Kardinali Pizzaballa wakati wa mahojiano. Kardinali Pizzaballa wakati wa mahojiano. 

Kard.Pizzaballa:amani ni ngumu leo hii bali kuna hitaji la kusitishwa mapigano haraka

Huko Rimini,katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vatican kabla ya kuzindua Mkutano,Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu alizungumza juu ya matumaini madogo yaliyopo Nchi Takatifu,msingi wa kutokubali vurugu:"tunafanya kazi ya kusaidia jumuiya ya Kikatoliki huko Gaza na Ukanda wa Magharibi kwa kupeleka chakula,kuna utamaduni wa kukuza upatanisho ili kuepuka vazi la ukandamizaji ambalo limezalishwa."

Vatican News

Hatuwezi kuzungumza juu ya amani kwa sasa Ni maneno ya Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, yanaonesha kwa uwazi hali iliyojitokeza katika Nchi Takatifu na mzozo ambao umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa kati ya Hamas na Israeli. Akizungumza na vipaza sauti vya vyombo vya habari vya Vatican  kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa  Urafiki wa Watu Rimini  tarehe 20 Agosti 2024,  ambapo Kardinali aliufungua  mkutano huo kwa  mada: “Uwepo wa Amani”, alisisitizia haja ya kufanyia kazi usitishaji mapigano, kukatiza shughuli za jeshi kuanza, mchakato wa uponyaji, na kujenga kuaminiana kati yao. "Njia ipo  lakini hakuna hamu ya kuifuata katika ngazi ya kitaasisi, inahitaji uongozi wa kisiasa na wa kidini ambao uko kwenye shida. Ni muhimu, kufanya kila linalowezekana hata kuanzia chini,”alisema Kardinali Pizzaballa.

"Matumaini madogo"

Matumaini ni neno linalohitajika wakati huu lakini, alisema Kardinali, kuwa hatupaswi kuchanganya maana ya maneno. "Matumaini haimaanishi kuwa mambo yanakaribia kuisha, matarajio si mazuri kwa muda mfupi. Matumaini ni mtazamo wa ndani unaotuwezesha kuona kwa macho ya Roho kile ambacho macho ya mwanadamu hayaoni.” Matumaini madogo yanahuisha Kanisa mahalia, linalojishughulisha na Gaza na Ukanda wa Magharibi katika kusaidia jumuiya ndogo ya watu wapatao 600 kwa usambazaji wa chakula. Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu alikumbuka ahadi ya kufungua kliniki, shule ambayo imefungwa kwa mwaka mmoja, ili kuanzisha upya mienendo ya mahusiano ya kawaida, lakini ambayo inasaidia kutoroka kutoka katika vazi la ukandamizaji ili kuunda kazi, fursa hata kama hazipo.”

Amani ni utamaduni

Akihitimisha mahojiano yake, Kardinali Pizzaballa alikumbuka kwamba kila mtu anaweza kufanya kitu ili kuleta amani. “Amani ni utamaduni, si jambo la lazima mtu afanye, ni siasa, ni elimu, ni dhamira ya vyombo vya habari, inafanya kazi kwa digrii 360, katika ulimwengu wa utandawazi ambao hakuna mtu kisiwa. Amani ni utamaduni."

Mazungumzo, ni treni ya mwisho

Katika hatua ya Mkutano, katika mazungumzo na rais wa  Mfuko wa Mkutano wa Urafiki Kati ya Watu, Bernard Scholz mkutano ambao ulizindua kwa ufanisi toleo la 45, Kardinali Pizzaballa alifafanua kwa upya miaka 35 ya maisha yake  ya utume katika Nchi Takatifu na ukuaji wake katika majadiliano ya kidini. Rejea ya matukio ya sasa haiwezi kuepukika, "tuko katika wakati wa maamuzi, na mazungumzo yanayoendelea," alisema, "vita vitakwisha, natumaini kuwa kwa mazungumzo hayo, jambo hilo litatatuliwa: Nina mashaka yangu, lakini ni treni ya mwisho". Hata hivyo Patriaki hafichi hatari ya kuharibika. Lugha ya kukataliwa - imekuwa jambo la kila siku ambalo linaweza kusikika kwenye vyombo vya habari na ni jambo la kushangaza kweli. Ushauri wake ni kuomba zaidi ya yote ili kukabiliana na "mielekeo hiyo ya chuki, kutoaminiana na dharau kuu" ambayo inahisiwa. Kuijenga upya kesho kutahitaji kujitolea kwa kila mtu. Kuhusu mazungumzo ya kidini, Kardinali Pizzaballa - hafichi shida kwa wakati huu. "Hali hii ni maji, hakuna mikutano ya hadhara, katika ngazi ya taasisi tunatatizika kuzungumza sisi kwa sisi. Hatuwezi kukutana." Mwaliko wa mwisho ni kwa ajili ya mazungumzo ambayo ni ya kijamii zaidi na sio ya wasomi. Viongozi wa kidini wana jukumu kubwa katika kuunda jumuiya ambazo hazijifungi lakini badala yake huinua macho yao.

Kardinali Pizzaballa

 

21 August 2024, 16:09