‘Utusamehe makosa yetu:utujalie amani’ndiyo mada ya Siku ya amani 2025
Vatican News
Alhamisi tarehe 8 Agosti 2024, Baraza la Kipapa la Huma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu limechapisha Kauli mbiu iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko ambayo itakaoongoza Ujumbe wa LVIII wa Siku ya Amani Duniani itakayoadhimishwa tarehe 1 Januari 2025 isemayo “Utusamehe makosa yetu: utujalie amani.” Kauli mbiu hiyo inaonesha asili ya kibiblia na ya kikanisa katika mwaka wa Jubilei na kuhuisha kwa msukumo kwa namna ya pekee katika Nyaraka mbili za Kitume za baba Mtakatifu: ‘Laudato Si’ na ‘Fratelli tutti’, hasa kwa kuzungukia muktadha wa Tumaini na wa Msamaha, Moyo wa Jubilei ya 2025. Huu ni mwito wa uongofu unaolekeza si kuhukumu, lakini kwa kufanya maridhiano na kufanya amani.
Mtazamo halisi wa dhambi za kijamii zinazoumiza ubinadamu leo hii
Kuanzia na mtazamo wa hali halisi ya migogoro na dhambi za kijamii zinazoumiza ubinadamu leo hii, kwa kutazama katika matumaini ambayo yanakita mzizi katika tamaduni ya kijubile, ya kuondolewa dhambi/ kufuta madeni na kutafakari Mababa wa Kanisa, inawezekana kwa hakika kuingia ndani ya mwelekeo wa dhati ambao ufikie katika mabadiliko ya lazima katika mantiki ya kiroho, kimaadili, kijamii, kiuchumi, kiekolojia na kiutamaduni. Ni kupitia uongofu wa kweli, kibinafsi, kijumuiya na kimataifa tu, inawezekana kwa hakika kuchanua amani ya kweli ambayo si tu katika kuonesha hitimisho la migogoro, lakini katika ukweli mpya, ambamo majeraha yanaweza kutibiwa na kila mtu anaweza kutambuliwa hadhi yake.