2024.08.11 Kardinali Parolin katibu wa Vatican aliongoza ibada ya Misa Takatifu huko Assisi katika sherehe za Mtakatifu Chiara. 2024.08.11 Kardinali Parolin katibu wa Vatican aliongoza ibada ya Misa Takatifu huko Assisi katika sherehe za Mtakatifu Chiara. 

Kard.Parolin atoa wito wa amani huko Assisi:Vita havina faida yoyote!

Katibu Vatican,Kardinali Parolin,11 Agosti 2024, akiwa katika mji wa Assisi katika siku kuu ya Mtakatifu Clara alisema: "Yeye,mfano wa maisha katika jamii yetu iliyoainishwa na utumiaji hovyo,ubinafsi,uchafuzi wa mazingira,utafutaji usiozuiliwa ili kukidhi mahitaji yanayotokana na matangazo na kuiga mitindo”.Alijibu maswali ya waandishi juu ya shambulio la Ukraine huko Kursk:"Kuna matukio ya kutisha na hatari ya amani."

Vatican News

“Kutoka Assisi, katika tukio hili ninataka kuzindua maombi ya nguvu na ombi la amani duniani kote. Kama Baba Mtakatifu alivyosisitiza mara kadhaa, vita ni kushindwa kwa kila mtu na havileti faida kwa mtu yeyote. Haya ndiyo aliyosema Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, Dominika tarehe 11 Agosti 2024 huko Assisi ambako aliongoza maadhimisho ya sherehe ya misa Takatifu kwa ajili ya Siku kuu ya Mtakatifu Klara, katika Kanisa lililowekwa wakfu kwake.

Wasiwasi juu ya kukera huko Kursk

Kardinali Parolin alirudi hivi karibuni kutoka kwenye utume  huko Ukraine mnamo Julai ambao ulimpeleka Kyiv, Odessa na Lviv, alijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari wa eneo hilo kando ya sherehe, kuhusu moja ya shambulio lililoanzishwa na Ukraine katika mkoa wa Kursk wa Urusi.  “Haya ni maendeleo yanayotia wasiwasi sana, kwa sababu inamaanisha kufungua nyanja mpya,” Kardinali huyo alisema. "Kwa maana hii uwezekano wa amani unazidi kuwa mbali.” Kardinali Parolin pia alizungumza kuhusu vita katika mahubiri  yake, ambapo alizindua tena wito kwa ajili ya amani duniani. Katika kumshukuru Askofu, Domenico Sorrentino, Waklara Maskini, Ndugu Wafransiska wadodo wa kiume  na watawa wote , mamlaka kuu ya kiraia,maaskari na maelfu ya waamini waliohudhuria sherehe hiyo, Katibu wa Vatican kisha alitaka kusisitiza haja ya kupenda katika ulimwengu unaozidi kuwa maskini katika upendo kwamba "kuna njaa ya upendo inayozidi.”

Mfano wa umaskini wa Mtakatifu Clara

Kardinali huyo akiendelea na dhana ya upendo, alitilia mkazo juu ya chaguo zito la Clara la umaskini, "ambalo linajionesha kuwa kielelezo cha maisha katika jamii yetu, kinachotambulika kwa utumia hovyo, yaani utafutaji usiozuilika wa kukidhi mahitaji yanayochochewa na shinikizo la matangazo na kutoka kwa matukio ya uigizaji wa kijamii, pamoja na upotevu wa kiuchumi usioepukika, uchafuzi wa mazingira, ambao unazingatia furaha kama wema mkuu wa mwanadamu na madhumuni ya pekee ya maisha.

Kuiga mfano wa Mtakatifu Clara

Hata kwa waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa sherehe, hiyo Kardinali Parolin alikuwa amesisitiza haja ya "kujitahidi kama Clara na Francis walivyofanya:" sio mali nyingi za kimwili, lakini ubinafsi, nafasi za mtu mwenyewe na kujifanya kuwa wazi kwa wengine hasa ikiwa ndiyo njia ya kidugu na ya amani."

Kardinali Parolini huko Assisi 11 Agosti

 

11 August 2024, 16:39