Tafuta

Kardinali  José Tolentino de Mendonça ,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Elimu na Utamaduni. Kardinali José Tolentino de Mendonça ,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Elimu na Utamaduni. 

Kard.José Tolentino de Mendonça atembelea Scholas huko Barrio 31 Buones Aires

Kardinali de Mendonça,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu,alikwenda Barrio Buenos Aires,21 Agosti 2024 nchini Argentina kumfahamu mwanahistoria wa makao makuu ya elimu ya kimataifa ya Harakati la Scholas Occurrentes,lililoundwa na Papa Francisko mwanzoni mwa upapa wake,ambapo alisikiliza ushuhuda wa vijana wanaoshiriki katika mipango na walimu mbalimbali.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali José Tolentino de Mendonça,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, alifanya ziara ya ghafla katika makao makuu ya Scholas Occurrentes huko Barrio 31 Buenos Aires, nchini Argentina tarehe  21 Agosti 2024. Hapo aliweza kuzungumza na waanzilishi, wa Harakati hiyo, maprofesa José María del Corral na Enrique Palmeyro, ambao, pamoja na Kadinali Jorge Bergoglio, alipokuwa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Buenos Aires, walianza kuwaleta pamoja wanafunzi na walimu kutoka shule za dini mbalimbali na madarasa ya kijamii, ya umma na ya kibinafsi, ili kutoa Utamaduni wa kukutana katikati ya shida na migawanyiko ya 2001.

Uwajibu wa mchungaji 

Katika hafla hiyo, Kardinali alisikiliza shuhuda za vijana wanaoshiriki katika shughuli za kimichezo na kiutamaduni, pamoja na waalimu kutoka jumuiya za Scholas za sehemu mbali mbali za nchi, kama vile katika kitongoji cha Villa Fiorito, huko Gran Buenos Aires  na katika El Impenetrable, katika jimbo la Chaco. Mwishowe, akionekana kuwa na shauku juu ya kila kitu alichosikia, alitoa hotuba yake kuonesha furaha yake ya kuwa huko, mbele ya familia kubwa. Alisema kuwa picha ni ya thamani zaidi ya maneno elfu na mkutano huo, unaona hali hii ya kuishi pamoja, kuona macho, kuhisi matamanio, ni ya thamani zaidi ya maneno elfu. Alithibitisha kwamba ni wajibu kwa mchungaji kama yeye, ambaye ana jukumu hili ambalo Papa Francisko alimkabidhi, kuendelea kusaidia katika nyanja ya elimu na kitamaduni ambayo Scholas anaendesha.

Kardinali Mendoca akiwa katika Scholas Occurrentente huko Argentina
Kardinali Mendoca akiwa katika Scholas Occurrentente huko Argentina

Alishukuru kwa mkutano huo kwani ulimgusa sana na kuongeza mguso wa mchoro wa Ukuta  ulioundwa na vijana kutoka jumuiya ya Scholas ya  Barrio 31, ambapo wanaelezea ndoto na mateso yao. Jukumu alilotakiwa kulieleza ndilo lilikuwa uamuzi mgumu zaidi aliotakiwa kuufanya katika maisha yake. Katibu Mkuu wa Sera za Chuo Kikuu, Dk. Alejandra Alvarez, pia alitoa ishara, kuchora kumbukumbu ya kwanza ya maisha yake. Alichora mioyo miwili iliyounganishwa na mstari na kusema ilikuwa inarejea upendo ambao uliwaunganisha wazazi wake.

Scholas ni Harakati ya kipapa 

Hata hivyo mnamo Mei mwaka huu 2024, Kardinali Tolentino alihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Hisia ulioandaliwa na Scholas Occurrentes katika Jiji la Vatican, ambapo maelezo zaidi ya taasisi hii mpya ya chuo kikuu iliyoundwa na agizo la Baba Mtakatifu, iitwayo Chuo Kikuu cha Sense. Kwa hisia kali, mkuu wa Scholas huko Barrio 31 alishukuru kwa ziara hii ya kihistoria na kwa msaada wake na idara yake kwa kuendelea kwa kazi ya elimu na kitamaduni ya Scholas duniani. Makao makuu ya kihistoria ya Scholas huko Barrio 31, yaliyozinduliwa mnamo mwaka 2018 na Papa Francisko mwenyewe kwa njia ya Mkutano wa Video na jumuiya inayoleta pamoja sio tu familia za Barrio 31,  lakini pia ambapo inawezekana kuhudhuria vyuo vikuu vingine (UBA CBC). Zaidi ya hayo, shughuli za michezo kama vile (Liga Internacional de Fútbol Pelota de Trapo,) mpira wa wavu, ndondi na shughuli zingine hufanyika. Katika ukumbi huo huo, shughuli za kisanii na kitamaduni pia hufanyika ambazo huleta pamoja jamii nzima na ambayo wasanii mbalimbali wa kimataifa hushiriki, kama vile Sebastian Yatra, miongoni mwa wengine.

Septemba ijayo uzinduzi wa Scholas huko Indonesia

Vile vile, maonesho ya (Teatro Colón)yanafanyika katika ukumbi wa Scholas del Barrio 31, na kila mwaka wajumbe wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Yerusalemu, miongoni mwa taasisi nyingine kuu za kitaaluma za kimataifa, hushiriki.  Scholas sasa yuko katika mabara matano, na kushiriki moja kwa moja katika nchi 70 na katika siku chache zijazo itazinduliwa, pamoja na Papa Francisko, makao makuu ya kwanza ya Scholas Kusini-Mashariki mwa Asia nchini Indonesia wakati Papa atakapotembelea nchi hiyo mwezi Septemba 2024.

Kardinali de Mendoca kutembele Scholas huko Barrio 31 Buones Aires
22 August 2024, 14:30