Tafuta

Roma: bandiera ya Ulaya Katika Ubalozi wa Ukraine kuunga Mkono Kiev Roma: bandiera ya Ulaya Katika Ubalozi wa Ukraine kuunga Mkono Kiev  (ANSA)

Mkutano wa Rimini,Balozi wa Vatican huko Kyiv:hapa ni ishara ya kutoa matumaini

“Ikiwa unataka amani,tayarisha amani.”Ni maneno yaliyosemwa na Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas Balozi wa Vatican Nchini Ukraine katika meza ya mduara huku akikimbuka mwanzo wa uvamizi wa Urusi na kusisitiza ishara nyingi za mshikamano zinazowafanya watazame tufanya siku zijazo kwa ujasiri.

Na Benedetta Capelli – Rimini.

Ishara za fadhili ambazo katika muktadha wa vita huwa ishara za kishujaa, na matunda ya mawazo ya hisani. Ni mawazo ya Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas, Balozi wa wa Vaticani huko  Kyiv, nchini Ukraine alivyozungumza  katika Mkutano wa Watu huko Rimini  uliofunguliwa tarehe 20 na utahitimishwa tarehe 25 Agosti 2024, ambapo alisema: “Ikiwa unataka amani, tayarisha amani.” Hadhira kubwa ilisikiliza historia yake,kupitia kiungo cha video, kwa kuakisi janga la muktadha ambao hunawafanya wale wanaoishi katika maeneo hayo kuteseka. Askofu Mkuu Kulbokas alikumbuka ukarimu wa mwanamke wa Kiukraine ambaye, kutokana na usaidizi wa marafiki wengi, alipeleka msaada wa dola milioni 60 kwa nchi. Askofu Kulbokas  aliongeza kusema: “Kisha kuna aliyeshirikiana na kila mtu, muungwana ambaye anaamini lakini hajihusishi na Kanisa lolote. Aliniambia jinsi alivyosaidia watu 280 kutoroka.” Balozi huyo vile vile aliwakumbuka wale watu 800 waliohamishwa kutoka Mariupol kutokana na uamuzi wa Parokia ya Kiprotestanti. “Hii ndiyo sababu kwa nini ninaweka matumaini yangu katika jumuiya ya kiraia ambayo inatilia maanani changamoto na yenye uwezekano zaidi wa kuwa mchambuzi.” Alisema

Zifahamu ishara

Jumuiya ya kiraia yenyewe ina uwezo, wa kuelewa hatari ya hali zingine kwanza. Kwa mujibu wa Balozi alisema: “Kulikuwa na dalili kwamba kuna kitu kibaya. Mimi pia nilidharau maendeleo ya michakato fulani, lakini maisha yanatufundisha kwamba tunapokabiliwa na changamoto kubwa, lazima juhudi pia ziwe kubwa, hapa ndiyo maoni yangu kwamba taasisi za kila aina zina ugumu wa kuzaliwa katika kutarajia. Kinyume chake Watu badala ya taasisi wanaweza kutambua dharura. Ni kweli, hata hivyo, kwamba vita havifuati sheria yoyote na kwa sababu hii taasisi hazijajiandaa.”

Usikate tamaa

Pia katika meza ya mduara alikuwapo Oleksandra Matvijcuk, wakili wa Kiukraine na kiongozi wa shirika la haki za kiraia lililoko Kiev, Kituo cha Uhuru wa Kiraia, ambacho kilipata Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 2022. Oleksandra aliripoti ushuhuda wa ghasia zilizotokea nchini na mwaliko wake kwa jamii ulikuwa wa ujasiri, kutekeleza ishara za mshikamano, kielelezo cha ubinadamu ambao haubaki tofauti na shida za wengine.

Historia za wasimamizi wa shirika lisilo la kiserikali la 'Emmaus'

Historia  za kugusa za Lali Liparteliani na Anastasia Zolotova, wasimamizi wa shirika lisilo ya Kiserikali(NGO) ya Kiukreni “Emmaus, pia walihusika katika uhamishaji wa watu wenye ulemavu. Wote wawili walikumbuka hali ya kutengwa iliyohisiwa, kupoteza utambulisho kwa sababu ya vita lakini pia asili kali ya ndiyo kwa Kristo, nguvu ya kushikilia ili kuwa na matumaini ya kesho yenye amani."

22 August 2024, 16:23