2024.08.05 Madhabahu ya Mama Yetu wa Afya Njema huko Vailankanni nchini India. 2024.08.05 Madhabahu ya Mama Yetu wa Afya Njema huko Vailankanni nchini India. 

Huko Vailankanni hakuna itikadi bali ni Mama anayekaribisha kila mtu!

Katika barua ya Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa katika matazamio ya Siku kuu ya Mama wa Afya huko Vailankanni nchini India:“Ni matunda mengi ya kiroho wapatayo mahujaji na hata wasio wakristo.Wale wasioweza kupokea sakramenti hawakatai faraja ya Mama wa Yesu.Papa anapongeza imani ya eneo hilo.”

Vatican News

Milioni ya mahujiji wanakwenda kwa imani katika Madhabahu ya Mama wa Afya, huko Vailankanni, katika Serikali Tamil Nadu  nchini India, “ni matunda mengi ya kiroho ambayo inatoka katika Madhabahu hiyo na uturuhusu kujua matendo yasiyo isha ya Roho Mtakatifu katika eneo hilo.” Ndivyo anaandika Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Kardinali Victor Manuel Fernández, katika barua iliyoandika tarehe 1 Agosti 2024 na kuridhiwa na Papa ambayo imetumwa kwa Askofu Sagayaraj Thamburaj, wa Tanjore, katika matazamio ya siku kuu ya Mama Yetu  Afya Njema mnamo  Sepemba ijayo ambapo ibada ya watu wa Vailankanni imeanza tangu karne ya XVI.

Tendo la Roho Mtakatifu katika mahujaji wengi wasio Wakristo

Haya yote  pia yanaoneshwa kwa mahujaji wengi wasio Wakristo wanaokuja kutafuta msaada. Baadhi yao wanaponywa magonjwa yao na wengi hupata amani na matumaini. Bila shaka, Roho Mtakatifu pia anafanya kazi ndani yao, akijibu maombezi ya Maria. Hii haipaswi kuchukuliwa kama aina ya kiitikadi au kuchanganya dini. Madhabahu ni mahali ambapo ukaribu wa Maria unadhihirika, ukimkaribisha kila mtu na kuonesha upendo wa Bwana kwa wale wanaomtafakari. Wale ambao hawawezi kupokea sakramenti za Kanisa Katoliki hawakunyimwa faraja ya Mama wa Yesu.” Anazidi kuandika Kardinali

Kuthamini kwa Papa nafasi hii ya imani

Kardinali Fernandez aidha katiika barua hiyo alikumbuka akiwa pamoja na Baba Mtakatifu Francisko, katika Mkutano wa  tarehe 1 Agosti 2024, juu ya uzuri wa kiroho wa mahali pale pa imani: “Baba Mtakatifu anajali sana uchaji wa mahujaji waamini, kwa sababu wanaakisi uzuri wa Kanisa linalosonga mbele linalomtafuta Yesu mikononi mwa Maria na kuacha maumivu na matumaini yake moyoni mwa Mama.” Kwa sababu hiyo “ Papa Francisko anaonesha shukrani kubwa kwa nafasi hiyo ya imani na, kwa kuzingatia maadhimisho ya mwezi Septemba katika Madhabahu ya  Vailankanni, anatoa baraka zake kutoka kwa Mungu kwa mahujaji wote.

Udhihirisho wa kwanza wa Maria

Kulingana na historia ya zamani, Bikira Maria alionekana kwa mara ya kwanza katika karne ya 16 kwa mvulana mmoja ambaye alikuwa amebeba maziwa ya mteja, na  aliimwomba amtolee maziwa  kwa ajili ya mtoto aliyekuwa amembeba mikononi mwake. Kijana huyo alikubali kwa urahisi, lakini mara tu alipomfikia mteja, hakukuwa na upungufu wa maziwa yaliyotolewa kwenye chombo chake. “Hivi ndivyo jinsi ukarimu wa wale ambao wana uwezo wa kutoa kitu kwa wengine na umaskini wao unaonyeshwa,” aliandika Kardinali. Na “kwa sababu sio lazima uwe na mambo mengi ili uwe mkarimu. Wito huu wa kushiriki, kusaidia, kuwa karibu na wale wanaotuhitaji daima usikike mahali hapo. Maria anapenda ukarimu wa watoto wake.”

Upole wa Maria, Mama wa wote

Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa anafafanua kuwa “mapokeo mazuri ambayo mahali hapa pa thamani pa ibada hukusanya katika baadhi ya mikutano ya Bikira na watoto maskini na wagonjwa. Hivi ndivyo upole na ukaribu wa Maria, ambaye Yesu alitaka kutuachia kama Mama wa wote, unavyodhihirika. Kupitia maombezi yake, Yesu Kristo mara nyingi humimina nguvu zake na kurejesha afya kwa wagonjwa.” Kardinali baadaye anakumbuka kwamba, kwa sababu hii, “mwaka 2002 Mtakatifu Yohane Paulo II alitaka Siku ya Wagonjwa Duniani iadhimishwe huko. Kwa sababu Bikira Maria yule yule aliyejidhihirisha huko Lourdes pia alijidhihirisha huko India kama Mama wa afya.”

Mbele ya Maria tunatambua upendo wa Yesu

“Sio tu kuhusu afya ya mwili, lakini pia ya roho. Kwa sababu mbele ya sura ya Maria tunatambua upendo wote wa Yesu Kristo ambao unaweza kuponya huzuni yetu, uchungu wetu, hofu zetu. Tukisimama mbele ya Maria, hata katika muda mfupi wa imani na upendo, mtazamo wake wa kimama unarejesha amani kwetu,” Amehitimisha Kardinali Fernández.

Bikira Maria katika Madhabahu ya Vailankanni
06 August 2024, 14:58