G7:Mawaziri kwa ajili ya ulemavu watembelea Makumbusho ya Radio Vatican!
Vatican News
Wakati wa utamaduni, mshikamano na ushirikishwaji ilijionesha katika Mawaziri wa G7 wa walemavu, baada ya kumaliza mkutano na Baba Mtakatifu Francisko walitembelea jengo la Marconi, katika bustani ya Vatican, nyumba ya makumbusho ya kihistoria ya Radio Vatican. Akiwakaribisha wajumbe walioongozwa na waziri wa ulemavu wa Italia, Alessandra Locatelli, Mwenyekti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini aliwataka mawaziri hao kuendelea kufanya kazi pamoja “kwa siku zijazo ambazo kila mtu, bila kujali uwezo wake, anaweza kuhisi kuwa sehemu muhimu ya jamii kwa sababu ni kwa njia hiyo tu tunaweza kutambua, hatua kwa hatua, ndoto ya jamii ambayo hakuna mtu anayetengwa inatimia.”
Dk. Ruffini alikumbusha kwamba, takriban miaka mia moja iliyopita baada ya kuzaliwa kwa Radio Vatican, kutokana na werevu wa Guglielmo Marconi, hata leo hii, Vatican linaweka teknolojia katika huduma ya mawasiliano inayoshinda kila aina ya vikwazo. Kwa hivyo alikumbuka mradi wa “Hakuna Mtu Aliyetengwa” na Programu ya “Vatican kwa wote” ambayo inalenga hasa kukuza mawasiliano ambayo yanajali wale walio pembezoni.
Ziara ya kutembelea makumbusho ya Radio Vatican iliambatana na kifungua kinywa kilichotolewa na Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) na kuandaliwa na vijana wa “Locanda dei Girasoli,” huduma ya upishi ambayo inachanganya umakini wa vyakula bora na ujumuishaji wa ajira kwa vijana walio na ugonjwa wa Utundio wa Ubongo, ugonjwa wa Williams na ulemavu mwingine wa utambuzi. Askofu Mkuu Erio Castellucci, makamu rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) na Sista Veronica Donatello, mkuu wa huduma ya kitaifa ya CEI kwa huduma ya kichungaji ya watu wenye ulemavu na mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambaye alishiriki katika kazi ya G7 huko Assisi na Solfagnano. Askofu Mkuu Castellucci na Sr Donatello waliwashukuru mawaziri kwa kujitolea kwao kuweka kwa mara ya kwanza katika historia ya G7 - suala la ulemavu na ushirikishwaji katikati ya ajenda ya kimataifa.