Papa wakati wa kuzindua michoro mkubwa huko Lisbon wakati wa WYD wa Harakati ya Schola Occurrentes. Papa wakati wa kuzindua michoro mkubwa huko Lisbon wakati wa WYD wa Harakati ya Schola Occurrentes.  (ANSA)

Scholas yazindua mpango wake wa kwanza wa elimu katika Asia ya Kusini-mashariki

Scholas Occurrentes,kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu,Utamaduni,Utafiti na Teknolojia ya Jamhuri ya Indonesia na kwa msaada wa Harakati ya Global 5P ilitangaza uzinduzi wa programu ya Uraia wa Scholas nchini Indonesia ambayo inawaleta pamoja wajumbe 200 wa wanafunzi kutoka taasisi mbalimbali za elimuna kutoka visiwa mbalimbali vya nchi.

Vatican News

Scholas Occurrentes, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Utamaduni, Utafiti na Teknolojia ya Jamhuri ya Indonesia na kwa usaidizi wa  Harakati ya Global 5P walitangaza kuzinduliwa kwa programu ya Uraia wa Scholas nchini Indonesia. Programu hii bunifu ya elimu inaleta pamoja wajumbe 200 wa wanafunzi kutoka taasisi mbalimbali za elimu na visiwa nchini kote, ikiashiria hatua muhimu kama programu ya kwanza ya Scholas Kusini-mashariki mwa Asia. Katika siku kumi zijazo, wajumbe 200 wa wanafunzi kutoka taasisi mbalimbali za elimu na kutoka makabila na dini mbalimbali wataishi uzoefu wa Scholas ili kusikiliza wasiwasi wao, maumivu yao na ndoto zao, kushiriki na wengine na kutafuta ufumbuzi pamoja.

Kutoa maana kwa vijana

Kusudi ni kutoa mafunzo kwa kikundi cha wanafunzi wa vyuo vikuu na walimu vijana ili waweze kutekeleza mbinu bunifu ya Scholas katika jamii zao. Mbinu hii inalenga kutoa maana kwa vijana na kukabiliana na mahitaji ya sasa ya jamii ya Indonesia. Baba Mtakatifu Francisko mwenyewe atakutana na wanafunzi ambao wameishi katika uzoefu wa Scholas nchini ili kuwasikiliza na kusherehekea nao (polyhedron-poligoni)ya elimu ambayo itawakilisha umoja katika utofauti na Utamaduni wa Kukutana. Washirika wa kwanza Mpango wa Scholas Occurrentes katika nchi ya Kusini-Mashariki mwa Asia unafanywa kwa ushirikiano wa Wizara ya Elimu, Utamaduni, Utafiti na Teknolojia ya Jamhuri ya Indonesia na usaidizi wa ‘Harakati ya  5P Global.

Harakati za Global 5P

Harakati ya Global 5P imejitolea kukuza maadili ya kidemokrasia, ushirikiano wa kimataifa na uwezo wa kibinadamu, ikizingatia kanuni tano za kimsingi: Amani, Ufanisi, Watu, Sayari na Ushirikiano. Dhamira yake ni kuunda ulimwengu ambapo haki za binadamu, haki ya kijamii na afya ya mazingira hustawi, kuelewa kwamba amani ya kweli inategemea ustawi na ushirikiano wa pamoja. Harakati ya Global 5P inashughulikia changamoto za kimataifa kupitia mshikamano, kufanya kazi ili kufanya amani, ustawi na uendelevu kuwa ukweli wa pamoja kwa siku zijazo.

Kushiriki katika Mkutano wa G20 mnamo 2022

Mnamo 2022, Scholas Ocurrentes ilialikwa kushiriki katika Mkutano wa G20 huko Bali, Indonesia. Wakati wa tukio hili la kimataifa, wawakilishi wa Scholas walikutana na viongozi wa dunia kutoka nyanja za kisiasa, kielimu na kijamii. Lengo lilikuwa kuwasilisha uzoefu wa kimataifa wa Scholas kama kielelezo cha ubunifu cha elimu katika kanda. Kama sehemu ya G20, Scholas pia alialikwa kushiriki katika Kongamano la Tri Hita Karana, ambapo kulikuwa na majadiliano na Waziri wa Elimu wa Indonesia kuhusu  Scholas kama anapaswa kufanya shughuli zake nchini Indonesia.

Kuelewa mazingira ya ndani na kubuni mikakati ya utekelezaji

Zaidi ya hayo, majadiliano yalifanyika na mratibu wa Jukwaa ili kuimarisha uhusiano na wadau mbalimbali nchini Indonesia na Asia kwa ujumla. Sambamba na utume wa Scholas, uliopendekezwa na Papa Francisko, wa kukuza utamaduni wa kukutana na amani, ziara ilifanywa katika kijiji cha Genggelang, katika kisiwa cha Lombok. Huko, wawakilishi wa Scholas walishiriki nyakati na vijana wa jumuiya na kupanda mzeituni kama ishara ya ahadi hii. Vijana hao wa Indonesia walifunzwa na timu ya Kimataifa ya Scholas nchini Hispania. Scholas walituma timu iliyojitolea nchini Indonesia ili kuelewa vyema mazingira ya ndani na kubuni mkakati wa utekelezaji unaofaa. Kwa kufanya kazi kwa karibu na mamlaka za mitaa, shule na vyuo vikuu, tumeunda mpango kazi wa kina unaolenga kukuza uraia wa kimataifa miongoni mwa vijana wa Indonesia.

Mafunzo ya vijana wa Indonesia kwa mbinu ya Scholas

Scholas amechagua Vijana wa Indonesia kupokea mafunzo ya kina katika mbinu ya Scholas katika makao makuu yetu huko Granada, Hispania. Kwa njia hii wamejitayarisha kuleta mbinu hii kwa jamii zao. Hivyo, baada ya kufanya tathmini ifaayo, iliamuliwa kwa pande zote mbili kufungua tawi la kwanza la Scholas katika kanda, na timu ya kudumu ya kuendeleza michezo, sanaa na programu za teknolojia. Itazinduliwa na Papa Francisko mnamo tarehe 4 Septemba 20244, wakati wa ziara yake ya kitume nchini humo.

Vijana wa Indonesia katika Scholas Occurrentes
08 August 2024, 14:54