Askofu Mkuu Philippe Curbelié Katibu mkuu Msaidizi Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 29 Julai 2024 amemteua Monsinyo Philippe Curbelié kuwa Katibu mkuu Msaidizi Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu, cheo binafsi. Askofu mkuu mteule Philippe Curbelié alizaliwa tarehe 13 Agosti 1968 huko Neuilly-sur-Seine, nchini Ufaransa. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 30 Aprili 1995 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Toulouse (Narbonne-Saint Bertrand de Comminges-Rieux), lililoko nchini Ufaransa.
Askofu mkuu mteule Philippe Curbelié Kunako mwezi Septemba 2012 aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa ni Afisa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki. Tarehe 5 Juni 2022 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Afisa Mwandamizi, Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Tarehe 6 Julai 2022 Baba Mtakatifu akamteuwa kuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na tarehe 29 Julai 2024 akampandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu.