Tafuta

2021.12.13  Baraza la Kipapa la Hati za kisheria . 2021.12.13 Baraza la Kipapa la Hati za kisheria .  (Vatican Media)

Papa amemteua Mons.Tuomo T.Vimpari kuwa katibu wa Nyaraka za kisheria

Jumatano tarehe 7 Agosti 2024 Papa amemteua Monsinyo Vimpari kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Nyaraka za Kisheria.Hadi uteuzi huo alikuwa mshauri wa Balozi wa Vatican nchini Romania na Moldavia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Jumatano tarehe 7 Agosti 2024 amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya  Nyaraka za Kisheria, Mheshimiwa Monsinyo Tuomo T. Vimpari, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa mshauri wa Ubalozi wa Vatican nchini Romania na  Moldavia.

Wasifu wake

Monsinyo Vimpari alizaliwa tarehe  29 Agosti 1968 huko Nokia (Finlandia) na alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 22 Mei 1999 kwa ajili ya Jimbo la Helsinki. Aliendelea na mafunzo na kupata digrii ya Sayansi ya Siawa katika Chuo Kikuu cha Helsinki na Udaktari wa Sheria za Kanoni katika Chuo Kikuu cha Gregoriana Roma (Italia). Katika jimbo lake kati ya mambo mengine amefunika nyadhifa za makamu jimbo. Mnamo tarehe 1 Julai 2006, bada ya masomo katika Taasisi ya Elimu ya Kikanisa Jijini Roma aliingia kufanya huduma ya kidiplomasia ya Vatican na kuendelea na shughuli za uwakilishi wa Kipapa katika Nchi ya Ukraine, Ujerumani, India na Nigeria na katika kitengo cha Masuala Makuu katika Ofisi ya Katibu wa Vatican. Hadi uteuzi alikuwa Mshauri katika Ubalozi wa Vatican nchini Romania na Moldavia.

Papa amemteua Katibu wa Baraza la Hati za kisheria
07 August 2024, 16:55