Askofu Victor Hugo Castillo Matarrita wa Jimbo Katoliki la Kaga-Bandoro: Uteuzi 5 Septemba 2024. Askofu Victor Hugo Castillo Matarrita wa Jimbo Katoliki la Kaga-Bandoro: Uteuzi 5 Septemba 2024.  (ANSA)

Askofu Victor Hugo Castillo Matarrita Jimbo Katoliki la Kaga-Bandoro

Askofu mteule Victor Hugo Castillo Matarrita, M.C.C.J., alizaliwa tarehe 19 Machi 1963 huko Mansiòn, Jimbo Katoliki la Tiaràn, Costa Rica. Baada ya malezi na majiundo yake ya maisha ya kitawa, tarehe 27 Septemba 1991 akaweka nadhiri zake za daima, huko Paris, nchini Ufaransa. Tarehe 8 Agosti 1992 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre nchini Costa Rica. Amewahi kuwa Mwakilishi wa mkuu wa Kanda na Mkuu wa Kanda ya Wamisionari wa Komboni Kanda ya Afrika ya Kati.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 5 Septemba 2024 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Victor Hugo Castillo Matarrita, M.C.C.J., wa Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Kaga-Bandoro lililoko katika Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule Victor Hugo Castillo Matarrita, M.C.C.J., alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kanda ya Afrika ya Kati. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Victor Hugo Castillo Matarrita, M.C.C.J., alizaliwa tarehe 19 Machi 1963 huko Mansiòn, Jimbo Katoliki la Tiaràn, Costa Rica. Baada ya malezi na majiundo yake ya maisha ya kitawa, tarehe 27 Septemba 1991 akaweka nadhiri zake za daima, huko Paris, nchini Ufaransa. Tarehe 8 Agosti 1992 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre nchini Costa Rica.

Askofu mteule Victor Hugo Castillo Matarrita
Askofu mteule Victor Hugo Castillo Matarrita

Tangu wakati huo kama Padre ameweza kufanya utume wake Parokiani Grimari kuanzia mwaka 1993 hadi 1998. Tangu mwaka 1998 hadi mwaka 2001 akateuliwa kuwa ni mlezi na mkuu wa Shirika mjini Bangui. Kati ya Mwaka 2002 hadi mwaka 2007 aliteuliwa kuwa ni Mwakilishi wa kanda na Rais wa Shirikisho la Wakuu wa Mashirika nchini Afrika ya Kati. Kati ya Mwaka 2008 hadi mwaka 2009 aliteuliwa kuwa ni mlezi wa wapostulanti huko “San Josè” na Mshauri wa Shirika huko Amerika ya Kati. Kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2020 akachaguliwa kuwa Mkuu wa Kanda ya Shirika Amerika ya Kati. Kati ya Mwaka 2020 hadi mwaka 2022 akateuliwa kuwa ni Mratibu wa wanafunzi wa Shirika la Comboni waliokuwa wanasoma mjini Roma. Kuanzia tarehe Mosi Januari 2023 hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kanda ya Afrika ya Kati.

Uteuzi Septemba 2024
06 September 2024, 14:01