Kard.Marengo aongoza misa ya shukrani ya kutangazwa Mtakatifu Yoseph Allamano!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu jioni, tarehe 21 Oktoba 2024, yalifanyika maadhimisho ya misa takatifu katika Basilika ya Mtakatifu Paulo nje ya Ukuta, ikiwa ni misa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutangazwa kuwa Mtakatifu Joseph Allamano, mwanzilishi wa Wamisionari wa Consolata; Sr Elena Guerra, mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Oblate wa Roho Mtakatifu; Sr Marie-Léonie Paradis, mwanzilishi wa Masista Wadogo wa Familia Takatifu na wafiadini kumi na mmoja Ndugu wadogo (11) wa Damasco waliouawa mwaka wa 1860 Manuel Ruiz López na Wenzake saba na Francis, Mooti na Raffaele Massabki, walei waamini wa Maronite. Dominika tareh 20 Oktoba 2024 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican, sambamba na Siku ya 98 ya Kimisionari Ulimwenguni. Kwa njia hiyo katika Misa hiyo iliongozwa na Kardinali Giorngio Marengo Mwakilishi wa Kitume wa Ulambaatar nchini Mongolia, kwa kuudhuriwa na Maaskofu wa Shirika la wa Consolata, Mapadre, Watawa wa kike na kiume, manovisi, waamini wa chama cha Waconsolata walei kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Akianza mahubiri mara baada ya masomo yaliyochaguliwa kuongoza shukrani hiyo, Kardinali Marengo.
Yafuatayo ni mahubiri kamili ya Kardinali Marengo.
Leo yametimia maandiko haya ambayo ninyi mmesikia.” Leo ni siku ya kutumiza. Leo tuko hapa katika kaburi la Mtume wa Watu, ili kumshukuru wote pamoja kwa zawadi kubwa ya utakatifu wa Yosefu Allamano, mwanzilishi wetu. Ni leo ya wakati unaondelea, unaouhisha Kanisa. Leo ni Pasaka. Leo ni Penekoste. Leo ni siku ambayo mitume kwa kubadilishwa na kukutana na Mfufuka, wanatoka Yerusalemu kutembea katika barabara za ulimwenguni. Liturujia ya leo inafanya kuwa wakati huu, sasa na unaoendelea. “Mungu ananiita leo hii, sijuhi kama ataniita kesho,” mnakumbuka mwanzilishi alipokuwa akifanya mang’amuzi wa wito wake. Utafutaji huu wa kila mara wa mapenzi ya Mungu, umakini huu wa kutimiza kazi yake , ulikuwa ishara ya maisha yake daima, na unatualika kufanya hivyo.
Ni wakati uliopita na uliopo unaruka umbali. Leo, Mtakatifu Yoseph Allamano, na Mtakatifu Paulo Mtume! “si mimi ninaye ishi, bali Kristo anaishi ndani mwangu.” Kuhusiana na hili, Mwanzilishi alikuwa anasema, na nukuu katika barua kwa Wagalatia: “kufanya kila njia inayowezesha maneno ya Mtakatifu Paulo.” Mtakatifu Paulo alikuwa zaidi ya kinyago. Tazama jinsi ilivyo nzuri. Inahitaji kufanyia tafakari. Hilo ndilo wazo ambalo, sisi kama Wamisionari ,tunapaswa kuwa zaidi ya kinyago, kuwa wazi katika uwepo wa Bwana. Nguvu ya Utume wa kimisionari, inachota katika kutafakari wakati uliopita na unaondelea kama inavyosema liturujia.
Kuna hata neno jingine lenye nguvu lililosikika katika Injili ambalo linaweza kutusaidia: “Utume wa Kimisionari, unatimizwa kiukweli kutokana na kuwa na mtazamo juu yake. Kama ilivyokuwa kwa wote, siku ile kwenye Sinagogi, walivyokuwa wakimazima macho Yeye, ili kuweza kujua namna ya kuwaelekea wengine, kwa ukaribu, huruma na upole, aliyasema jana Papa Francisko. Ekaristi ya kila siku ilikuwa daima ikimzugunguka, yaani ikuzungukia maisha ya Mtakatifu Yoseph Allamano. “Huu ni Mwili wangu, hii ni Damu yangu, Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Na roho ya aliuunda moyo wa Mtakatifu Yoseph Allamano, kwa kuruhusu kuwa chombo safi katika mikono yake. Katika wakati unaoendelea wa leo, wa sasa. Fumbo lililoadhimishwa katika liturujia, ni nguvu inayonyanyua wakati uliopo. Ni leo ya wakati uliopita wa kuchota nguvu ya umisionari kutoka wakati uliopita na sasa kwa matendo. Yeye alikuwa anatueleza kuwa, ninanukuu: “Tuache tuzungukwe. izunguke talanta yake,kwa namna ya kwamba tutakuwa watakatifu wa kweli wamisionari.
