Baada ya kutua Roma Papa amesali mbele ya Salus Popouli Romani
Vatican News.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya Habari Vatican, Dominika tarehe 29 Septemba 2024, kuhusu safari ya kurudia kwa Baba Mtakatifu Francisko kutoka katika Ziara yake ya 46 ya Kitume iliyoanza tangu tarehe 26 Septemba, amebainisha kwamba: “Mara baada ya kurudi kutoka Ziara ya Kitume nchini Luxembourg na Ubelgiji, Papa Francisko alikwenda katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu, mahali ambapo amekaa kitambo kwa sala mbele ya Picha ya Bikira Salus Populi Romani. Na baada ya kutembea amerudi mjini Vatican.
Kwa Mfalme wa Ubelgiji
Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika Ndege ya kurudi mjini Vatican alituma hata Telegram kwa Marais wa nchi ya Ubelgiji, Ujerumani, Austria na Italia. Katika telegram kwa Mfalme Phillip wa Ubelgiji Papa amebainisha kuwa “Nikiwa ninarudi Roma baada ya kuhitimisha Ziara yangu ya Kitume katika Nchi yako, ninaeleza shukrani kwako wewe na wajumbe wote wa familia ya kifalme na Watu wote wa Ubelgiji kwa ishara nyingi za makaribisho na udugu mpana kwangu katika siku hizi za ziara yangu. Ninapyaisha uhakika wa sala zangu kwa ajili ya ustawi wa taifa na kwa hiari ninawaombea baraka nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.”
Kwa Rais wa Ujerumani
Na kwa upande wa Nchi ya Ujerumani, Baba Mtakatifu amemtumia, Bwana Franck Walter Steinmeir, Rais wa Shirikisho la Ujermani–Berlin kwamba: “Kwa mara nyingine tena ninakutumia salamu njema kwa raia wako ninapopita juu ya Ujerumani katika safari yangu ya kurudi kutoka Ubalgiji hadi Roma. Ninaomba Taifa libarikiwe sana kwa kipaji cha karama za Mwenyezi Mungu.”
Kwa Rais wa Austria
Papa vivile kwa mkuu wa Austria, amebanisha kuwa: “Mheshimiwa Alexander Van Der Bellen, Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Austria–Vienna, ninapopitia juu ya Nchi yako nikirudi Roma kufuatia na ziara yangu yakitume kutoka Ubelgiji ninapyaisha matashi mema katika maombi kwako na kwa watu wa Austria na juu yako na wote ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu umoja na furaha.”
Kwa Rais wa Italia
Hatimaye Baba Mtakatifu alituma telegram yake kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella ambapo ameandika kuwa: “Nikiwa ninarudi kutoka ziara yangu ya kitume huko Luxembourg na Ubelgiji, mahali ambapo nilipata fursa ya kukutana na tamaduni za kale za kiroho na zinazotamani kuendelea katika huduma ya Udugu, kwa kufungua njia ya matumaini, Ninakutakia kwa moyo wote mheshimiwa Rais wa Taifa, pendwa la Italia shauku ya upendo na utulivu huku nikikuhakikishia sala yangu daima.”