Papa Francisko akutana na Rais wa Malawi Bwana Chakwera
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu tarehe 19 Agosti 2024, Ofisi ya Vyombo vya habari, Vatican imeota taarifa kuwa Baba Mtakatifu Francisko amekutana katika Jumba la Kitume na Rais wa Jamhuri ya Malawi Bwana Lazarus McCarthy Chakwera ambaye amefika na kukutana mjini Vatican kuanzia saa 3.00 asubuhi na mazungumzo yaliyodumu kwa dk. 20 na kuondoka saa 3.35.
Baada ya Mkutano huo, Rais huyo pia alikuwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Masuala ya Uhisiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.
Katika mazungumzo yao na Sekretarieti ya Vatican, wameonesha mahusiano mazuri kati ya Vatican na Malawi, ambapo wamesisimama kuzungumzia baadhi ya mantiki ya hali halisi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Nchi, hasa juu ya ushirikiano na Kanisa Katoliki katika muktadha wa Afya, Elimu na mafunzo ya kitaaluma.
Wakiendelea na mazungumzo hayo vile vile wamebadilishana mawazo juu ya mada zenye tabia ya kikanda na kimataifa, wakisisitizia umuhimu wa kuhamasisha mazungumzo na maridhiano kati ya watu.
Wakati wa kubadilishana zawadi za kiutamadini, Baba Mtakatifu amemzawadia picha ya yenye ishara ya mikono miwili inayoshikana ikiwa imezungukwa na nuzi za Uwanja wa Mtakatifu Petro, kukiwa na mwanamke na mtoto na Meli iliyojaa wahamiaji kwa kuandikwa: “ Tujaze mikono kwa mikono mingine; ”Ujumbe kwa ajili ya amani mwaka2024, Kitabu cha Statio Orbis cha 27 Machi 2020, kilicho tayarishwana LEV kinachohusu, Njia ya Msalaba ya wakati wa kipindi kigumu cha Uviko.
Wakati huo huo zawadi ya Rais Chakwera ni Sanamu iliyotengenezwa mahalia ambayo inaonesha ramani ya Malawi ikiwa na mji mkuu na wanyama ambao wanaishi katika Nchi hiyo.