Jukwaa la Sinodi:Makanisa mahalia yanatoa utajiri katika mazungumzo kupitia utofauti
Na Antonella Palermo na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatano jioni tarehe 16 Oktoba 2024, Jukwaa la nne la kitaalimungu-kichungaji lililoandaliwa katika muktadha wa Mkutano Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu kwa lengo la kuelewa kwa kina baadhi ya vipengele vya uhusiano kati ya mamlaka ya Askofu wa Roma; "kanuni ya kudumu na inayoonekana na msingi wa umoja wa maaskofu na umati wa waamini" (Lumen gentium, 23), na Sinodi ya Maaskofu, chombo kilichoanzishwa mnamo 1965 na Paulo VI lilifanuka katika Taasisi ya Kipapa ya Baba wa Kanisa Agostino. Jukwaa la Jumatano, lilifuata loe lililoakisi uhusiano wa Makanisa mahalia na Kanisa la Ulimwengu, lilifanyika katika Ukumbi Mkuu wa Wajesuit, huko Roma.
Kwa njia hiyo "Uhusiano wa pande zote kati ya Kanisa maalumu na Kanisa la Ulimwengu" ndiyo ilikuwa mada elekezi ya maingiliano yaliyosimamiwa na Profesa Anna Rowlands, mshiriki wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu. Wazungumzaji walikuwa ni baba na mama wa mkutano wa Sinodi, akiwemo Profesa Antonio Autiero, Padre kutoka Jimbo kuu la Napoli; Profesa Myriam Wijlens, mwanasheria wa kanuni za Kiholanzi na mtalimungu, mshauri wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi; Profesa Miguel de Salis Amaral, padre wa Kireno na mshauri wa kitaalimunu wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kutawangaza watakatifu na, Kadinali Robert Francis Prevost, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu.
Utajiri katika utofauti
Kardinali Prevost alielekeza uingiliaji kati wake katika mang’amuzi mawili binafsi yanayohusiana na malezi yake ya kiaskofu. Wakati wa kozi ya malezi ya kichungaji huko Roma mwaka 2011, iliyoandaliwa na "Baraza la Kipapa la Maaskofu" wakati huo, alikumbuka "msisitizo juu ya jukumu la askofu katika kusaidia watu mahalia kutazama zaidi ya mipaka ya majimbo, kupanua mtazamo wao wa kukuza kuelewa maana ya kuwa sehemu ya Kanisa." Pia alikumbuka kwamba maaskofu wapya kutoka Asia na Afrika walikuwa wakihudhuria kozi tofauti huko Roma baada ya kuchaguliwa kwao. Hata hivyo, alisema Kardinali huyo, “mwaka huu kozi hiyo ilipangwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya Mabaraza ya Kipapa husika ili kila mtu aweze kukutana.”
Kardinali Prevost alishirikisha tathmini ya mbinu mpya ya kufundisha, ambayo ilipokelewa kwa shauku kubwa kwa kutoa "uzoefu wa asili ya Kanisa kwa ujumla ambao haukuweza kupatikana katika muundo mwingine wowote." Fursa ya kuketi na maaskofu kutoka duniani kote, "kuweza kufanya mazungumzo tu" ilifanya kujifunza "kukumbukwa." Makanisa ya watu wa Asili alisema, si "sehemu tu" za Kanisa la ulimwengu, ambalo linawakilisha "jumla ya yote." Badala yake, kila Kanisa maalum huleta upekee na utajiri kwa Kanisa la kiulimwengu kama sehemu ya “utu wao wa ajabu” wa jumuiya mbalimbali.
Kanisa linaloishi sehemu zote
Akizungumza na Vatican News baadaye, Kardinali Provost alisisitiza umoja wa mwili wa Kristo ndani ya Kanisa. "Katika historia ya Kanisa, uundaji wa jumuiya za mahalia umekuwa ukweli katika maeneo mbalimbali, lakini daima kwa kuzingatia Kanisa moja la Kristo. "Lazima tusijaribu kuelewa hili kama suala la hisabati au jiografia, lakini kuliona katika kiwango cha ndani zaidi cha ushirika. Kanisa linaishi sehemu zote."
Watu wote wa Mungu
Padre Miguel de Salis Amaral alithibitisha kwamba mahusiano yote, ikiwa ni pamoja na yale yaliyochunguzwa katika Jukwaa, yamejengwa juu ya mienendo inayokuzwa na Sinodi ya sasa, akimulika umuhimu wa uhusiano unaofungamanisha ukweli mbalimbali wa kikanisa. Padre wa Kireno alibainisha kwamba Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican uliashiria ufunguzi wa kwanza katika mwelekeo huu, akimaanisha Makanisa ya mahali kama "sehemu ya jumla," na akimaanisha jumuiya ya kikanisa ya ulimwengu wote, na wakati huo huo, "yapo na yanafanya kazi katika nzima." Akinukuu kifungu cha Lumen Gentium, kuhani huyo alisisitiza kwamba "katika kila Kanisa mahalia" hukaa "nguvu, utajiri wa karama zote za sakramenti na kiroho."
