Tafuta

Papa Francisko akisalimiana na Paolo Garonna wakati wa Mkutano wa Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontifice mapema Juni 22,2024. Papa Francisko akisalimiana na Paolo Garonna wakati wa Mkutano wa Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontifice mapema Juni 22,2024.  (Vatican Media)

Paolo Garonna ni rais mpya wa Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontefice

Profesa Garonna ni Mkufunzi wa Chuo Kikuu Luiss na tangu 2008 amekuwa mjumbe wa Kamati ya Kisayansi wa Mfuko huo wa kipapa na ambaye anachukua nafasi ya Profesa Anna Maria Tarantola aliyewahi kuwa Makamu mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Italia na Rais wa Shirika la Matangazo na Televisheni Italia(RAI).

Vatican News

Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus pro Pontifice, unaye Rais mpya, Profesa Paolo Garonna ambaye anachukua nafasi ya Profesa Anna Maria Tarantola aliyewahi kuwa Makamu mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Italia na Rais wa Shirika la Matangazo na Televisheni Italia (RAI) na amekuwa mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi tangu Novemba 2015 na rais wa Mfuko huo wa kipapa tangu Machi 2019.

Uteuzi wa Ptofesa Garonna

Baada ya kujua nia ya Profesa Tarantola ya kutopyaisha hatua nyingine kwa sababu binafsi, mamlaka husika ilichagua Rais mpya  Profesa Paolo Garonna  ambaye tangu  2008 amekuwa mjumbe wa Kamati ya Kisayansi ya Mfuko huo huo. Paolo Garonna ni Profesa wa Siasa ya uchumi katika Chuo Kikuu cha LUISS Guido Carli, Roma. Ana Degrii katika Chuo Kikuu cha Sapienza Roma, na mafunzo zaidi na utafiti huko Marekani katika Chuo Kikuu cha Denver, katika chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.   

Katika ya nyadhifa nyingine ni pamoja na kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi barani Ulaya katika Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi Mkuu wa ISTAT, Mchumi Mkuu wa Confindustria na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Benki, Bima na Fedha. Yeye ndiye mwandishi wa mafunzo na machapisho kuhusu Mafundisho Jamii ya Kanisa, uchumi na fedha.

Prof Garonna ni Rais Mpya wa Mfuko wa Centesimu Annus pro Pontefice
02 September 2024, 12:09