Tafuta

Kardinali Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji. Kardinali Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji. 

Ziara ya kitume ya Papa huko Asia na Ocean:Tagle,Makanisa madogo yanaweza kuwa shule!

Kardinali Luis Antonio Gokim Tagle,Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji amefanya mazungumzo na waandishi wa habari Gianni Valente na Fabio Beretta kuhusiana na ziara ya kitume ijayo kwanda Mataifa manne katika mabara mawili."Safari hizi ndefu ni nzito.Kwa kukumbatia hata juhudi hii ni kitendo cha unyenyekevu."

Na Gianni Valente e Fabio Beretta

Mataifa manne katika mabara mawili, kwa jumla ya karibu kilomita elfu 40 kusafiri. Ndege ya Papa itapaa kutoka uwanja wa ndege wa Fiumicino, Roma mnamo tarehe 2 Septemba 2024 na ziara ndefu zaidi na yenye mahitaji makubwa zaidi ya kitume kwa Papa Francisko atakayojikita nayo kati ya Asia na Ocean. "Lakini Askofu wa Roma haondoki katika jimbo lake kwa ajili ya kuvunja rekodi, badala yake ni tendo la unyenyekevu mbele ya Bwana anayetuita. Kitendo cha utii kwa utume.” Hayo yalisemwa na  Kardinali Luis Antonio Gokim Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, wakati safari itakayompeleka Baba Mtakatifu hadi Indonesia, Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na Singapore inapokaribia. Kwa njia hiyo  Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji- (Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya), katika mazungumzo na  Shirika la Habari za Kimisionari pia alipendekeza kwa nini safari ya Mrithi wa Petro kati ya Makanisa ya kundi ndogo ni muhimu kwa Kanisa zima la ulimwengu, na inaweza kuvutia wale wote wanaojali amani duniani. Yafuatayo ni mahojiano hayo na mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji.

Akiwa na takriban miaka 88, Papa Francisko anakaribia kufanya safari ndefu na ya kuchosha zaidi ya upapa wake. Ni nini kinachomsukuma kukumbatia “tour de force” hii?

Nakumbuka kwamba kiukweli safari hii ya Asia na Ocean ilikuwa tayari imepangwa kwa 2020. Nilikuwa nimewasili Roma tu, kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na ninakumbuka kwamba mpango huu ulikuwa tayari hupo. Kisha janga la Uviko-19 lilisimamisha kila kitu. Na nilishangaa sana kwamba Baba Mtakatifu aliurudisha mpango huo mikononi mwake mwenyewe. Ni ishara ya ukaribu wake wa kibaba kwa kile anachokiita "maisha ya pembezoni. 'existential peripezie'. Ninasemaukweli: Mimi ni mdogo kuliko Papa na ninashuhudia kuwa safari hizi ndefu ni nzito. Kwake, Yeye kukumbatia hata juhudi hii ni kitendo cha unyenyekevu. Si onesho la kuonesha kile ambacho bado ana uwezo nacho. Kama shahuda, ninasema kwamba ni tendo la unyenyekevu mbele za Bwana anayetuita. Tendo la unyenyekevu na utii kwa utume.

Wengine wanarudia: Safari hii pia inathibitisha kwamba, Papa anapendelea Mashariki na kupuuza Magharibi.

Wazo hili la kuzingatia ziara za kitume kama ishara kwamba Baba Mtakatifu “anapendelea” bara au sehemu ya ulimwengu au kudharau sehemu zingine ni tafsiri ya uwongo ya safari za upapa. Baada ya safari hii, mwishoni mwa mwezi Septemba, Papa anapanga kutembelea Luxembourg na Ubelgiji. Ametembelea nchi nyingi ikiwa ni pamoja na kanda nyingi za Ulaya. Inaonekana kwangu kwamba, kwa safari hizi, anataka kuwatia moyo Wakatoliki katika mazingira yote ambayo wanajikuta. Na pia ni muhimu kukumbuka kwamba wengi wa wanadamu wanaishi katika maeneo haya ya dunia. Theluthi mbili ya idadi ya watu duniani iko katika bara la  Asia. Wengi wa watu hawa ni maskini. Na kuna ubatizo mwingi miongoni mwa maskini. Papa Francisko anajua kwamba kuna watu wengi maskini huko, na miongoni mwa maskini kuna mvuto huu kwa mtu wa Yesu na Injili, hata katikati ya vita, mateso na migogoro.

Wengine wanasisitiza kuwa Wakristo, katika nchi nyingi atakazotembelea na Papa, ni wachache kwa idadi ikilinganishwa na idadi ya watu.

Kabla ya kufanya safari zake, Papa alipokea mialiko sio tu kutoka kwa Makanisa mahalia, bali pia kutoka kwa viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa ambao waliomba rasmi uwepo wa Askofu wa Roma katika nchi yao. Wanataka uwepo wa Papa sio tu kwa sababu za imani, lakini pia kwa sababu zinazohusu mamlaka za kiraia. Kwao Papa anabaki kuwa ishara yenye nguvu ya kuishi pamoja kwa binadamu katika roho ya udugu na kwa utunzaji wa Uumbaji.

