Tafuta

Askofu Orthasie Marcellin Herivonjilalaina wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka, lililoko nchini Madagascar. Askofu Orthasie Marcellin Herivonjilalaina wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka, lililoko nchini Madagascar.   (Vatican Media)

Askofu Orthasie Marcellin Herivonjilalaina Jimbo la Ambatondrazaka, Madagascar

Askofu mteule Orthasie Marcellin Herivonjilalaina wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka, alizaliwa tarehe 13 Septemba 1979 huko Morarano Chrome nchini Madagascar. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kikasisi ndani na nje ya Madagascar tarehe 21 Januari 2006 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka. Kama Padre alijiendeleza kwa masomo ya juu, wakati huo akiwa ni Paroko-usu katika Parokia ya “Santa Maria Maddalena.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 14 Agosti 2024 alimteuwa Monsinyo Orthasie Marcellin Herivonjilalaina, Gambera wa Seminari kuu ya Falsafa ya Toamasina kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka, lililoko nchini Madagascar. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Orthasie Marcellin Herivonjilalaina wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka, alizaliwa tarehe 13 Septemba 1979 huko Morarano Chrome nchini Madagascar. Baada ya malezi na majiundo yake ya Kikasisi ndani na nje ya Madagascar tarehe 21 Januari 2006 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka. Kama Padre alijiendeleza kwa masomo ya juu, wakati huo akiwa ni Paroko-usu katika Parokia ya “Santa Maria Maddalena, huko Campo Calabro, nchini Italia kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2008.

Askofu Orthasie Marcellin Herivonjilalaina wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka,
Askofu Orthasie Marcellin Herivonjilalaina wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka,

Baada ya kurejea nchini mwake, kati ya Mwaka 2008 hadi mwaka 2009 aliteuliwa kuwa Gambera wa Seminari ndogo ya “Saint Pierre” Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka. Kati ya Mwaka 2011 hadi mwaka 2015 alijiendeleza zaidi na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu toka Chuo Kikuu cha Sophia, Loppiano, kilichoko nchini Italia na wakati huo huo aliendelea kuwa ni Paroko usu wa Parokia ya “Santa Maria Regina huko Matassino pamoja na Parokia ya “San Miniato huko Montanino. Kati ya Mwaka 2015 hadi mwaka 2021 aliteuliwa kuwa Gambera wa Seminari kuu la Falsafa ya “Saint François de Sales di Toamasina.” Mwaka 2021 aliteuliwa kuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya “Saint François de Sales di Toamasina.” Na ilipogota tarehe 14 Agosti 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka.

Uteuzi Madagascar
17 August 2024, 13:59