Papa apokea hati na barua za utambusho kutoka kwa Balozi wa Israeli
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 16 Septemba 2024 amepokea hati na barua za utambusho kutoka kwa Balozi Mpya wa Israel, kuwakilisha nchi yake mjini Vatican ziliwakilishwa na Bwana Yaron Sidema. Alizaliwa huko Israeli tarehe 30 Agosti 1967 ameo na ana watoto wawili.
Ameshika nyadhifa mbalimbali kama vile: Balozi wa Nigeria (1996 - 1999) - Balozi wa Masuala ya Umma, Ubalozi Mkuu huko New York (1999 - 2001), Ofisi ya Masuala ya Kiyahudi na Kidini Ulimwenguni, MFA (2001 - 2007), Mkuu wa Idara ya Masuala ya Bunge, Kitengo cha Amerika Kaskazini, MFA (2007 - 2011), Chuo cha Ulinzi cha Israeli (2011 - 2012), Balozi Mkuu, Ubalozi Mkuu katika Mkoa wa Atlantiki ya Kati (2012 - 2016), Mkuu wa Ofisi, Idara ya Masuala ya Bunge, Kitengo cha Amerika Kaskazini, MFA (2016 - 2021), Mkuu wa Ofisi, Ofisi ya Amerika Kaskazini, MFA (2021 - 2024)