2024.09.29 Wakati wa misa Takatifu katika Uwanja wa Mfalma Baudouin. 2024.09.29 Wakati wa misa Takatifu katika Uwanja wa Mfalma Baudouin.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto) Tahariri

Nyanyaso na aibu

Kwa kukumbuka maneno ya Francisko huko Ubelgiji

Andrea Tornielli

Katika safari zake, Papa Francisko anajiruhusu kupingwa na kuumizwa na hali halisi anayokutana nayo: si kila kitu kinaweza kutayarishwa mapema. Hii pia ilitokea katika safari ya Luxembourg na Ubelgiji iliyomalizika Dominika tarehe  29 Septemba 2024. Mbele ya mfalme na Waziri Mkuu wa Ubelgiji ambaye kwa sauti tofauti aliibua janga la nyanyasoz  watoto ambalo ilikuwa na ulali na uzito wa kijiwe katika maisha ya Kanisa la nchi hiyo na madaraja yake, Askofu wa Roma alisema wazi kwamba hata kisa kimoja tu cha watoto walionyanyaswa na viongozi wa dini ni wengi mno. Akiwa  mbali na maandishi yaliyotayarishwa, alitaja “watakatifu wasio na hatia,”waathiriwa wa Mfalme Herode, kusema kwamba hii bado inatokea leo hii. Haikuwa mara ya kwanza kwa Papa kufanya ulinganisho huu kwani, mnamo Februari 2019, akihitimisha mkutano wa kilele juu ya  unyanyasaji alioitisha jijini Vatican  alitoa mfano wa Herode na mauaji yake ya watoto, na kuongeza kuwa “Shetani ndiye anayehusika na unyanyasaji wa watoto.”

Katika mahubiri ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa katika uwanja wa Mfalme Baudouin, Papa Francisko alitaka kuongeza aya zinazoeleweka na kali na alifanya hivyo baada ya kuguswa sana na mkutano na baadhi ya wahanga wa unyanyasaji uliofanyika siku mbili zilizopita, ambapo yalikuwa mazungumzo makubwa na ya kusisimua ambayo yalidumu zaidi ya saa mbili katika Ubalozi wa Vatican huko Bruxessels. Papa alirudi “kwa akili na moyo wake” katika historia zao na mateso yao, na kurudia kwamba katika Kanisa hakuna mahali pa unyanyasaji na kuficha unyanyasaji. Alisema kuwa uovu “haufichiki” lakini lazima ufichuliwe kwa ujasiri kwa kumpeleka mnyanyasaji mahakamani, yeyote yule “mlei, kuhani au askofu.” Kuna kipengele kingine muhimu cha kuzingatia katika maneno ya Papa Francis. Katika Jengo la kifalme la Ubelgiji na katika mazungumzo ya kiutamaduni na waandishi wa habari kwenye ndege hiyo, Papa alitaja takwimu zinazoonesha kuwa unyanyasaji mwingi hutokea katika familia, shuleni, katika ulimwengu wa michezo. Tena, hii haikuwa mara yake ya kwanza kufanya hivyo. Lakini safari hii kwa uwazi usio kifani alitaka kuondoa kila aina ya upendeleo kwa nia ya matumizi ya idadi hizo na wale ambao wangependa kujitetea kwa kusisitiza majukumu ya wengine na kupunguza.


Ni kweli kwamba Kanisa, katika robo ya karne iliyopita, limechukua njia ambayo imesababisha sheria kali za dharura dhidi ya jambo hilo. Ni kweli kwamba wengine hawajachukua hatua sawa. Walakini, ni kweli vile vile kwamba unyanyasaji katika nyanja ya kikanisa ni kitu cha kutisha, ambacho huanza kila wakati na matumizi mabaya ya madaraka na kudanganya dhamiri ya wasio na ulinzi: familia zilizowakabidhi watoto wao katika Kanisa ili waelimishwe katika imani, zikiwaamini kuwa wako salama, ziliwaona wakirudi wakiwa wamejeruhiwa na  mauti mwilini na rohoni. Kwa sababu hiyo hakuwezi kuwa na matumizi yoyote muhimu ya takwimu, kana kwamba kupunguza kitu ambacho hakiwezi na hakipaswi kupunguzwa kwa njia yoyote, lakini lazima ipigwe vita na kutokomezwa kwa azimio lolote linalowezekana. Kwa sababu ni uhalifu ambao “unaua roho”, kama Monsinyo Charles Scicluna alivyosema. Kwa sababu hiyo, Mrithi wa Petro, ambaye baada ya watangulizi wake wawili ametangaza sheria mpya kali sana kukomesha jambo hilo, alisema hata kesi moja ya unyanyasaji wa watoto katika muktadha wa kikanisa itakuwa nyingi sana.

Na alionesha kwa Kanisa kwa ujumla mtazamo unaofaa zaidi ni ule wa aibu, unyonge na ombi la msamaha. Ni mtazamo ule ule wa toba ambao Papa Benedikto XVI pia alipendekeza - hakuelewa - aliposema kwamba adui mkuu wa Kanisa sio nje bali dhambi ndani yake. Kufedheheshwa na ombi la msamaha ni mitazamo ya Kikristo sana: yanatukumbusha kwamba jumuiya ya kikanisa inaundwa na wadhambi waliosamehewa na kwamba dhuluma zilizotokea ndani yake ni jeraha linalotuhusu sisi sote.

30 September 2024, 16:30