Padre Miguel alitoa mfano wa uhusiano huu ka mfano wa kipande cha keki. "Katika kila sehemu, kuna ladha yote, watu wote wa Mungu," alibainisha. Kwa kumalizia, profesa huyo alibainisha muktadha wa sasa wa kimataifa, unaojulikana na "polarization, ubinafsi, vita, na utandawazi ambao hutufahamisha tu kuhusu sehemu ya ukweli, lakini sio daima hutuunganisha." Akikabiliana na hali hii, alisema, "wachungaji" wanaitwa kusisitiza "Kanisa" na nyanja zake mbalimbali "ambapo kweli uhusiano wa kibinadamu, uwazi kwa wengine, huishi."
Ukuu wa Jumuiya mahalia
Fr. Autiero kisha alisema kwamba "Kanisa mahalia, katika maelezo yake" inawakilisha "mahali ambapo tunaweza"kupta uzoefu wa "sinodi na maisha ya kimisionari ya Kanisa zima." Padre huo huyo alisema suala la uhusiano kati ya jamii za wenyeji na zima linahusishwa na uainishaji wa dhana ya mahali. "Mahali ni kubwa zaidi," alisema, akiongeza kwamba "mahalia" inawakilisha upeo wa mtazamo "ambapo mafunzo tofauti hukutana, yakiunganishwa na nia ya pamoja, matarajio ya kawaida" ya Kanisa. Tabia ya mahalia haiwezi , kupunguzwa kwa kipengele cha pili lakini, kinyume chake, "inaingia ndani ya kitu kizima cha kikanisa. Ingawa uzoefu wa mtu binafsi wa Kanisa kimsingi ni wa kawaida, kila mtu anaweza kutumia "kanuni ya umoja" ingawa sura ya Askofu wao wa eneo na ushirika wake na Kanisa la ulimwengu wote. Mifumo ya kikanisa mara nyingi "huhojiwa na kupingwa" na madai haya, ambayo "hayaitii tu marekebisho ya kiutaratibu au maboresho ya kando kwa mazoea yetu yaliyoanzishwa," lakini badala yake inasisitiza katika dhamiri "hitaji la uongofu, wa uhusiano na wa muktadha."
Mfano wa Australia wa mabaraza ya majimbo na wajumbe wote
Uingiliaji kati wa Profesa Wijlens ulilenga aina mbalimbali za mabaraza ya kichungaji ya kijimbo na parokia, pamoja na mabaraza ya mashauri. Alibainisha kuwa "watu wa Mungu" wanatarajia "mengi zaidi; wanatamani kanuni za kisheria ziwabadilishe kuwa vyombo halisi vya Kanisa la kisinodi, kuwaruhusu kushiriki katika huduma ya ufalme wa Kristo."Kando ya mabaraza ya majimbo kuna mabaraza ya jumla, yenye sifa ya "ushirikiano uliopangwa" na yenye uwezo wa "kuonesha mawazo ya ukatoliki, hata kwa Kanisa zima." Profesa Wijlens aliwaweka katikati kati ya jumuiya zawatu wa asili. Maaskofu wote hai katika eneo maalum hushiriki, lakini makundi mengine kadhaa ya watu "wanaweza na wanapaswa kualikwa," ikiwa ni pamoja na mapadre, maaskofu, wakuu wa seminari, wakuu wa vitivo vya taalimungu na hata mashirika ya kidini
Mtaalimungu wa Uholanzi alitoa mfano mbadala katika uzoefu wa Kanisa la Australia, "ambalo hivi karibuni lilifanya Mkutano Mkuu katika muktadha wa "mgogoro mkubwa kutokana na kashfa za nynyaso za kijinsia." Maaskofu "walihisi hawawezi kurejesha imani katika Kanisa peke yao," na hivyo wakawaita waamini wote "kuchukua hatua, ili waweze kuibuka pamoja." Ushiriki mpana zaidi wa washiriki "walioalikwa" ulitolewa kupitia "msaada kutoka Vatican," na kuleta pamoja muundo wa maaskofu 44 na waamini 275. Profesa Wijlens alibainisha kwamba "maamuzi yalifanywa kikamilifu hata na washiriki wasio maaskofu," na akaelezea matumaini yake kwamba taasisi kama hizo zingeweza kubadilishwa kulingana na mahitaji katika Makanisa mengine.