Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo Jean Bosco Ntagungira, Paroko wa Parokia ya “Regina Pacis” iliyoko Kigali, Rwanda kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Butare. Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo Jean Bosco Ntagungira, Paroko wa Parokia ya “Regina Pacis” iliyoko Kigali, Rwanda kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Butare. 

Askofu Jean Bosco Ntagungira Jimbo Katoliki la Butare, Rwanda

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Philippe Rukamba wa Jimbo Katoliki Butare, lililoko nchini Rwanda la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo Jean Bosco Ntagungira, Paroko wa Parokia ya “Regina Pacis” iliyoko Kigali, Rwanda kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Butare. Alizaliwa mwaka 1964, Akapadrishwa Mwaka 1993 na kuteuliwa kuwa Askofu mwaka 2024.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Philippe Rukamba wa Jimbo Katoliki Butare, lililoko nchini Rwanda la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Monsinyo Jean Bosco Ntagungira, Paroko wa Parokia ya “Regina Pacis” iliyoko Kigali, Rwanda kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Butare. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Jean Bosco Ntagungira, alizaliwa tarehe 3 Aprili 1964 huko Kigali. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe Mosi, Agosti 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Kigali. Tangu wakati huo kama Padre alikuwa ni Mlezi, Seminari Ndogo ya Ndera kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1994.

Askofu Jean Bosco Ntagungira Jimbo Katoliki la Butare, Rwanda
Askofu Jean Bosco Ntagungira Jimbo Katoliki la Butare, Rwanda

Baadaye akatumwa kwenda Roma kwa ajili ya kujiendeleza kwa masomo ya juu kati ya Mwaka 1994 hadi mwaka 2001 na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano kilichoko mjini Roma. Aliporejea nchini Rwanda, akateuliwa kuwa “Kansela” wa Jimbo kuu la Kigali, Rais wa Tume ya Kiekumene Jimbo kuu la Kigali, Gambera wa Seminari Ndogo ya “Saint Vincent” Ndera. Na kuanzia mwaka 2002 hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni mjumbe wa Baraza la Kikanisa kwa Jimbo kuu la Kigali. Na tangu mwaka 2019 hadi kuteuliwa kwake, amekuwa ni Paroko wa Parokia ya “Regina Pacis” huko Kigali.

Watu wa Mungu kutoka Nchini Rwanda
Watu wa Mungu kutoka Nchini Rwanda

Itakumbukwa kwamba, Askofu Mstaafu Philippe Rukamba wa Jimbo Katoliki Butare alizaliwa tarehe 26 Mei 1948 huko Kabarondo. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 25 Julai 1974. Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 2 Januari 1997 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Butare, nchini Rwanda na kuwekwa wakfu 12 Aprili 1997. Baba Mtakatifu Benedikto XVI tarehe 28 Mei 2012 akamteuwa kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki Gikongoro hadi tarehe 26 Novemba 2014, utume huu ulipokufa rasmi. Kimsingi Askofu Mstaafu Philippe Rukamba wa Jimbo Katoliki Butare, nchini Rwanda, amelitumikia Kanisa kama Padre kwa takribani miaka 50 na kama Askofu kwa muda wa miaka 27. 

Uteuzi Rwanda
12 August 2024, 16:00