Wewe, kama mchungaji wa Kanisa la Ufilippini na kisha Kardinali wa Baraza la Kipapa la kimisionari, ni uzoefu gani na mikutano gani umekuwa nayo na nchi na Makanisa ambayo Papa atatembelea katika siku chache zijazo?

Huko Papua New Guinea nilifanya ziara ya kitume kwenye Seminari ya ombi la Kardinali Ivan Dias, ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa  Propaganda Fide. Nilifanya safari mbili katika muda wa miezi miwili, nikizuru seminari za Papa New Guinea na Visiwa vya Solomon. Pia nimetembelea Indonesia na Singapore, lakini sijawahi kufika Timor Mashariki, ingawa nimekutana na maaskofu, mapadre, Watawa na walei kutoka nchi hiyo mara nyingi. Kwangu mimi, Asia ni “ulimwengu unaojumuisha ulimwengu tofauti”, na kama Mtu kutoka Asia naona kwamba kusafiri kwenda Asia kunafungua akili na moyo kwa upeo mkubwa wa ubinadamu, wa uzoefu wa mwanadamu. Ukristo pia umejumuishwa katika bara la Asia kwa njia ambazo zinanishangaza. Ninajifunza mengi sana kuhusu hekima na ubunifu wa Roho Mtakatifu. Mimi hushangazwa kila mara na njia ambazo Injili inaoneshwa na kufanyika mwili katikati ya mazingira tofauti ya kibinadamu. Matumaini yangu ni kwamba Papa, na pia sisi sote katika msafara wa upapa na hata waandishi wa habari tunaweza kuwa na uzoefu huu mpya, uzoefu wa ubunifu wa Roho Mtakatifu.

Je, ni zawadi zipi na sehemu za faraja ambazo jumuiya za kikanisa zilizotembelewa na Papa katika safari yake, inayofuata zinaweza kutoa kwa Kanisa zima?

Katika nchi hizo, jumuiya za Kikristo karibu kila mahali ni wachache, yaani ni kundi dogo. Katika maeneo kama Ulaya, Kanisa bado linafurahia hadhi fulani ya kiutamaduni, kijamii na hata ya kiraia. Lakini pia katika nchi nyingi za Magharibi tunarudi kwenye uzoefu huu wa Kanisa kama kundi dogo. Na inaweza kuwa vizuri kuangalia Makanisa ya nchi nyingi za Mashariki ili kuona jinsi  gani mtu anavyofanya wakati yuko katika hali, katika hali ya udogo. Uzoefu wa Mitume wa kwanza, wa wanafunzi wa Yesu, unarudiwa mara nyingi katika nchi hizi. Padre wa parokia ya Nepal aliniambia kwamba eneo la parokia yake ni kubwa kama theluthi moja ya Italia: Yeye ana waamini 5 tu waliotawanyika katika eneo hilo kubwa. Tuko  hili katika 2024, lakini muktadha na uzoefu unaonekana kama ule wa Matendo ya Mitume. Na Makanisa madogo yanayoishi Mashariki yanaweza kutufundisha. Indonesia ni taifa la visiwa, na kuna hali nyingi tofauti katika ngazi ya kiutamaduni, lugha, kiuchumi na kijamii. Pia ni nchi duniani yenye idadi kubwa ya wakazi Waislamu. Na zawadi kubwa ya Roho Mtakatifu kwa jumuiya ya Kikatoliki ya Indonesia ni ile ya kuishi pamoja ambayo haikatai utofauti. Ninatumaini kuwa ziara ya Papa italeta msukumo mpya katika udugu kati ya waamini wa dini mbalimbali.

Je, umeweza kupata uzoefu wa ishara madhubuti za kuishi pamoja kidugu wakati wa matembezi yako?

Walinisimulia kwamba ardhi ambayo Chuo Kikuu cha Kikatoliki kimejengwa ilikuwa zawadi kutoka kwa Rais wa kwanza. Ujumbe mzito, wa kuonesha kwamba miongoni mwa watu wa Indonesia kila mtu anakubalika kama kaka na dada. Pia ninakumbuka niliposhiriki Siku ya Vijana huko Asia. Kwa kuzingatia idadi ndogo ya Wakristo, miongoni mwa watu waliojitolea kushiriki katika tukio  hilo pia kulikuwa na vijana wengi wa Kiislamu. Baraza la Maaskofu lilinipatia wasaidizi wawili, wote Waislamu, ambao niliwaona wakitekeleza majukumu yao kwa heshima kubwa kwa Kanisa.

Kituo cha pili: Papua New Guinea.

