Kutoka katika andaki la vita hadi lile la udugu
ANDREA TORNIELLI
Kuna andaki za vita, na hofu ile inayosaidia kuficha wanajeshi, wanamgambo na waliotekwa nyara. Na kuna andaki za kuunganisha katika urafiki wa watu wa imani tofauti. Huko Jakarta Msikiti wa Istiqlal, ulio mkubwa zaidi kusini mashariki mwa Asia na Kanisa Kuu Katoliki la Mama Yetu Mpalizwa, yanatazamana, na yako karibu lakini yanatengenishwa na barabara yenye njia tatu. Daraja moja la zamani, lilikarabatiwa, likapambwa kwa kazi ya kisanii na kubadilishwa kuwa “andaki la udugu” ili kuunganisha eneo la sala ya Waislamu na ile ya wakristo wanaoadhimisha Ekaristi. Katika wakati ambao dunia inawaka moto mahali ambapo kuna mapambano ya vita, vinavyosimuliwa na vyombo vya habari na vile vilivyosahaulika, mahali ambao vurugu na chuki utafikiri zinashinda, tunahitaji kupata njia za urafiki, za kuwa na ahadi ya mazungumzo na juu ya amani kwa sasabu “sisi sote ni ndugu”
Ndicho anachotushuhudia Mfuasi wa Petro mjenzi wa madaraja. Papa Francisko leo anasafiri na Ndege inayoelekea Asia na Oceanea, katika safari ndefu zaidi ya upapa wake kuanzia Indonesia, nchi kubwa ya kiislamu katika sayari, hadi Papua New Guinea na baadaye kurudi kuelekea Timor ya Mashariki na hatimaye Singapore. Hija hii, ni kuweza kuwa karibu na wakristo pale ambao ni “zizi dogo” kama huko Indonesia; au mahali ambapo wanawakilishwa karibu jumla ya watu kama vile Timor ya Mashariki. Safari kwa ajili ya kukutana wote na kuthibitisha tena kuwa hatuhukumiwa na kuta, vizuizi, chuki, na vurugu, kwa sababu wanawake na wanaume wenye imani tofauti, kabila na tamaduni tofauti wanaweza kuishi pamoja, kuheshimiana na kushirikiana. Hata kama ilikuwa imepangwa miaka 4 iliyopita na baadaye kuhairishwa kwa sababu ya janga la Uviko, Ziara ya Asia na Oceania inachukua maana ya kinabii leo hii.
Askofu wa Roma kwa mtindo wa Mtakatifu wa Assisi ambaye anachukua jina lake, anajiwakilisha bila silaha, bila nia ya ushindi au itikadi, bali mwenye shauku tu ya kushuhudia uzuri wa Injili ikimsukuma hadi Vanimo, mji wenye roho za watu elfu zilizoko kwenye uso wa Bahari ya Pasifiki. Ndicho kilikuwa kimemvuta mtangulizi wake, Papa Paulo VI na ambaye tarehe 29 Novemba 1970 akiwa katika Ndege ndogo alikuwa amefikia Apia katika kisiwa cha Samoa Huru ili kusherehekea misa katika altare ndogo, inayotetemeka huko Leulumoega kwa ajili watu mia wanaoishi kisiwani huko. Na ndicho hicho kilicho msukuma Papa Yohane Paulo II kutambelea mara nyingi maeneo ya ulimwenguni kama vile mnamo tarehe 20 Novemba 1986 huko Singapore kwa mapendekezo ya kutokuwepo kweli kwa mafundisho ya Yesu: “Upendo hujibu kwa ukarimu mahitaji ya maskini, na huoneshwa kwa huruma kwa wale wanaoteseka.” Upendo huko tayari kutoa ukarimu, na ni mwaminifu katika nyakati ngumu; Na daima huko tayari kusamehe, kutumaini na kubadilishwa kashfa kuwa baraka. Upendo hautakuwa na mwisho(1Kor 13,8). Amri ya upendo ni kiini cha Injili.”