Tafuta

2024.08.23  Askofu Mkuu Fisichella katika Mkutano wa Rimini. 2024.08.23 Askofu Mkuu Fisichella katika Mkutano wa Rimini. 

Fisichella:katika hali ya chuki na kisasi,Jubilee ni njia ya matumaini

Katika Mkutano wa Rimini,Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji alizungumzia juu ya Mwaka Mtakatifu huku akielezea thamani ya tumaini na kusisitiza kuwa kusamehewa ni msamaha wa Mungu,zawadi ya bure kwa sababu siyo ya kununuliwa.Meya wa Roma,Gualtieri,alitangaza kwamba zaidi ya mahujaji laki moja kwa kila siku wanatarajiwa katika mji mkuu wa Italia wakati wa Jubili.

Na Benedetta Capelli – Rimini.

Tumaini na Msamaha: Haya ndiyo maneno mawili muhimu ambayo Askofu Mkuu  Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji na anayehusika na  maandalizi ya Jubilei ya 2025, aliyofafanua kwa wasikilizaji wa Mkutano wa  Urafiki kati ya Watu huko Rimini kuelezea Mwaka Mtakatifu ambao Papa Francisko alitangaza na Waraka wake wa Spes non confundit yaani(Tumaini halikatishi tamaa). Katika mkutano wa meza ya mduara kuhusu mada ya Jubilei ya 2025, Askofu Mkuu Fisichella alikumbuka mada ya mapitio ya Harakati ya 'Comunione e Liberazione' kwa kukumbuka kuwa “bila tumaini hatuwezi kufahamu mambo muhimu ya maisha, matumaini ni ya muhimu ya maisha ya Kikristo kwa sababu pamoja na imani na upendo inawakilisha mtindo wa mwamini.”

Tumaini ambalo linakuwa ishara

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Fisichella Asili ya tangazo la Jubilei iko katika umoja wa vipengele viwili: matumaini yenyewe lakini pia uwezo wa kuchangia, kutoa, kushiriki, kuweka ishara thabiti za matumaini.” Askofu Fisichella alikumbuka kwamba inamaanisha safari ya kibinafsi ya Kanisa zima, ya ubinadamu, na hii ndiyo sababu sisi ni mahujaji. Na zaidi katika kipindi kama hiki, ambacho kuna vurugu nyingi za kila siku.

Rehema, msamaha wa Mungu: “hakuna kitu cha kufaidika nacho”

Ni lazima ifutwe neno la Faida katika rehema. Sijawahi kutumia kitenzi hiki na ninatamani kisingetumiwa kamwe. Katika rehemu hakuna cha faida kwa sababu hakuna cha kununua. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu na Jubilei ni tangazo la msamaha mkuu ambao tumepewa.” Askofu Mkuu Fisichella alisisitiza na kukumbusha kwamba Papa Francisko katika Waraka wa kitume  wa maelekezo ya Jubilei, alisisitiza kwamba "msamaha haubadilishi yaliyopita, lakini unaweza kutusaidia kuishi vyema katika siku zijazo."

Ishara ya lazima ya kutazama mbele

Kwa kusisitiza zaidi Askofu Mkuu Fisichella alisema “Katika hali ya chuki, vurugu, kisasi, Jubilei inakuja kutukumbusha juu ya zawadi kuu ya Mungu Msamaha, unyenyekevu. Ni neema, na sio mafanikio. Kupata pesa haimaanishi chochote. Na uzoefu wa msamaha wa Mungu hutokea kwa njia ya safari: hija, kupitia Mlango Mtakatifu, ungamo la imani, na kazi ya upendo. Tangazo ni kwamba Mungu anakuja kukutana na wewe.”

Uzuri wa Injili

Akihitimisha mkutano huo, Askofu Mkuu Fisichella alikumbusha kazi kubwa ambayo haionekani katika kamati ya Maandalizi ya Jubilei na, alitumia mfano wa Olimpiki kueleza kuwa nyuma ya majukwaa daima huwapo dhamira kubwa isiyoonekana! “Kwa hivyo ikiwa ninaweza kuruhusiwa mlinganisho, wa kazi itapita ... jambo muhimu ni kwamba tupate kuishi uzoefu wa kushinda medali 40." Lakini shauku iliyomo moyoni mwake ni ile ya "Kanisa ambalo, liishi Jubilei kwamba: “naomba nisadikishwe zaidi kuhusu uzuri na wajibu wa kuleta Injili kwa kila mtu. Kwa sababu Jubilei ni usemi wa kipekee wa uinjilishaji.”

Gualtieri, kuingilia kati kwa maelewano na Mafundisho ya Papa

Pia kupitia kiunga cha video alikuwa kamishna wa Jubilei na Meya wa Mji wa  Roma, Bwana Roberto Gualtieri ambaye alizungumzia juu ya Mwaka Mtakatifu kama “changamoto inayofanya mikono yake kutetemeka," lakini pia kama fursa ya kiroho, na sio tu kuufanya mji mkuu wa Italia kuwa mzuri,na wa kujumuisha, lakini kwa maelewano na maadili yaliyooneshwa na Papa kama vile: mshikamano, ushirikishwaji, ulinzi wa kazi ya uumbaji, jukumu la kukaribisha kila mtu ili aweze kuwa bora iwezekanavyo.” Mahujaji milioni 33 wanatarajiwa, zaidi ya mahujaji 100,000 kwa kila siku, idadi muhimu ambayo Roma itakuwa tayari kupokea,” alisema Meya wa mji wa Roma.

Fisichella na Jubilei 2025
23 August 2024, 12:05