Kanisa la Papua New Guinea ni Kanisa changa, lakini tayari limetoa Kanisa la ulimwengu wote mfiadini Peter To Rot, ambaye pia alikuwa katekista. Papua New Guinea pia ni nchi yenye tamaduni nyingi, yenye makabila mbalimbali ambayo mara kwa mara yanagombana. Lakini ni nchi ambayo utofauti unaweza kuwa mali. Ikiwa tutasimamisha mawazo yetu ya awali, hata katika tamaduni za kikabila tunaweza kupata maadili ya kibinadamu karibu na maadili ya Kikristo. Na kisha huko Papua New Guinea kuna mahali ambapo asili haijachafuliwa. Miaka miwili iliyopita nilikuwepo kwa ajili ya kuweka wakfu kwa Kanisa Kuu jipya. Nilimwomba Askofu maji, akaniambia: “Tunaweza kunywa maji ya mto, ni ya kunywa.” Shukrani kwa hekima yao ya kikabila wameweza kudumisha maelewano na asili na wanaweza kunywa moja kwa moja kutoka katika mto. Kitu ambacho sisi katika nchi zinazoitwa zilizoendelea hatuna tena uwezo huo.

Kituo cha tatu: Timor Mashariki.

Ni muhimu kwamba Papa anagusa Indonesia na kisha Timor Leste. Nchi mbili ambazo zina historia ya mapambano na sasa zina amani. Amani dhaifu, lakini shukrani kwa wote wawili inaonekana kudumu. Hapo uhusiano kati ya Kanisa mahalia na serikali ni mzuri sana. Serikali mahalia pia inasaidia huduma za elimu zinazohusiana na Kanisa. Na inaonekana kwangu kwamba Kanisa lilikuwa mojawapo ya vituo vya kumbukumbu kwa idadi ya watu wakati wa vita vya uhuru. Watu wa Timor Leste wanasema imani yao katika Kristo iliwategemeza wakati wa miaka ya kupigania uhuru. Ni miongoni mwa nchi tajiri zaidi duniani, na inashangaza kuona watu ambao wamefikia kiwango hicho cha taaluma na hali ya juu ya teknolojia kwa miaka michache tu na rasilimali chache, shukrani pia kwa nidhamu. Serikali ya Singapore inahakikisha uhuru kwa jumuiya zote za waamini na kuwalinda dhidi ya mashambulizi na vitendo vya kukosa heshima. Makosa dhidi ya dini yanaadhibiwa vikali. Watu wanaishi salama, na watalii pia wanaishi salama. Lakini usawa unahitajika. Historia inatufundisha kuwa makini ili utumizi wa sheria usiishie kupingana na maadili ambayo sheria zinapaswa kulinda.

Hata katika nchi hizo - hasa katika Papua New Guinea - kazi ya kitume inaakisiwa na historia za wafiadini wamisionari. Lakini wakati mwingine kazi ya wamisionari inaendelea kuoneshwa tu kama kielelezo cha ukoloni wa kiutamaduni na kisiasa.

Sasa kuna mwelekeo huu na kishawishi hiki cha kusoma historia, hasa historia ya utume, na mifumo ya kiutamaduni ya leo hii na kulazimisha maono yetu kwa wamisionari walioishi karne nyingi zilizopita. Badala yake unahitaji kusoma historia kwa uangalifu. Wamisionari ni zawadi kwa Kanisa. Wanamtii Kristo mwenyewe aliyewaambia wafuasi wake waende mpaka miisho ya dunia kutangaza Injili, akiahidi kwamba atakuwa pamoja nao daima. Wakati fulani baadhi ya viongozi wa mataifa waliwapeleka wamisionari sehemu mbalimbali wakati wa mchakato wa ukoloni. Lakini wamisionari hao walihamia kueneza Injili, si kudanganywa na kutumiwa na wakoloni. Mapadre wengi, wamisionari na watawa walitenda kinyume na mikakati ya serikali yao na wakauawa kishahidi.

Je, ni fumbo gani la ajabu linalounganisha daima kifo cha kishahidi na utume?

Miaka miwili iliyopita utafiti kuhusu uhuru wa kidini ulichapishwa. Kulikuwa na ukweli mmoja wazi: katika nchi hizo ambapo kulikuwa na vitisho na mateso, idadi ya ubatizo ilikuwa ikiongezeka, ambapo kuna uwezekano wa kweli wa kifo cha kishahidi, imani kuenea. Na hata wale ambao sio waamini hujiuliza: nguvu zote hizi zinatoka wapi, ambazo huwaongoza kutoa maisha yao? Ni Injili inayotenda kazi. Na lengo letu pia kwa Baraza la Uinjilishaji, ni kusaidia Makanisa mahalia, si kulazimisha mawazo au utamaduni tofauti na wao.

Mahojiano ya Kardinali Tagle katika matazamio ya Ziara ya Papa Barani Asia
27 August 2024, 14:45