Tafuta

Picha ya ufunguzi wa Mlango mtakatifu wa Jubilei ya huruma tarehe 8 Desemba 2015. Picha ya ufunguzi wa Mlango mtakatifu wa Jubilei ya huruma tarehe 8 Desemba 2015. 

Jubilei 2025,baadhi ya ufafanuzi kuhusu ufunguzi wa Mlango Mtakatifu

Katika taarifa iliyotolewa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji, Sehemu ya Masuala Msingi ya Uinjilishaji Ulimwenguni,linatoa ufafanuzi fulani kuhusiana na uwezekano wa kufungua Mlango Mtakatifu katika makanisa makuu,madhabahu na mahali pengine pa kuabudia tofauti ya Basilika za Kipapa,kwa kuzingatia Jubilei 2025.

Vatican News

Ujumbe kutoka Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji unanuia kujibu swali lililoulizwa hivi karibuni, kutokana na mipango ya Jubilei ya 2025, ya kuweza kutazamia  ufunguaji wa Mlango Mtakatifu katika Makanisani Makuu, katika Maeneo ya Madhabahu ya  Kimataifa na Kitaifa na vilevile katika sehemu nyingine muhimu za ibada.” Kuhusiana na hamu hiyo, kifungu cha habari kinabainisha kwamba, pamoja na kuelewa  sababu za kichungaji na za ibada ambazo zinaweza kuwa zimependekeza, ni wajibu wake kukumbusha ishara sahihi zilizowekwa na Baba Mtakatifu katika Barua ya Papa (Bolla Spes non confundit,) ya maelekezo ya Jubilei ya 2025, ambayo inaonesha kama Mlango Mtakatifu ule wa Basilika ya Mtakatifu Petro na Basilika zingine tatu za Kipapa, ambazo ni Mtakatifu Yohane  huko Laterano, Maria Mkuu na Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta(Roma).

Matarajio: Papa atafungua mlango katika gereza 

Matazamio yanayotarajiwa ni hamu yaliyooneshwa na Baba Mtakatifu katika Barua yake ya kibinafsi ya kutaka kufungua Mlango Mtakatifu katika gereza ili 'kuwapa wafungwa ishara halisi ya ukaribu'. Maandiko ya Baraza la Kipapa  pia yanakumbusha kwamba “ishara ya kipekee na ya kutambua ya Mwaka wa Jubilei daima imekuwa ya kupokea Rehema kamili ambayo ina lengo la kueleza utimilifu wa msamaha wa Mungu usio na mipaka', kwa njia ya Sakramenti ya Kitubio na ishara ya upendo na matumaini.” “Katika lengo la kuishi kikamilifu  Mwaka Mtakatifu ujao tunahimiza - kurejea mahali fulani na njia tofauti zilizooneshwa na Hati(Dikrii) ya Toba ya Kitume ya tarehe 13 Mei 2024,”taarifa hiyo inahitimishwa.

05 August 2024, 17:43