Bango la kukaribisha Papa nchini Indonesia. Bango la kukaribisha Papa nchini Indonesia.  (AFP or licensors)

Parolin:Papa atapeleka huko Asia na Oceania ukaribu na amani

Indonesia,Papua New Guinea,Timor ya Mashariki na Singapore wanajiandaa kumpokea Mfuasi wa Petro.Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican,katika kesha la safari ndefu zaidi ya upapa,anasistiza subira na shauku ya kukutana na Papa.Kardinali hatasafiri kwa ndege ya kipapa kwa sababu tarehe 3 septemba kutakuwa na mazishi ya mama yake aliyefariki tarehe 31 Agosti.

Massimiliano Menichetti

Nchi Nne zinamsubiri Papa kuanzia tarehe 2 hadi 13 Septemba 2024 ambaye atakuwa huko Asia na Oceania, ili kupeleka mwana wa Kristo. Atakuwa shuhuda wa mazungumzo ili kujenga udugu wa kweli na mshikamano. Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, katika mkesha wa safari ya  45 ya Ziara ya Kitume, amefafanua kwa Vyombo vya habari kiini cha ukaribu wa Upapa wa Papa Francisko na kusisitiza kuwa, amani katika ulimwengu uliojeruhiwa na vita na vurugu unajengwa katika kukutana, kuingia katika uhusiano wa kweli na kuvunja ubinafsi. Kardinali hatasafiri leo na ndege ya Kipapa kwa sababu Jumanne tarehe 3 Septemba 2024, itafanyika misa ya mazishi ya Mama yake Ada, huko Schiavon, Wilaya ya Piacenza, aliyefariki tarehe 31 Agosti akiwa na umri wa miaka 96. Mahojiano hayo yalifanyika tarehe 27 Agosti 2024.

Mwashamu, Papa anajiandaa kusafiri safari ndefu zaidi ya upapa: atatembelea Indonesia, Papua New Guinea, Timor ya Mashariki na Singapore. Ni matumaini gani ya Papa Francisko?

Tumaini la ambalo Papa Francisko anapeleka katika moyo ni lile la kukutana: kwanza kibinafsi na watu wa Nchi ambazo atatembelea. Kwa maneno mengine ni kujikita mara nyingine katika mada ya ukaribu, wenye tabia ya upapa wake, ukaribu wa kubeba matatizo, mateso na matarajio ya watu, ukaribu wa kupeleka kwa wote furaha, faraja na tumaini la Injili. Kwa kuchukua maneno ya Mtakatifu Paulo VI ninaweza kusema kama ilivyo mbali kijiografia, Nchi ambazo anakwenda Baba Mtakatifu anahisi sana katika moyo dharura hii.

Indonesia ni Nchi ya Kiisilamu zaidi ya watu ulimwenguni: hapo Kanisa linajibidisha katika kukuza udugu katika ushuhuda kwenye hali halisi ya wingi ambao unakabiliwa hata na matatizo ya kijamii na kisiasa. Uwepo wa Mfuasi wa Pietro unaweza kusaidia mchakato huo wa umoja?

Wale ambao Papa atatembelea ni maeneo yenye tabia za wingi wa tamaduni, madhehebu na tamaduni za kidini. Ni hali halisi kweli ya wingi! Ninafikiri kwa namna ya pekee Indonesia, mahali ambapo shukrani hata kwa Pancasila, yaani misingi mitano ambayo inasimamia Taifa, mahusiano kati ya makundi tofauti hadi sasa wameishi, msingi wa kukubaliana na kumpokea mwingine, kuheshimiana, mazungumzo na wa kiasi. Dhidi ya tabia yoyote ya kubadilisha hali hii, dhidi ya majaribu yoyote ya misimamo, kwa bahati mbaya inawakilisha kila sehemu za ulimwengu, neno la Baba Mtakatifu na ishara zake zitakuwa za nguvu na mialiko ya nguvu ya kutoacha safari na itachangia kusaidia na kutia moyo udugu , ambao kama yeye anavyopenda kusema umoja katika utofauti. Katika nuru hiyo msingi inapaswa kukabiliana hata matatizo kijamii na kisiasa ambayo yanachangamotisha sehemu kubwa ya kisiwa.

Huko Papua New Guinea, Papa atakutana na watu wa mila na tamaduni za kizamani, ambazo zina imani ya nguvu. Katika eneo hilo tajiri sana la rasilimali na maskini, mahali ambapo asili imechafuliwa, wanakabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, lakini hata na unyonyaji na ufisadi. Port Moresby inafikiriwa kuwa ni moja ya mji hatari duniani. Ziara ya Papa inapeleka mwelekeo mpya?

Ndiyo, hapakosekani hata Papua New Guinea ishara zinazopingana: kuanzia na utajiri maalum wa rasiliamali ambapo mara nyingi madhara yake ni umaskini mkubwa unaosababishwa na dhuluma, ufisadi, ukosefu wa usawa kisiasa na kiuchumi, na kama ilivyo uzuri uliochafuliwa wa uumbaji ambao unakabiliana na madhara makubwa ya mabadiliko ya tabianchi na unyonyaji kiholela wa mali asili. Papa Francisko ana nia ya kukuza nguvu kwa vote iwezekanavyo, kwa upande wa taasisi za kisiasa, za kidini, lakini pia kwa kutoa wito wa uwajibikaji wa kila mmoja, ili kuleta mabadiliko kwa maana ya jitihada hai na zinazoendelea katika mwelekeo wa haki, umakini kwa masikini zaidi na utunzaji wa nyumba ya pamoja.