Ninataka kunukuu tena, neno la Mwanzilishi katika fursa maalum, ambayo ilikuwa tarehe 24 Januari 1905 kwatika Nadhiri za watawa wawili wamisionari, wakiwa wanaondoka ambapo yeye alisema hivi: “ Bwana wetu Yesu Kristo kutoka katika altare hii, anawambia ninyi wana wapendwa, maneno makuu ambayo alisema siku moja kwa mitume ‘Nendeni, mkahubiri watu, mkawabatize, tazama mimi nitakuwa nanyi siku sote.’! Haya ni maneno sawa aliyowaeleza daima kwa karne. Na kwa watu wengi wa kitume ambao waliitwa naye na kupewa utume sawa kwa ahadi sawa, alikuwa anaongeza: “Leo maneno haya ni kwa ajili yenu mliobahatika, wana wa Consolata, kwa ajili ya ndugu zenu waliowatangulia na wale watakaowafuata, utume wenu ni ule ule, utume wa Bwana wetu Yesu Kristo, Utume wa kimungu, ”mwisho wa kunuu.
Kwa njia hiyo wapendwa kaka na dada, leo tuwe na mtazamo kuelekea kwake. Moja ya mambo yanayoeleza utakatifu wa Joseph Allamano kwa kujua ni kwa jinsi gani inabidi kupata hata sisi pamoja Naye katike eneo la kusali kwenye madhabahu ya Consolata, ni ile ya kuweza kukaa kwa masaa marefu huku akikazia kwa macho yake juu ya Taberkulo, na juu ya Picha ya Consolata, kwa kutumia muda wa kusikiliza wana na binti wa kiroho, na kama ilivyokuwa kwa watu wa kawaida waliokuwa wanakuja katika madhabahu ili kupata ushauri; ile ya kuweza kushirikishana na mwenzake, ndani ya nyumba ya kikuhani Yakobo Camisassa, na watu wengine wanawake wa masaa ya kwanza, wasiwasi na matumaini ya familia moja ya kimisionari iliyokuwa inazaliwa. Hata sisi tunapaswa kuwa na ujasiri wa kufunga nyumba ya kwanza ya malezi (Consolatina yaani Consolata ndogo) na kupeleka ufunguo kwa Consolata hadi kuwa na uhakika wa muundo wa makandidate kwa ajili ya utume. Tunapaswa hatakuwa tumehangaika, kutokuelewana na hata kutengwa ambako tunafanyia uzoefu kwa miaka ya mwisho ya maisha.
Tazama kwa watakatifu hakuna umbali , kuna ile ya uendelezaji wa wakati uliopita na uliopo . Fumbo lilioadhimishwa ni nguvu inayotuchoche ya leo hii. Kuwa leo hii hapa, ili kuweza kutumwa ulimwenguni. Kwa njia hiyo watakatifu wanajiachie Roho awape wao nguvu kwa mtindo anaoutaka. Kwa Joseph Allmano, pamoja na sisi, ni mtino wa utume wa Ad Gentes (Utume wa Watu). Uinjilishaji wa kwanza, mahali ambapo Mktadha wa Kanisa ulikuwa bado haujasimika mizizi, na hapakuwapo na wengine mashuhuda wa Mfufuka. Kwa mtindo wa Maria, na mtindo huo unaoishi kwa ukaribu, katika huruma na katika upole. Ni kwa jinsi gani Mtakatifu Yosefu Allmanao alikuwa anazingatia umakini wa kupendana kati yetu.
Alikuwa anauzingatia kama kipaumbele yaani kitovu cha umakini unaoendelea. Hapa na sisi tumo. Kwa hiyo tunaweza kujiuliza: Wakati uliopo unatueleza nini katika utakatifu wa Baba Mwanzilishi? Inatujia kusema kwamba, ikiwa hatuzingatii kwa usahihi mwaliko huo wa kuwa na mtamamo wa dhati kwa Bwana wetu, aliye katikati yetu, ikiwa hatujali leo hii, ambayo ina uwezekano wa kupendana sisi kwa sisi kweli, bila mantiki za vikundi, bali kwa maelewano ya kweli kati yetu sisi, utakatifu wa Joseph Allamano, labda hautaweza kusaidia sana. Iwapo hatuanzi leo hii na daima safari ya kweli na dhati ya uongofu binafsi, ya kurudi kwa Bwana, ya ufunguzi wa Kanisa ambalo linatutuma, na mahali ambapo kuna mahitaji, labda tunaweza kusema haitasaidia hata kuwa na Mwanzilishi kutangazwa Mtakatifu. Ndiyo tunapaswa kusema haya kwa ukweli, utakatifu wake lazima ututafakarishe, la sivyo hatutafaidika.
