Askofu Mkuu John Joseph Kennedy Katibu Mkuu, Idara ya Nidhamu
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 29 Julai 2024 alimteuwa Monsinyo John Joseph Kennedy kuwa Katibu mkuu, Idara ya Nidhamu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu, Cheo binafsi. Askofu mkuu mteule John Joseph Kennedy alizaliwa tarehe 15 Julai 1968 huko Jimbo kuu la Dublin, nchini Ireland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Julai 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu, Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko mjini Roma.
Kuanzia mwaka 2003 aliteuliwa kuwa ni Afisa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Na tangu Mwaka 2017 akateuliwa kuwa ni Afrisa Mwandamizi Idara ya Nidhamu, Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Tarehe 23 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Katibu mkuu, Idara ya Nidhamu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na tarehe 29 Julai 2024 akampandisha hadhi na hivyo kuwa ni Askofu mkuu, Cheo binafsi.