Timor ya Mashariki itakuwa nusu ya tatu ya safari ya kipapa. Hapa wameishi maisha ya mateso, hadi kufikia uhuru uliotokea miaka 25 iliyopita. Mwaka ujao Nchi hiyo itaingia katika Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia(ASEAN), lakini bado inabaki na ukosefu wa msimamo sana kati ya sehemu za pembeni na katikati. Ni ujumbe gani Papa Francisko atapeleka katika eneo ambalo imani na historia zinazosukana bila kutengenishwa?

Kutokana na kufuatilia mimi binafsi Timor ya Mashariki kwenye miaka niliyo kuwa Mkuu wa Ofisi ya Katibu wa Vatican, zilikuwapo shuhuda moja kwa moja za mateso ambayo yaligusa historia. Kulikuwa na hisia kwamba ilikuwa imefungwa kabisa, hali iliyozuiwa. Kwa hivyo, siku zote nimezingatia kile kilichotokea miaka 25 iliyopita, na kupatikana kwa uhuru, kama aina ya ‘muujiza.’Imani ya wakristo ambayo kama Timor ya Mashariki kuwa Nchi ya Kwanza katoliki barani Asia, ilichukua jukumu madhubuti katika kusindikiza juhudi kuelekea lengo hili. Ninakumbusha sasa kuwa imani hiyo hiyo, hata kwa njia ya mafunzo ya kiroho zaidi ya kina, lazima ihamasishe Watu wa Timor ya Mashariki katika mabadiliko ya kijamii, kwa kushinda migawanyiko, kupendana kwa dhati dhidi ya ukosefu wa usawa na umasikini, kwa kupinga matukio hasi kama vile vurugu kati ya makundi ya vijana na ukiukwaji wa hadhi za wanawake. Uwepo wa Baba Mtakatifu utatoa kwa hakika msukumo thabiti wa maana hiyo.

Hatua ya mwisho katika safari hii itakuwa katika mji wa Serikali ya Singapore, eneo ambalo dini tofauti zinaishi kwa maelewano. Ni kwa namna gani Papa ataweza kuhamasisha kwa hakika mazungumzo ya kidini na kukuza mahusiano kati ya jumuiya tofauti za Nchi?

Singapore ni kituo cha mwisho wa safari yake ndefu, inawakilisha mfano wa amani ya kuishi katika jumuiya ya tamaduni nyingi na dini nyingi za kisasa. Tunajikuta katika Mji wa Serikali ambao unawakaribisha watu wanaotoka katika pande zote za dunia, ni mchanganyiko wa tamaduni tofauti na tamaduni za kidini na kiroho. Papa Francisko atakutana kwa namna ya pekee vijana wanaojikita katika mazungumzo ya kidini na kuwakabidhi mustakabali wa safari hii, ili waweze kuwa mstari wa mbele katika ulimwengu wa udugu zaidi na wa amani.

Safari hii huko Asia inaweza kufungua madaraja mengine na kuongeza nguvu ya mahusiano kati ya Vatican na chi za Asia?

Katika jibu la swali hili ninakwenda Singapore, ambapo watu wa sehemu  ni wa kabila la wachina na ambao kwa hiyo ni mahali pa pekee pa kufanya mazungumzo na utamaduni wa China na watu kwa ujumla. Indonesia kama ilivyosemwa ni Nchi ambayo sehemu kubwa ni Waislamu: kutembelea Jakarta kunaweza kutoa fursa muafaka kwa ajili ya kukutana na Usilam katika Eneo kubwa la Asia, lakini si hiyo tu. Nchi mbili na karibuni ya tatu kati ya nchi zilizohusika katika ziara ya upapa ni wanachama wa ASEAN, jumuiya ambayo pia inajumuisha mataifa mengine muhimu katika eneo kama vile, kwa mfano, Vietnam na Myanmar. Ukaribu na ujumbe wa amani ambapo Papa Francisko atapeleka wakati wa safari hii, ni sawa sawa na zile zinazohusu hali halisi hiyo.

Katika wakati huu mkubwa wa mivutano kimataifa kwa sababu ya vita, kwa namna ya pekee, Ukraine na Mashariki ya kati, ziara hii kwa hakika ni mbegu ya matumaini, mazungumzo na udugu. Inawezakanaje kukua uelewa wa Jumuiya ya kimataidfa na kwa dhati kujenga amani katika ulimwengu ambao utafikiri unakwenda kuelekea shimo?

Ninarudi katika muktadha wa ukaribu na ambao ni ukaribu niliosisitiza hapo mwanzo. Ili kujenga amani ni lazima kutia juhudi za kuchukua zile tabia ambazo kila hija ya kitume inapendekeza: kukutana, kutazamana machoni na kuzungunza kwa dhati. Mkutano wa moja kwa moja, ikiwa unahuishwa na utafutaji wa wema wa pamoja na siyo wa maslahi maalum na mwishowe ubinafsi, unaweza kuvunja hata mioyo isiyo na hisia na migumu na kufanya mazungumzo ya heshima na yenye kujenga iwezekanavyo.

Mahojiano na Kardinali Parolin Katibu wa Vatican kuhusu ziara ya Papa
02 September 2024, 15:55