Papa apokea Barua na Hati za Utambulisho wa balozi wa Slovakia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Alhamisi tarehe 22 Agosti 2024, Baba Mtakatifu Francisko amepokea Hati na barua za Utambulisho kutokakwa Bwana Juraj Priputen, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia akiwakilisha Nchi yake mjini Vatican. Bwana Juraj Priputen alizaliwa tarehe 18 Julai 1975 huko Bratislava, ameona na kuwa na familia ya watoto wawili. Elimu ya mafunzo, ni pamoja na kupata Shahada na Shahada ya Uzamili kutoka Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa huko Moscow, Kitivo cha Haki za Kimataifa (1992 – 1997) na Udaktari katika Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Comenius huko Bratislava (1999 – 2000) na ambacho ni chuo kikuu cha kisasa cha Ulaya kilichoanzishwa miaka zaidi ya 105 iliyopita.
Vile vile Balozi huyo amefunika nyadhfa mbali mbali kama vile: Afisa wa Dawati, Idara ya Haki za Kibinadamu, Idara ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, MAE (1997 - 2000), Mshauri wa Haki za Kibinadamu, Ujumbe wa Kudumu wa Jamhuri ya Slovakia katika Umoja wa Mataifa, New York (2000 - 2004), Mkurugenzi wa Ofisi ya Katibu Mkuu, MAE (2004 – 2006), Naibu Mkuu wa Balozi, Ubalozi katika Shirikisho la Urusi (2006 - 2010), Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Mkurugenzi Mkuu wa Rasilimali Watu na Naibu Katibu Mkuu, MFA (2010 - 2013), Balozi wa Kroatia (2013 - 2018), Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Kibinadamu, MAE (2018 - 2019), Mshauri wa Sera ya Kigeni kwa Rais wa Baraza la Kitaifa la Jamhuri ya Slovakia (2019 - 2024).