Mwaka mmoja wa WYD,Lisbon 2023:picha na maneno ya mkutano na Yesu hai
Vatican News
Sauti ya Baba Mtakatifu ikiwasihi washiriki milioni moja na nusu wasiogope yajayo, nyuso za mahujaji waliokuja Lisbon kutoka pande zote za dunia na muziki wa wimbo "Ai pressa no ar": ndivyo viungo vya video iliyochapishwa tarehe 6 Agosti 2024 kwenye Tovuti rasmi ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha kuhusu Siku ya Vijana Duniani, katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja wa Siku hiyo iliyomalizika tarehe 6 Agosti 2023 huko Lisbon nchini Ureno.
Kardinali Aguiar:Ilistahili,kwa sababu tulikuwa Kanisa lililo hai la Bwana Wetu
Akitoa maoni yake Mratibu Mkuu wa Siku ya Vijana Duniani ya Ureno(WYD), Mwadhama Kardinali Americo Manuel Alves Aguiar, alisema kuwa “Mwaka mmoja baadaye ninatazama nyuma na ilikuwa na thamani yake. Kila siku, kila safari, kila mkutano tena na kumekuwa na maelfu ya kila sherehe.
Mwaka mmoja baadaye, kama kawaida mwishoni mwa kila Siku ya Vijana Ulimwenguni, hakuna mtu anayeweza kufikiria matunda yanayoweza kuzaliwa na kukua katika maisha ya mahujaji vijana, Makanisa mahalia au hata Kanisa la Ulimwengu. Hatuna uwezo wa kufanya hesabu kama hizo tunapozungumza juu ya maisha ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. Hata hivyo, hatua kwa hatua, katika maisha ya kawaida ya Kanisa, Mungu anafanya kazi kubadilisha maisha ya kila mtu.
Kardinali Aguiar, aliendelea kueleza kuwa: “Ilistahili, zaidi ya yote, kwa sababu tulikuwa Kanisa lililo hai la Bwana Wetu na ambaya huimba, kuomba na kulia. Ambaye anafurahi, huzuni, amejaa tumaini na uaminifu. Anayeungana tena ndani ya Yesu na Yesu aliye hai.” Ambao hukusanyika karibu na Mchungaji na kufurahi tu kumwona akipita. Kanisa lililo hai la Bwana Wetu, ambapo sisi sote ni wana na binti wapendwa, wote, wote, wote.”
Novemba,alama za WYD kutoka Lisbon kwenda Seoul-Korea Kusini
Sasa, kwa jicho la kuelekea Seoul 2027, kuvuka Jubilei ya Vijana mwaka 2025 ambapo Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha linaendelea kusindikiza na maandalizi ya Siku ya Vijana duniani inayokuja kwa kiwango cha Makanisa mahalia, ambayo itaadhimishwa kwenye Maadhimisho ya Kristo Mfalme, Dominika tarehe 24 Novemba 2024. Katika tukio hilo, alama za mkutano zitapitishwa na kukabidhiwa ambazo ni msalaba na nakala ya Picha ya Maria ya Salus Populi Romani (Maria Afya ya Waroma) kutoka kwa vijana wa Lisbon kuelekea kwa vijana wa Seoul.