Papa anaendelea na upendo kwa Ukraine:vifurushi vya chakula na dawa katika maeneo ya vita
Vatican News
Hatua ya Papa ya upendo kuelekea Ukraine, ambayo imekuwa ikifafanuliwa kama nchi ya ‘kuteswa’, inaendelea pia katika msimu wa joto. Kama ilivyokuwa katika miezi iliyopita, malori yenye chakula, nguo na madawa kwa ajili ya watu wanaoteseka katika nchi ya Ulaya Mashariki yameondoka Jumatano tarehe 7 Agosti 2024 kutokea katika Basilika ya Kiukreni ya Hagia Sophia huko Roma. Hasa, wakati huu masanduku yenye tuna na chakula cha muda mrefu.
Ishara ya kuonesha ukaribu wa kibaba
Kwa mara nyingine tena, Ofisi ya Baraza la Kipapa la Upendo linaloongozwa na Kardinali Konrad Krajewski, ndiyo lenye dhamana ya kutuma na kusambaza zawadi hizi kutoka kwa Baba Mtakatifu kwenda Ukraine. Ishara mpya ya kusisitiza ukaribu wake na nchi, ambayo hata leo, mwishoni mwa hadhara kuu, aliomba sala na ukaribu kutoka kwa waamini wote.