Papa Francisko amemteuwa Katibu Mkuu Mpya wa Shirika la Kipapa la Kimisionari la Utoto Mtakatifu. Papa Francisko amemteuwa Katibu Mkuu Mpya wa Shirika la Kipapa la Kimisionari la Utoto Mtakatifu. 

Papa amemteua Sr.Inês,A.S.C.,kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Shirika la Kimisionari la Utoto Mtakatifu

Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024,BaBa Mtakatifu amemteua Sr. Inês Paulo Albino,A.S.C.,Mshauri wa Shirika la Waabuduo wa Damu Takatifu kuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Kimisionari la Kipapa la Utoto Mtakatifu.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024 amemteua Katibu Mkuu mpya wa shughuli za  Kipapa za Shirika la Kimisionari la Utoto Mtakatifu, Mhemishwa Sr. Inês Paulo Albino,A.S.C.,ambaye hadi uteuzi alikuwa ni Mshauri wa Shirika la Masisita Waabuduo  wa Damu Takatifu.

Wasifu wake

Sr. Ines Paulo Albino, alizaliwa tarehe 25 Aprili 1969 huko Bula(Guinea-Bissau) na alifunga nadhiri za daima katika Taasisi ya Waabuduo wa Damu Takatifu mnamo tarehe 4 Septemba 1997. Aliendelea na masomo na kupata leseni ya Taalimungu ya Biblia katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma. Tayari alikuwa ni mhusika wa kichungaji wa Parokia ya Mtakatifu Maria de Mattias huko Ingoré na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Kitaifa ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa huko Bissau. Alijikita kwenye nyanja za uinjilishaji, wa katekesi, ufundishaji na utume wa vijana. Mnamo 2022 amekuwa Mshauri na Mchumi wa Kanda ya Italia Shirika hilo la kitawa.

Papa amemteua Katibu Mkuu wa hirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu
24 August 2024, 12:18