Tafuta

Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. 

Kard.Fernández:Tufanye kazi ili kuwapa wanawake nafasi na madaraka

Wakati wa mkutano wa Sinodi ya alasiri tarehe 24 Oktoba 2024 pamoja na washiriki wa kikundi kazi cha 'Kundi la 5',Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa,alieleza kwa nini hawakuzingatia uamuzi wa ushemasi wa kike kuwa'mkomavu,'akisema kuwa haimaanishi kuzima uwezekano."

Na Andrea Tornielli

Saa moja na nusu ya mazungumzo ya bure, ya kindugu na ya wazi yalifanyika katika Sinodi ya kisinodi katika Ukumbi wa Paulo VI alasiri Alhamisi tarehe 24 Oktoba 2024. Mkutano huo ulifuatia hatua ya mpango wa Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa,  Juma lililopita, ambapo uwepo wa maofisa wawili wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa (DDF) ulisababisha baadhi ya watu kutoridhishwa na kutokuwepo kwake, hata kama ingetangazwa kabla ya muda kuwa hawezi kuhudhuria kutokana na ahadi za awali.

Kwa njia hiyo Siku ya Alhamisi,24 Oktoba,  Kardinali Victor Manuel Fernández alishiriki katika mkutano na washiriki wapatao 100 wa Sinodi, wakiwemo wanachama, wageni, na wataalam, kusikiliza maswali yao, kupokea mapendekezo na kutathmini kazi ya 'Kundi la 5', ambalo katika Baraza Hilo( DDF) linashughulikia suala la uwezekano wa huduma kwa wanawake. Kardinali, kwa kukubaliana na Sekretarieti ya Sinodi na washiriki katika mkutano uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa  la Mawasiliano, Dk. Paolo Ruffini, aliamua kuweka rekodi kamili ya sauti kwa umma kwa kipekee kwa kuzingatia sheria za Sinodi. Kwa hiyo  sauti hiyo imetolewa hapa kwenye tovuti za Vatican News, baada ya pendekezo la kuichapisha kupokelewa na makofi kutoka kwa washiriki hao. Rekodi kamili ya sauti ya mazungumzo na Kardinali Fernandez pia tunaitafsiri katika lugha ya kiswahili kwa kuelezea kile kilichojiri:

Kazi ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa

Katika sehemu ya kwanza ya mkutano huo, Kardinali Fernandez alieleza jinsi gani Baraza lake lote—ambalo jukumu hili lilikabidhiwa mahususi hata kabla ya Sinodi—limejitolea kuimarisha mada ya jukumu la wanawake na kuchunguza uwezekano mpya wa huduma zinazotolewa kwao. Kisha akasimulia jinsi wanavyofanya kazi, akianza na (Consulta-ushauri), yaani, kusikiliza mapendekezo ya kundi kubwa la washauri wanawake, kundi ambalo katika kesi hii limepanuliwa kwa kuomba maoni na kusikiliza uzoefu mbali zaidi ya washauri rasmi wa Baraza la Kipapa. Mikutano miwili ya kawaida ya Makardinali na Maaskofu wa Baraza la Kipapa tayari yamefanyika (Feria quarta,) kwa sababu kawaida hufanyika siku ya Jumatano), na kazi hiyo inaratibiwa na Katibu wa Kitengo cha  Baraza la Kipapa la  Mafundisho  Tanzu ya Kanisa, Padre Armando Matteo.

Uzoefu tayari unaendelea

Kardinali Fernandez alisisitiza kwamba njia ya kufanya kazi ni sinodi, na uwepo wa Maaskofu na Makardinali kutoka pande zote za dunia ina maana kwamba kazi ya ‘Quarta ya Feria’ inazingatia hisia na tamaduni mbalimbali. Pia alisisitiza kwamba wajumbe wa Sinodi wametakiwa kupeleka michango na mapendekezo, pamoja na kutilia maanani uzoefu ambao tayari unaendelea na kuwaona wanawake wanasimamia jumuiya zinazoongoza, kwa mfano Amazoni, lakini pia Afrika na Asia. Kwa usahihi ili kusisitiza umuhimu wa kuanza kutoka katika ukweli, i.e. kupata kujua na kuthamini uzoefu ambao tayari unaendelea ambao labda haujulikani au unajulikana kidogo na taalimungu ya Ulaya. Kwa hivyo barua za mashauriano bado zitatumwa kwa watu na taasisi zingine.

Kutambua jukumu

Lengo la msingi la kundi hilo, Kardinali alieleza, ni nafasi ya wanawake katika Kanisa, si hasa uwezekano wa ushemasi wa kike, ambao tume inayoongozwa na Kardinali Giuseppe Petrocchi bado inafanyia kazi. Kardinali Fernandez alisema kwamba, wanawake wanataka kusikilizwa na kuthaminiwa: wanaomba kuwa na mamlaka na kuendeleza karama na uwezo wao, lakini wengi wao hawaombi ushemasi, yaani, hawaombi ‘ukleri’. Hii ndiyo sababu kazi ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  ni kuendelea wakati huo huo kwa hatua 'madhubuti' kwenye njia hiyo. Alisema ni jambo la msingi kuchunguza tofauti kati ya Daraja Takatifu na madaraka, ili kuweza kuwakabidhi walei na hivyo wanawake pia kuwa na nafasi za uongozi katika Kanisa—njia ambayo inawezekana kuwa na maafikiano makubwa. Mkuu huyo wa Baraza la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  kisha akauliza swali: Ikiwa inatokea kwamba zamani wanawake walihubiri wakati wa adhimisho la Ekaristi au walitumia mamlaka bila kuwekwa shemasi, je, hii labda inahesabiwa kuwa ndogo?

Ushemasi, utafiti unaendelea

Kardinali Fernandez aliendelea kusema kuwa kuhusu mada mahususi ya ushemasi, tume inayoongozwa na Kardinali Petrocchi itaanza tena kazi yake kwa nguvu zaidi, ikisikiliza mapendekezo ya mkutano wa sinodi na wengine kutoka sehemu mbalimbali za dunia: mapendekezo na maoni hayo yaweza kutumwa kupitia Sekretarieti ya Sinodi. Kardinali alibainisha katika  hotuba yake katika ukumbi wa Sinodi, ambapo alitoa muhtasari wa msimamo wa Papa kuhusu suala hilo. Alisisitiza kwamba kusema kwamba ‘uamuzi juu ya ushemasi haujakomaa’ haimaanishi kwamba Papa Francisko anataka kulifunga suala hilo, bali aendelee kusoma, ikizingatiwa kwamba mahitimisho ya kazi ya tume hiyo si ya sauti moja. Mkuu pia alieleza kuwa kuna wanahistoria ambao kulingana na wao hapo zamani kulikuwa na kesi za wanawake waliowekwa wakfu, wanahistoria wengine ambao kulingana na wao ilikuwa ni baraka na sio kuwekwa kiukweli.

Hatua thabiti

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  alihitimisha kwa kusema ana hakika kwamba tunaweza kusonga mbele kwa hatua zilizo wazi na madhubuti zinazowawezesha wanawake katika Kanisa, kwa kuanzia na kutofautisha kile ambacho hakitenganishwi na Daraja Takatifu na kisichoweza kutenganishwa. Hatimaye, alitoa wito kwa wale waliohudhuria wawe na moyo wazi ‘ili kuona mahali ambapo Roho Mtakatifu anatuongoza.’

25 October 2024, 14:53