Taasisi zetu zinapitia kipindi nyeti katika historia yake, inayoshirikishwa na kutokuwa na uhakika na maendeleo ya haraka katika ulimwengu. Leo hii, kitovu cha kufika, kinapaswa kiwe wakati wa kuanzia safari. Shauku ya upendo wa Baba Mwanzilishi aliyoionesha tangu kizazi cha kwanza cha wamisionari wa kike na kiume, kazi kubwa ya kimisionari iliyopelekwa mbele na Ndugu wengi, kaka na dada, ambao leo hii tunawakilisha, jitihada za michakato ya kutangazwa, na maandalizi, yote yatalipwa kwa upande wake ikiwa yote yatachukuliwa kwa umakini wa ‘leo hii’ na kuwa na kukazia mtazamo wa kina kwa Bwana, ambaye kwa upole alipendwa na kuhudumiwa na Mtakatifu Joseph Allamano.
Tutatimiza kweli shauku yake ya kutoa, kama familia ya Consolata wanaopendana, ambao wanataka ari ya kitume. Siku hii iliyobarikiwa, itusaidie kugundua mshangao, uaminifu mbunifu, zawadi ya kuwa wamisionari wa CONSOLATA wanaotumwa mahali ambapo labda wengine hawahisi kwenda ili pazewekane kwa dhati kukutana na Kristo, kwa kuiga hivyo Mama wa Mungu, ambaye alichukuliwa kwtu kati ya mambo mazuri zaidi kujifunza kutoka kwake. Asubuhi ya leo katika sehemu ya Mkutano wa Sinodi, nimependelea kwenda kumshukuru Baba Mtakatifu aliyekuwa nasi, kwa ajili ya zawadi ya kuwatangaza watakatifu. Nimeshangazwa Naye nikiwe niemekaa mbele yake, alinishika mikono yangu na kuniambia: “kuwa jasiri, nenda mbele,” kama kile alichokuwa anatuambia Mtakatifu Yoseph allamano. Kwa njia hiyo tuseme daima kwa upya nunc cepmus, yaani “tunze sasa,” “tuanze leo.”Tazama, sisi ni Watumishi wa Bwana tutendewe kama ulivyonena!
Mara baada ya Mahubiri na kuhitimishwa kwa misa, wimbo wa Bikira Maria wa kummtukuza Bwana, uliimbwa na manovisi na masisita wa Consolata. Baadaye Vatican News, ilipata kuzungumza na mmoja wa Maaskofu wa Consolata kutoa Jimbo katoliki la Isiolo nchini Keny Askofu Peter Manguti Makau, na baadaye Dk Catherine Shao, Mwakilishi wa Walei wa Consolata Tanzania kutoka Parokia ya Kigamboni, jijini Dar Es Salaam. Kwa hakika walikuwa ni waamini wengi kutoka ulimwenguni kote.
Je unawajua maaskofu wa Shirika la wamisionari wa Consolata?
Hawa ni Kardinali, Maaskofu wakuu na Maaskofu wa Shirika la Kimisionari la Consolata:
1.Kardinali Giorgio Marengo, Mwakilishi wa Kitume wa Ulaambaatar nchini, Mongolia
2. Giovanni Crippa wa Jimbo la Ilhéus, nchini Brazil
3. Askofu Elio Rama wa Jimbo la Pinheiro, Brazili
4.Askofu Mkuu Joaquín Humberto Pinzón Güiza, Msimamizi wa Kitume wa Puerto Leguízamo– Solano,Jimbo la Kikanisa la Florencia, nchini Colombia
5. Askofu Mkuu Francisco Javier Múnera Correa, wa Jimbo kuu la Cartagena, Colombia
6. Askofu Hieronymus Joya Jimbo la Maralal nchini Kenya
7. Peter Kihara Kariuki wa Jimbo la Marsabit nchini Kenya
8. Askofu Anthony Ireri Mukobo, Askofu Mstaafu Jimbo la Isiolo, Kenya
9. Peter Munguti Makau Jimbo la Isiolo, nchi Kenya
10 Askofu Virgilio Pante, askofu Mstaafu wa Maralal nchini Kenya
11.Askofu Osorio Citora Afonso, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Maputo, Msumbiji
12. Askofu Mkuu Inácio Saure wa Jimbo Kuu la Nampula nchini Msumbiji
13. Askofu Diamantino Guapo Antunes wa jimbo la Tete, nchini Msumbiji
14. Askofu José Luis Gerardo Ponce de León wa Jimbo la Manzini nchin Eswatini.
15. Askofu Lisandro Alirio Rivas Durán Askofu Msadizi wa Jimbo Kuu la Caracas, nchini Venezuela.