Kard.Tagle huko Bibione:Tuwe shuhuda na vyombo vya huruma!
Na Angella Rwezaula -Vatican.
Mwaliko wa huruma, upatanisho na msamaha katika ulimwengu unaotamani amani ulidhihirisha katika ziara nzima ya Kardinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji ambaye aliongoza maadhimisho Jumamosi tarehe 3 Agosti 2024 uzinduzi wa Msamaha katika mji wa Bibione Jimbo katoliki la Concordia-Pordenone. Ziara ya Kardinali huyo pia ilisukumwa na kumbukizi ya Kardinali Celso Costantini, aliyewahi kuwa mjumbe wa kwanza wa kitume nchini China na Katibu wa Propaganda Fide, ambaye aliyezikwa jimboni kwake , miaka mia moja baada ya maadhimisho ya Mtaguso wa Concilium sinense ya Shanghai, ambayo tayari yameadhimishwa katika matukio makubwa mawili ya mwezi Mei na Juni katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana.
Dunia yetu inahitaji sana huruma,upatanisho na msamaha unaoleta amani
Akikaribishwa na kusindikizwa na Askofu wa jimbo hilo, Giuseppe Pellegrini, Kardinali Tagle alifungua Mlango wa Msamaha na kuingia kwanza akiwa amebeba kitabu cha Injili, huku na watu wote. Kisha aliongoza Ibada ya Ekaristi, iliyohitimishwa na mapadre wengi, majimbo, wageni na washiriki kwa ajili ya shughuli ya kichungaji ya majira ya kiangazi katika eneo la mapumziko maarufu ya bahari kwenye pwani ya Veneto. Kuanzia kwa usahihi kutoka katika sura ya Costantini, Kardinali Tagle aliendeleza tafakari yake, akikumbuka uaminifu wake kwa Injili ya huruma na bidii yake ya kimisionari ambayo bado inatia moyo hadi leo. Kisha, Kardinali alikazia usomaji wa kiliturujia, ambayo kila moja inaonesha kipengele cha huruma ya Mungu: “Dunia yetu inahitaji sana huruma, upatanisho na msamaha unaoleta amani. Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kutoa zawadi hizi,” alisema Kardinali Tagle. Sisi, wanafunzi wa Yesu, tumeitwa sio tu kuwa wapokeaji wa huruma ya Mungu tu, lakini pia kuwa mashahidi wake wa kweli na vyombo: Tumepokea rehema nyingi kutoka kwa Mungu, angalau kwa sehemu ndogo tujaribu kuwamiminia ndugu zetu.”
Je tunaishije na watu wanakabiliwa na matatizo?
Kardinali Tagle akitafakari juu ya maisha ya kila siku, alihimiza uchunguzi wa dhamiri kwamba: “Je, tunaishije na watu wanaokabili dhoruba na kuchanganyikiwa maishani? Kwa wasiwasi au kwa kutojali? Je, tunakabiliana vipi na vijana na wakosoaji wanaotutilia shaka na kuhoji misimamo yetu? Kwa unyenyekevu au kwa kiburi cha kulipiza kisasi? Je, tunaitikiaje maombi ya msaada kutoka kwa wagonjwa, wazee, wakimbizi na watu tofauti na sisi? Kwa huruma au kwa sikio kiziwi? Tujifunze kutoka kwa Yesu.” Huruma iliyooneshwa na Mungu inapaswa kuwa kanuni ya maisha katika familia na jumuiya za Kikristo na hata katika mahusiano kati ya mataifa. Fikiria ulimwengu ambao wale wanaofanya makosa wanasahihishwa kwa rehema badala ya kulaumiwa na kuangamizwa.” Kwa njia hiyo “Hebu wazia ulimwengu ambapo wanyonge wanaungwa mkono badala ya kudanganywa. Hebu tuwazie ulimwengu ambapo mazungumzo yanashinda kulipiza kisasi. Hebu tuwazie ulimwengu ambapo kila mtu anachangia kwa manufaa ya wote badala ya kutafuta maslahi binafsi.” Kwa hiyo, mwaliko wa mwisho ambao Kardinali Tagle aliutoa ni kwamba: “Bila huruma ulimwengu hautaona haki, ukweli, upendo na amani. Chagua huruma. Eneza huruma. Ishi huruma.”