timu ya Kriketi ya Mfalme XI, iliyojumuisha washiriki wa nyumba ya kifalme. Mechi hiyo ilikuwa kilele cha ziara ya Timu ya Vatican ikiongozwa na kauli mbiu: “Nuru ya Imani Uingereza”, ikiwa ni safari yake ya kumi ya ugenini tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2014 ambayo pia imeshuhudia wakicheza na timu ya Wazee ya Uingereza na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Maria.
Mchezo wa mvutano
Katika mechi hii, bao la polepole lilimaanisha mpira kuwekwa chini, na kusababisha matatizo kwa wagonga wa pande zote mbili. Vatican, ambao walifungua pambano, walipoteza kwa haraka, na ilibidi watoe alama ya mwisho ya 98 kwa 8. Lakini baada ya kucheza mara tatu iliweza kujimudu kwa kuchukia wiketi tatu, na kuwawekea wapinzani wao mikimbio saba. Kufika mizunguko kumi na mbili mvua ilianza kunyesha, na kusababisha matatizo kwa mipira yao. Ushirikiano wa nguvu na wiketi sita chini uliruhusu timu ya Mfalme XI kukusanya kwenye mikimbio. Wiketi nane na tisa zilianguka katika zaidi ya kumi na tisa, na mchezo ulikuwa wa usawa kwenye ukingo. Mwishowe, katika kipindi cha mwisho, Tumu ya Mfalme XI iliweza kupita na kushinda ikimaliza 99 kwa 9 na wakawa washindi.
Ujumbe kutoka kwa Papa Francisko na Mfalme Charles
Kabla ya mechi, Padre Eamonn O'Higgins, meneja wa kikosi cha Vatican, alikuwa amesoma ujumbe kutoka kwa Papa Francisko ambapo alituma salamu zake kwa timu zote mbili, na akaeleza matumaini yake kwamba tukio hilo lingekuwa tukio la “kujenga madaraja ya mshikamano wa kidugu, kukuza umoja wa Kikristo, na kuendeleza mipango ya ukarimu ya hisani." Kwa upande wa Mfalme Charles pia alikuwa ametayarisha ujumbe kwa hafla hiyo. Kwa njia hiy alisema kwamba hii ilikuwa mechi ya nne kati ya Vatican na timu ya kifalme, na akasema “alifurahi” kwamba pande hizo mbili “zimeunganishwa tena kwa kupenda kriketi. Akibainisha kwamba Vaticanini “mabingwa watawala”, baada ya kushinda mechi iliyotangulia, Mfalme aliongeza kuwa “anasubiri kwa hamu kusikia matokeo!
Mchezo: diplomasia katika ulimwengu uliogawanyika
Padre O'Higgins pia aliwasilisha barua na medali kwa Bwana John Spurling, mfanyabiashara wa Uingereza na mlezi wa timu ya Kriketi ya Vatican. Barua hiyo, iliyoandikwa na Kardinali Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu ambayo inasimamia timu ya kriketi – huku akimshukuru Bwana John kwa msaada wake wa ukarimu wa ajabu. Kardinali aliendelea kusisitiza umuhimu wa diplomasia ya michezo ya timu katika muktadha wa kile ambacho Papa Francisko anakiita vita vya tatu vya dunia vilivyogawanyika vipande vipande. Hii ilikuwa mada ambayo Chris Trott, Balozi wa Uingereza anayewakilisha nchi yake jijini Vatican aliichukua pia, katika mahojiano na Vatican News kuwa “mechi hiyo ilikuwa na mvuto mkubwa katika ngazi kadhaa, za kisiasa na kidini. Michezo hujenga urafiki na kushinda vikwazo, na mechi hii ni mfano mzuri wa hilo.”